Kama ambavyo mtoto anayejifunza kutembea anavyosaidiwa na vigari, huku mwenyewe akiwa anajitengenezea nguvu za kutembea kwa miguu yake mwenyewe, ndivyo msomaji wangu utakavyofaidika na Maarifa na Mbinu nitakazo share na wewe kwenye ukurasa wangu.

Kwa miaka kadhaa kwenye maisha yangu ya kusoma, nimebahatika kukutana na watu wanaojua vitu, watu ambao wana akili za asili na ndio watu ambao haswa walinifunza maarifa na mbinu zilizomo kwenye ukurasa wangu.

Kwa miaka kadhaa nimezitendea kazi nadharia nilizojifunza, kufundishwa na kisha kuwafundisha wengine, Maarifa na mbinu hizi hazimpi msomaji vitu vya kukariri wala amri za lazima uwe useme hivi uishi hivi, ama lazima uwe hivi ama vile unapoishi, hasha!

Mbinu na maarifa yaliyomo kwenye ukurasa wangu huu yanalenga kumsaidia msomaji wangu kutengeneza "personality" yake ambayo itamsaidia kuwa na Ujuzi(skills) na Maarifa ambayo kiuhalisia ni yamelenga kumsaidia msomaji kujijengea taratibu zake nwenyewe zitakazomsaidia kuishi maisha tofauti na alivyokuwa kabla ya kujifunza.

Kama ambavyo baadae mtoto ataanza kutembea mwenyewe kwa miguu yake mwenyewe, ndivyo ambavyo Maarifa na Mbinu zilizomo kwenye ukurasa wangu huu zitakavyokusaidia msomaji wangu.

Karibu. click here to unlock the post