

WAKALE. @wakale
Picha ya kwanza inayokujia kichwani ukiskia “msanii maarufu”
*Ni mtu anaye heshimika,
*Mwenye maisha ya anasa,
*Anaependwa na wengi
*Anafuraha na anaishi maisha yake anavyotaka.
Lakini si kweli!! angalau naweza kusema hivyo juu ya msanii huyu tutakaye mzungumzia leo.
Leo tutaangalia maisha ya msanii maarufu wa dunia, aliyeishi maisha yake kinyume na yale yote tunayo shabihisha na usanii.Na chenye utata zaidi kuliko maisha yake ni kifo chake.
KWA TSH 1000 TU!! UNAPATA ACCESS YA MKASA MZIMA TAKRIBAN PAGE 40
ENDELEA KUSOMA HAPO CHINI
click here to unlock the post

WAKALE. @wakale
Unit 731_UTAFITI WA KIKATILI ULIOWAHI KUFANYIKA KWA BINADAMU (JAPAN)
Historia ya vita vya Japani na serikali ya Japan iliyopelekea kuundwa kwa Unit 731 ni ndefu sana, lakini nataka tuzingatie yale yanayohusiana na Vita vya Pili vya Dunia.
Mwaka 1925, Mkataba wa Geneva ulipiga marufuku matumizi ya silaha za kibaiolojia na kemikali. Sababu kubwa ya hii ni kwamba wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, moja ya mambo mabaya zaidi ya vita vya mahandaki ilikuwa matumizi ya silaha za kemikali. Na ingawa mkataba huu uliwazuia mataifa kadhaa kutumia silaha hizo kabisa, si kila nchi ilikubaliana na sheria hiyo moja wapo ikiwa Japan
Sasa, kama tutakavyoona muda si mrefu, Japan haikuwa na mchezo linapokuja suala la ukatili. Na kuhusu silaha za kemikali na kibaiolojia,na kupigwa marufuku hakumaanisha hawatazitumia, ilimaanisha watazitumia kwa ujanja sana.
Katika miaka ya 1930, watafiti wa Kijapani walianza kuchunguza uwezekano wa kutumia vita vya kibaiolojia. Na kwa kuweka wazi, vita vya kibaiolojia hapa tunazungumzia kutengeneza magonjwa kama silaha, au kutumia maambukizi kama njia ya kushambulia maadui.
Kuhusu utafiti huu kulikua na Tatizo, kwa mtazamo wa serikali ya Japani, changamoto ni kwamba huwezi kujua kama silaha za kibaiolojia zinafanya kazi vizuri kama huna watu wa kujaribia hizo silaha. Na pia, katika kipindi hicho cha miaka ya 1930, Japan ilianza kuvamia bara la China.
Kwa wakati huo kihistoria, China ilikuwa inahaha kuingia katika ulimwengu wa kiteknolojia, na sehemu kubwa ya jeshi lake lilikuwa na makundi madogo ya wapiganaji wa kijamii waliokuwa wanajitahidi kupigana kwa hali na mali. Lakini kwa upande mwingine, Japan ilikuwa na jeshi kubwa na hatari sana. Ndio maana uvamizi wa China unaitwa ‘ushindi wa mabavu’ kwa sababu Wachina walijaribu kupambana kadiri wawezavyo lakini kila wakati walikuwa wanapigwa vibaya na Wajapani.
Kwa hiyo tunaona vipande vya mchezo vinaanza kupangwa…Japan inavutiwa na vita vya kibaiolojia na kemikali, wanaanza kuingia China kwa nguvu, na kumbuka, haya yote yanatokea takriban muongo mmoja kabla Vita vya Pili vya Dunia kuanza.
Wakati huu, daktari mkuu wa upasuaji wa Kijapani, anayeitwa Shiro Ishii, akaja na pendekezo kuwa Japan inapaswa kuwekeza kwenye vita vya kibaiolojia. Alisema, "Hili jambo linakuja, vita viko njiani, na kama hatuchukui hatua mapema, basi Marekani au mataifa mengine yataanza kabla yetu."
Serikali ya Kijapani ilikubaliana na hii idea ya "mashindano ya silaha za kibaiolojia" na mwaka 1932 wakamteua Ishii kuwa mkuu wa maabara ya jeshi ya kuzuia magonjwa ya mlipuko. Juujuu, maabara hii ilisemekana kuwa inatafiti tiba za magonjwa yanayoweza kuathiri wanajeshi vitani. Lakini kiundani, walikuwa wanatafuta njia za kufanya magonjwa yaathiri majeshi ya maadui.
Chini ya mpango huu, kulikuwa na tawi maalum ndani ya maeneo yaliyodhibitiwa na Japan huko China, ambalo lilijulikana kama Kitengo cha Togo, na lilikuwa sehemu ya mpango huu wa vita vya kibaiolojia.
Na kitu kingine cha muhimu kukumbuka hapa ni kwamba, wakati huu kihistoria, Japan ilikuwa na dharau kubwa kwa yeyote ambaye hakuwa Mjapani. Imani ya kwamba wao ni bora ilikuwa na nguvu kiasi kwamba walihalalisha dhana ya kuwa wao wana haki ya kutawala na kudhibiti wengine.
Hii ndiyo sababu wanajeshi na viongozi wa Kijapani waliona yeyote anayewapinga kuwa si binadamu mwenye hadhi sawa na wao…au sio binadamu kabisa. Na kama unakumbuka nilivyosema awali, huwezi kujaribu silaha za kibaiolojia kama huna watu wa kuzifanyia majaribio...
Kwa hiyo, kikosi cha Togo kiliona njia bora kabisa ya kujaribu silaha hizi mpya na idea yao mpya ilikuwa kwa kutumia wakazi wa China kama panya wa majaribio.
Mwanzo, utafiti huu ulifanyika katika eneo lililojulikana kama Ngome ya Zongma. Ngome hii ilikuwa jengo la zamani lenye muundo wa kasri huko Manchuria, China, ambalo liligeuzwa kuwa kituo cha majaribio cha kikosi cha Togo.
Majaribio ya awali katika Ngome ya Zongma yalihusisha kuwakamata raia wa kawaida kutoka China na kuwafungia katika vyumba vilivyobadilishwa kuwa magereza.
Mwanzoni, mateka walikuwa wanapewa chakula cha kutosha na kuhakikisha afya nzuri, waliwapa chakula si kwamba walikua wanawajali bali ilikuwa ni hatua ya kwanza ya utafiti, lengo lilikuwa waanze majaribio na watu wenye afya na nguvu.
Baada ya hapo, majaribio yenyewe yalianza, watafiti waliwafanyia vitendo vya kikatili kama kuwavujisha damu polepole kwa siku kadhaa, kuwaacha na kiu au njaa ili kuona miili yao ita react vipi na kujua ni muda gani mtu anaweza kuishi bila maji au chakula.
Kila kitu kilifanywa lengo la "kuelewa ni jinsi mwili wa binadamu unaweza kustahmili mateso”
Ukiachana na hayo, mateka walikuwa wanapatiwa magonjwa kama pigo jeusi (Bubonic Plague), na katika hatua tofauti za maambukizi, walikuwa wanavunjwa viungo vyao au kufanyiwa upasuaji wa bila ganzi. Hii ilikuwa kwa lengo la kuona kwa macho yao wenyewe jinsi magonjwa haya yanavyoshambulia mfumo wa ndani wa mwili wa binadamu.
Na huu ulikua ni mwanzo tu, mambo mengi mabaya na ya kikatili yanakuja...
Hali katika Ngome ya Zongma ilikuwa yakutatanisha. Kumbuka, wakati huu walikuwa ni wanasayansi waliokuwa wakifanya majaribio haya, na sio wanajeshi. Japokuwa walikuwa sehemu ya serikali ya Japani, kundi hili halikuwa pamoja na jeshi. Hii ilisababisha matatizo kadhaa.
Mwaka 1934, kulikuwa na tukio la wafungwa kutoroka, idadi kubwa kati yao walikimbilia mashambani mwa China. Mwaka mmoja baadaye, mlipuko mkubwa ulitokea na sehemu kubwa ya ngome hiyo ilichomeka.
Licha ya matukio haya mawili kutokea , bado serikali ya Kijapani iliendelea na uchunguzi juu ya vita ya kibaiolojia.
Kwa hiyo, mwaka 1936, waliwapa kikundi cha Togo pesa zaidi na kuwapatia rasilimali zaidi kutoka jeshini, wakawapa wanajeshi wa Kijapani kwa kazi za ulinzi, na wafungwa wa Kijapani waliotumiwa kama panya wa majaribio.
Kila kitu kilikua kinaenda sawa kabisa..
Baadae kundi la Shiro Ishii…ambalo wakati huo lilijulikana kama Maabara ya Jeshi ya Kuzuia Magonjwa ya Mlipuko, lilihamishwa rasmi chini ya serikali ya Kijapani, Mfalme Hirohito alilibadilishia jina na kuliita "Idara ya Kuzuia Magonjwa na Usafi wa Maji." Jina hili lilikuwa ni trick ya kuficha lengo halisi la kuundwa kundi hili, kwa kufanya ionekane kama kundi linalo shugulika na usalama wa afya za watu.
Na katika kipindi hiki, kikundi cha Ishii kilipata jina rasmi la Unit 731.
Baada ya hapo,nguvu zao zote zilihamia China
why?
ENDELEA KUSOMA HAPO CHINI
click here to unlock the post

WAKALE. @wakale
JINSI GAMER ALIVYOPANGA MAUAJI YA KIKATILI click here to unlock the post

WAKALE. @wakale
JESHI LA KIVITA LILILO VUNJA RECORD YA KUWA NA BAHATI MBAYA DUNIANI click here to unlock the post

WAKALE. @wakale
Hili Ndilo Tukio la Kutisha Zaidi Kuwahi Kutokea Baharini...MEDUSA (1816) click here to unlock the post

WAKALE. @wakale
Promo Text click here to unlock the post