0%
Josias Charles

Josias Charles

Active Author,Diplomat, Psychologist, Politician

Josias Charles
Josias Charles @Josiascharles

MAGUFULISM- Falsafa Mpya Kuelekea Afrika Huru Kiuchumi || Vita ya Kiuchumi dhidi ya Propaganda.

Sehemu ya 18

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya

Tarehe 12, February, 2017, Rais Magufuli alitangaza vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za Kulevya. Tangazo hilo la Vita dhidi ya Dawa za Kulevya alilitoa akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kumuapisha Kamishna mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na dawa za Kulevya Bwana Rogers Siyang´a. Katika hotuba aliyoitoa Rais Magufuli, aliviagiza vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama kuongeza juhudi katika vita dhidi ya dawa za kulevya ili kuhakikisha watu wote wanaojihusisha na biashara haramu ya Dawa za Kulevya wanakamatwa na kufikishwa mbele ya Mkono wa Sheria.

Inaendelea..... .... click here to unlock the post

Josias Charles
Josias Charles @Josiascharles

MAGUFULISM- Falsafa Mpya Kuelekea Afrika Huru Kiuchumi || Vita ya Kiuchumi dhidi ya Propaganda.

Sura ya 17

VITA YA SERIKALI YA DR. MAGUFULI NA KAMPUNI YA BARRICK NA KAMPUNI YA PETRA DIAMOND
Kufuatia hatua hiyo, kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia inayomilikiwa na Kampuni ya Barrick Gold Mines ilitangaza kupunguza wafanyakazi na kupunguza shughuli zake za migodini ikiwa ni sehemu ya athari ya uzuiaji wa usafirishwaji wa makinikia uliowekwa na serikali ya Tanzania mwezi Machi mwaka huo. Hali hiyo ilisababisha uendeshaji wa siku hadi siku kwa moja ya migodi yake mikubwa Bulyanhulu kuathiriwa kwa kiasi kikubwa. Wakati wa mgogoro huo, Serikali ya Tanzania ilikuwa ikiishutumu kampuni ya Acacia kwa kukwepa kulipa kodi inayostahili, tuhuma ambazo kampuni hiyo ilikuwa ikizikanusha vikali. Katika taarifa iliyotolewa na Kampuni hiyo ilisema baadhi ya shughuli ndani ya mashimo yake ya dhahabu na shughuli za uchenjuaji wa makinikia zitasimama. Taarifa hiyo ilisema:-

Inaendelea......... click here to unlock the post

Josias Charles
Josias Charles @Josiascharles

MAGUFULISM- Falsafa Mpya Kuelekea Afrika Huru Kiuchumi || Vita ya Kiuchumi dhidi ya Propaganda.

Sehemu ya 16.....

Uanzishwaji Wa Masoko Ya Madini Hususani Dhahabu:

Tarehe 27 Apr 2019 Rais Dkt. John Pombe Magufuli alitoa siku saba kwa Wakuu wa Mikoa inayozalisha dhahabu nchini kushirikiana na Wizara ya Madini katika kufungua masoko ya madini ikiwemo dhahabu ili kuifanya sekta ya madini kuweza kuleta tija ya kiuchumi kwa Watanzania wote hususani wachimbaji wadogo. Rais Magufuli alitoa maagizo hayo akiwa Mkoani Mbeya katika hafla ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi la barabara ya Mbeya-Lwanjilo-Chunya-Makongosi yenye urefu wa Kilometa 111. Wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika eneo lile, Rais Magufuli alisema Serikali anayoiongoza kamwe haitokubali kuona wachimbaji wadogo wakiendelea kuteseka nchini.........

Inaendelea click here to unlock the post

Josias Charles
Josias Charles @Josiascharles

MAGUFULISM- Falsafa Mpya Kuelekea Afrika Huru Kiuchumi || Vita ya Kiuchumi dhidi ya Propaganda.

Sehemu ya 15

Ujenzi wa Ukuta wa Mererani:

Baada ya Rais Magufuli kujiridhisha vya Kutosha kuwa kuna utoroshaji Mkubwa wa Madini ya Tanzanite alichukua hatua za kudhibiti mchezo huo mchafu wa uhujumu uchumi. Dr Magufuli alitoa agizo la Kujengwa kwa Ukuta wa Mererani akiwa kwenye sherehe ya ufunguzi wa barabara ya KIA - Mererani iliyofanyika katika eneo la Mererani. Agizo hilo lilitolewa Tarehe 21 Septemba 2017 ambapo Dr Magufuli aliliagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kujenga ukuta wa kuzunguka vitalu kuanzia A hadi D vyenye madini ya Tanzanite katika eneo la Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ili kudhibiti uchimbaji na utoroshaji wa madini hayo ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.
Inaendelea....... click here to unlock the post

Josias Charles
Josias Charles @Josiascharles

MAGUFULISM- Falsafa Mpya Kuelekea Afrika Huru Kiuchumi || Vita ya Kiuchumi dhidi ya Propaganda.

Sehemu ya 14

Vita dhidi ya Unyonyaji katika Sekta ya Madini.

©Marekebisho Ya Sheria Na Mikataba Ya Madini Nchini.

Inaendelea........

Tarehe 12, June, 2017 Rais Magufuli alichukua hatua ya kuiagiza Wizara ya Katiba na Sheria chini ya Waziri wake Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuunda timu ya wataalam wa sheria ili kupitia upya sheria za mikataba ya madini nchini na kuzipeleka Bungeni kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho.
Rais Dkt. Magufuli alitoa maagizo hayo baada ya kupokea ripoti na kukubali mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Pili ya kuchunguza mchanga wenye madini yaani Makinikia. Dr. Magufuli alisema
“Timu ya wataalam wa sheria waaminifu wapitie sheria na mikataba yote ya madini na ipelekwe bungeni hata kama itahitajika kuongeza muda wa bunge”. click here to unlock the post

Josias Charles
Josias Charles @Josiascharles

MAGUFULISM- Falsafa Mpya Kuelekea Afrika Huru Kiuchumi || Vita ya Kiuchumi dhidi ya Propaganda.

Sehemu ya 13

Vita dhidi ya Unyonyaji katika Sekta ya Madini.

Baada ya Rais Magufuli kufanya ziara ya Kushtukiza katika Bandari ya Dar es salaam na kupiga marufuku usafirishaji wa Mchanga wa Madini (Makinikia) kwenda Nje ya Nchi alitangaza kuwa tupo katika vita ngumu ya kiuchumi katika sekta ya madini. Dr Magufuli alitahadharisha kuwa vita hii ya Uchumi ni kubwa na ni vita hatari zaidi duniani kwa kuwa inayahusu mataifa makubwa yenye uwezo kiuchumi. Katika kutoa tahadhari hiyo Dr. Magufuli alisema :“Hii ni vita kubwa kwa kuwa Kampuni za uwekezaji katika sekta ya madini zinatoka mataifa ya magharibi ambayo yanatumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa nchi za Afrika ambazo zina utajiri wa madini zinaendelea kupoteza huku mataifa hayo yakiendelea kuneemeka na rasilimali za Afrika”.

Inaendelea........ click here to unlock the post

Josias Charles
Josias Charles @Josiascharles

MAGUFULISM- Falsafa Mpya Kuelekea Afrika Huru Kiuchumi || Vita ya Kiuchumi dhidi ya Propaganda.

Sehemu ya 12

MAGUFULI ATANGAZA VITA YA UCHUMI.
Dr.John Pombe Magufuli alikuwa kiongozi aliyefahamika kwa ufanisi wake katika kutekeleza sera za maendeleo na mapambano dhidi ya uzembe, ufisadi, unyonyaji, rushwa na biashara haramu. Baadhi ya sera na mikakati aliyoiweka ililenga kuimarisha uchumi wa nchi, kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, na kukuza maendeleo ya miradi ya miundombinu.
Kwa mara ya Kwanza Dk. John Magufuli alitangaza Vita ya Uchumi tarehe 31, December 2015 katika mkesha mkubwa wa kuliombea Taifa pamoja na kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016, uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Kupitia hotuba yake aliyoifanya kwa njia ya Video Dr. Magufuli alisema: .......
Inaendelea click here to unlock the post

Josias Charles
Josias Charles @Josiascharles

MAGUFULISM- Falsafa Mpya Kuelekea Afrika Huru Kiuchumi || Vita ya Kiuchumi dhidi ya Propaganda.

Sura ya 11.

MAGUFULI AANZA KAZI KWA KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA.

Rais Dr. Magufuli alianza utumishi wake katika namna ya kustaajabisha sana. Alitumia Mfumo wa ziara za Kushtukiza........ Huu ulikuwa mfumo ambao haujazoeleka kabisa nchini Tanzania kwani hakuna Rais aliyewahi kutumia Mfumo huo toka Nchi imepata Uhuru..........Kupitia ziara ya Kushtukiza, Dr. Magufuli alikuwa akiibukia kwenye Ofisi ama miradi mbalimbali bila kutoa Taarifa na bila maandalizi yoyote.

Mfumo huu uliwafanya watumishi wa Umma kwenye Ofisi na Miradi mbalimbali kukaa Chonjo maana hawakujua Siku wala Saa ambayo Magufuli angeibukia kwenye eneo lao la kazi. Fuatana nami ili kuweza kujionea baadhi ya ziara za kushtukiza alizozifanya Dr. Magufuli na uone matokeo yake.
Inaendelea......... click here to unlock the post

Josias Charles
Josias Charles @Josiascharles

MAGUFULISM- Falsafa Mpya Kuelekea Afrika Huru Kiuchumi || Vita ya Kiuchumi dhidi ya Propaganda.

Sehemu ya 10

RAIS MAGUFULI AUNDA BARAZA LA MAWAZIRI.

Baada ya Kutumia Takribani mwezi Mmoja na nusu bila Kutangaza Baraza la Mawaziri ilianza kuibuka minong'ono mbalimbali kuhusu sababu zilizopelekea Dr. Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri. Baadhi ya sababu zilikuwa pamoja na Umakini Mkubwa ambao Dr. Magufuli alihitaji ili kuunda Baraza la Mawaziri litakalochapa Kazi kwa kasi na Viwango vyake. Ni wazi kuwa Dr. Magufuli alitumia Umakini Mkubwa sana katika Kuunda Baraza lake la Mawaziri.
Tarehe 10 Disemba 2015 Rais John Magufuli alivunja ukimya kwa kutangaza baraza lake la mawaziri ambalo.........
Inaendelea...... click here to unlock the post