How it worksCLUBZILA.
Clubzila ni mtandao unaowezesha mtumiaji kuweza kuuza maudhui yake ya kidigitali (maandishi,picha,video,files,live streams,) kwa urahisi zaidi.
WALENGWA.
Watengeneza maudhui wote ambao maudhui yao yako na monetizable value.
AINA ZA MAUDHUI
MAANDISHI
AUDIO
VIDEO
PICHA
LIVE STREAMS
ZIP FILES-PDF,E BOOKS,ETC

MITINDO YA MALIPO
Ifuatayo ni baadhi ya mitindo ya malipo muuza maudhui anaweza kutumia kuuza maudhui yake ndani ya platform ya Clubzila.
MALIPO YA MWEZI.
Kupitia Clubzila, muuza maudhui anaweza kuamua kuuza maudhui yake kwa mtindo wa malipo ya ada kila mwezi.
Mchapisha maudhui anaweza kuset gharama (bei/ada)ambayo mtu atahitajika kulipia kwa mwezi ili aweze kua mfuasi wake na kuweza kuona maudhui yake anayoyachapisha ndani ya mwezi huo...pindi mwezi utakapo isha,mfuasi atahitajia kulipia tena ili aweze kuendelea kupata maudhui yale.
PAY PER CONTENT. (LIPA KWA ANDIKO MOJA MOJA)
Clubzila inampa mchapishaji uwezo wa  kuuza maudhui moja moja (individual content)..kwa gharama utakayoweka mwenyewe. Yaani,unaweza kuamua ,ili mtu aweze kuona post fulani..nahitajia alipie gharama ya mara moja ya shilingi kadhaa....na kwa mtindo huu,maudhui hayo yataonekana kwa wale watu watakolipia ile gharama pekee..na sio kwa wengine.
TIP/SUPPORT. (HELA YA SHUKRAN)
Wewe kama muandaaji maudhui,kuna watu wengi sana wanaopenda kazi yako na kunufaika nayo kiasi kwamba wako tayari kukusaport katika juhudi zako. Clubzila iko na option inayomruhusu mtu kusaport maudhui yako moja kwa moja kwa ku “TIP” katika ukurasa wako ,kama sehemu ya kuthamini maudhui yako.
PAID LIVE STREAM.
Kama wewe ni muandaaji wa maudhui ya video za moja kwa moja(live streaming),platform ya clubzila imekuwezesha kuweza kurusha maudhui yako moja kwa moja kwa walengwa wako,lakini pia, Clubzila imekuongezea uwezo wa kuuza maudhui hayo kwa urahisi zaid kwa kuset gharama unayotaka walengwa wako walipie ili waweze kuungana na wewe kwenye live stream yako.
Mchapisha maudhui anaweza kufanya maudhui yake yapatikane bure kwa watu wote