About us

Clubzila ni jukwaa digitali (digital platform) inayokuwezesha  kuuza maudhui yako ya kidigitali moja kwa moja kwa hadhira yako kwa urahisi na usalama zaidi.

Kupitia ukurasa wako wa clubzila, unaweza kuchapisha na kuuza maudhui katika mtindo wa maandishi, picha, audio au video.

Ukiwa mchapisha maudhui ndani ya clubzila, utakua na ukurasa wako maalumu, ambao utachapishia maudhui yako,(maandishi, picha,audio au video),maudhui haya unaweza kuamua  hadhira yako iyapate kwa mtindo wa kulipia malipo ya mwezi, au malipo ya mara moja (kwa post husika) au bila gharama yoyote (bure).

Hadhira yako, itaweza kulipia maudhui hayo hapo hapo kwenye  ukurasa wako wa clubzila, kupitia mitandao ya simu kama M-pesa, tigo pesa, airtel money, halopesa nk.

Clubzila inalenga kuwarejeshea creators(watengeneza maudhui) nguvu ya kudhibiti na kunufaika na maudhui yao, aidha iwe ni taarifa,mafunzo,maisha binafsi(lifestyle & personality),hamasi/ushawishi na aina zingine za maudhui wanayoamua kuchapisha katika kurasa zao za clubzila.

Utengenezaji wa mtandao wa Clubzila umelenga kuleta urahisi wa matumizi kwa jamii za kiafrika,kwa kuzingatia uhalisia wa mazingira ya kiafrica.
Unaweza ukajisajili clubzila kupitia application zetu zinazopatikana ndani ya playstore na  appstore au kupitia website yetu ya clubzila.com