JM COMPANY
JM COMPANY @JMihambo

Sisi ni viumbe nuru, sisi ni nuru yenyewe sisi ni source/chanzo chenyewe sisi ni mmoja/moja (we are one) sisi ni Mungu. Ni atom source, Energy/nishati.

NB: Ukisoma kama Stori hutaelewa

Mfano Mwili, Mwili unatengenezwa na viungo vingi mpaka ukaitwa Mwili.

Mfano kuna mkono, mguu, kichwa, macho, pua, masikio, ubongo n.k, unaitwa mwili (mmoja/moja) unaotokana na viungo vingi.

Kwahiyo viungo vyote vinapata sifa ya kuitwa Mwili kwasababu viungo hivyo vimesababisha uwepo wa Mwili.

Na bila viungo hivyo huyo kiumbe mkubwa mmoja mwenye viungo vingi akikosa hivyo viungo hawezi kuwepo na hakutokuwepo na kitu kinachoitwa Mwili.

Mfano kichwa kijione chenyewe ni kikuu kuliko vyote kwenye mwili, ebu fikiria tumekiondoa tumekata kichwa tumeweka pembeni.

Je mtu atakiita kichwa Mwilli? hapana atasema hiki ni Kichwa cha mwili wa binadamu, kwamba tayari kimepoteza sifa ya kuwa Mwili.

Ila kinaitwa kichwa cha mwili, Sijui kwa mfano huu naeleweka?

Sasa hata katika dhana ya Mungu we are all Gods and Goddess. Kwamba sote ni Mungu wa kike kwa wakiume.

Na kitendawili na fumbo la imani ni kwamba tunafikiri sisi ni tofauti kwa kutazama mwonekano wa nje sura zetu kumbe sisi sote ni mmoja yule yule, Kivipi? click here to unlock the post

JM COMPANY
JM COMPANY @JMihambo

Tofauti ya nafsi na Roho

Nianze kwa kusema ya kwamba "Mizimu Sio Roho" imezoeleka watu wakiambiwa mizimu ni nini? Husema Mizimu ni Roho za Watu walio kufa, wengi hujidanganya hivyo.

Sihitaji kuwakosoa au kuwatukana nahitaji niwape maarifa niwaongezee hekima ya kweli.

Sishindani sipambani nimeamua kuishi katika ulimwengu wa Baba (Spirit Realm) angali nipo katika Ulimwengu wa Matrix (Virtual Simulation Matrix Worlds) au ulimwengu wa Watchers.

Naam, Kwahakika atakae pokea hekima hii ya Baba atafunuliwa ule ukweli mkuu.

Basi kwanini Mizimu sio Roho?

Kwanza huenda hatufahamu maana ya Roho na Nafsi pia hatujui tofauti ya kweli kati ya Nafsi na Roho. Nitakufafanulieni kadri Baba atakavyo fafanua kwangu.

Nitakufafanulieni Baba ni nani? na wala si vema kutumia viwakilishi vya mtu maana Siyo kiumbe you will understand at The End.

Neno Roho yaani Spirit ilitafsiriwa kutoka kwenye neno la kihebrania "Rauch" likimaanisha "Upepo" au "Pumzi" pia kisayansi ni "Energy" yaani Nishati.

Na neno Nafsi yaani Soul lilitafsiriwa lilipatikana kutoka kwenye neno la kihebrania "Repesh" likimaanisha "Breathing Creature" yaani "Kiumbe mwenye kupumua" hiyo ndiyo nafsi.

Hapo sijazungumzia mwili nimezungua Nafsi na Roho. click here to unlock the post

JM COMPANY
JM COMPANY @JMihambo

Chanting

Ni utajo ambao mtu hutaja kwa mtindo wa kurudia rudia ambao unaweza kwenda kama nyimbo ya rejeo la Zaburi, au torat ama wimbo wa injili hiyo ndio mifano yake.

Tukiangalia haijalishi yeye alikuwa ana chant nini?

Yoyote mwenye kuchant chochote maana yake anajaribu kuamsha energy ambayo inasafiri kutoka kwenye Throat chakra kisha inatetemesha Third eye chakra na mwisho inagonga hodi kwenye Crown chakra.

Ambayo huanza kumrejeshea Cosmic energy ambayo itasambaa eneo hio na maeneo ya nje kwake ambayo yataleta kwake mbadirishano wa mawimbi.

Kumbuka, Ubongo wa mwanadamu kazi yake si kufanya matendo ya hiari na yasiyokuwa ya hiari pekee, Bali muda mwingine hutumika kama receiver ya kupokea cosmic messages.

Hivyo anaefanya chanting ni sawa na anaefanya zikiri ikiwa chanting yake ni ya maneno au Humming and Buzzing sound mfano, kuunguruma au kufanya mitetemo yoyote ya koo. click here to unlock the post

JM COMPANY
JM COMPANY @JMihambo

Zijue ishara kwamba muda hio unapokea Cosmic Energy katika maisha yako.

• Kuongezeka kwa hisia​

Mara nyingi cosmic energy pia humtembelea mtu pale anapokuwa na hisia kali na ghafla hisia hizo zinakata na anaanza kuhisi jambo lingine la ghafla lenye kumliwaza na kumpa picha kamili kwenye akili.

Huo huwa ni ujumbe kutoka kwenye cosmic energy.

• Kujihisi unapenda bila sababu​

Muda mwingine mtu humuingia upendo usiokuwa na sababu na kuanza kujihisi kupenda mazingira na watu wanaomzunguka.

Kama ghafla tu kujiona umependa mtoto ama muonekano wa mtu mzima na kujihisi kutaka kumsaidia kujihisi unapenda kila mtu na kila kitu bila sababu nayo hutokea kwa muda mfupi.

Ama unajihisi kumuona mtu kabeba mzigo mzito unajihisi kutaka kwenda kumsaidia na unakuwa na kishawishi kikubwa.

Hii ni alama kuwa kwa muda huo unakuwa unapokea cosmic energy na kama unaijua basi utakuta mtu hazubai na anaanza kujitahidi kukaa na kupokea zaidi na zaidi ukiinuka hapo wewe ni mtu mwingine. click here to unlock the post

JM COMPANY
JM COMPANY @JMihambo

Katika dunia tunayoishi leo, kila kitu tunachokiamini kama historia au elimu rasmi kimetufikia kupitia vitabu, masomo shuleni, na makala mbalimbali.Lakini, je, umewahi kujiuliza kama kila kitu tunachoambiwa ni cha kweli?Je, historia ni ukweli mtupu, au kuna sehemu zilizopangwa, kufinyangwa, na hata kuongezwa ili kuendana na maslahi fulani?Nikiwa nafuatilia mijadala mitandaoni, nikakutana na hoja inayosisitiza kwamba historia nyingi tulizo nazo si ukweli mtupu, bali ni simulizi zilizoandikwa na washindi au watu waliotaka kudhibiti fikra za wengine.Moja ya mifano inayotajwa sana ni Atlantis, mji wa kifahari unaodaiwa kutoweka baada ya kumezwa na maji.Hadithi ya Atlantis ni mojawapo ya simulizi zinazopendwa sana duniani.Watu wengi wamekuwa wakiusaka mji huu kwa miaka mingi, wengine wakiutafuta chini ya bahari, wengine wakitengeneza nadharia mbalimbali juu ya uwepo wake.Lakini ukweli ni kwamba Atlantis ni kisa kilichobuniwa na mwanafalsafa Plato.Plato, mmoja wa wanafalsafa wakubwa wa Kigiriki, alikuwa akitumia mfano wa mji huu katika mijadala yake na wanafunzi wake.Alitumia Atlantis kama mfano wa ustaarabu uliofanikiwa lakini ukaja kuanguka kwa sababu ya kiburi na tamaa. Lakini kumbe, haikuwa historia halisi. click here to unlock the post

JM COMPANY
JM COMPANY @JMihambo

Sina budi kusema kuwa inawezekana tumedanganywa sana au nimepotoka pia kuamini hili.Kupitia speculations zangu nimekuja kung'amua kuwa hatupaswi kuwa na ugomvi wa kidini na kimadhehebu.Kwa kuwa wote tunachezeshwa na ka kikundi ka watu wachache wajiitao luciferian.Hivyo ili kuakikisha siwi na bias katika judgement zangu nimeamua kuweka hisia/mihemko ya kidini kando nakuamua kuchimba kujua chanzo cha yote haya ni nini na haya ndo majibu nilokuja nayo.The luciferian Mindset yaani fikra au mtizamo wa ki-ibilisi ambao ni chambo au mtego ambao ukishanasa humo kutoka ni vigumu.Unakuwa humo kwenye cage ambako uoni mlango wakutokea wala mwangaza wa kujinasua na dogma hii yenye nguvu kuu ulimwenguni.Ambayo imefanikiwa kuteka fahamu za mabilioni ya watu duniani nakuwafanya kuwa watumwa wake kwa miaka mingi sasa.Katika ngazi za juu kabisa za maamuzi wanakaa waanzilishi wa dogma hii yaani kikundi cha wachache au wapigaji wa ngoma then sisi tumeachiwa tuingie kucheza staili yeyote tuitakayo maadamu lengo lao wao litimie.Wao utambua kuwa "There Is No Supreme God" hakuna Mungu mkuu mwenye mamlaka yote.Isipokuwa umoja mmoja wa wapotoshaji wa kishetani waliojifanisha kana kwamba ni miungu Mungu na shetani. A Cabal yaani wala njama dhidi yetu wanadamu.Likitoka daraja hili la watunga sera, miongozo na taratibu zakufuatwa yanakuja madaraja makuu mawili ya mrengo wa kukinzana.Yaani wale wanaoonekana kana kwamba wanatuambia ukweli ila uthibitisho ni kwa njia ya kiroho na wale tunaowashuku kuwa wanatudanganya ila wao ufanya mengi kimwili zaidi. click here to unlock the post

JM COMPANY
JM COMPANY @JMihambo

Unajimu wa kale au astrolojia ya kitamaduni uhifadhiwa katika mikono ya wateule tu, mara zote watu hawa huwa na uwezo mkubwa wa kiufahamu kuliko wanadamu wakawaida.Katika viganja vyao vya mikono huwa na alama ya utawa au maono alama hii ya cross huwa kama majambia mawili yaliyopishana au mithili ya alama ya jembe na nyundo katika bendera.Mistari hii miwili inayokutana na kupishana uacha umbo kama la piramidi au pembe tatu sawa katika viganja vyote viwili vya mikono.Mara nyingi alama hii ukaa katikati ya kidole cha kwanza baada ya gumba na kile cha kati kirefu na mstari wa kitako unaofunga umbo hilo la pembe tatu huwa mstari wa moyo kwa chini yake.Pia wanaweza kuwa na vidoti vya mviringo vyeusi tokea kuzaliwa katikakati ya nyayo au pembezoni mwa dole gumba la mguu au kwenye viganja vyao.Sifa nyingine ni uwepo wa alama ya pembe tatu katikati ya kiganja ikiwa ni matokeo ya mstari wa bahati au karma (fate line).Hugawanyika kama huma ukielekea chini ya kiganja huku mstari mmoja ukiungana na mstari wa maisha, huku mwingine ukielekea uelekeo wa mount ya mwezi nafikiri wale wenye elimu ya palmistry kidogo wamenielewa. click here to unlock the post