Mbarouk
Mbarouk @Mbarouk

RIWAYA: KIKAO USIKU WA MANANE (Sehemu ya 37)+18
MTUNZI&MWANDISHI: Sherally Mbarouk
Email: sherallymbarouk@gmail.com
Hellen alifika nyumbani kwake usiku mrefu. Alienda moja kwa moja kwenye chumba cha matibabu ya mama yake na kumkuta Nasra akiwa amekaa pembeni ya kitanda cha mgonjwa. Alimtazama na kugundua kuwa alikuwa amechoka sana kutokana na kazi ngumu ya kuuguza mgonjwa aliye mahututi.

Alimtazama mama yake, hakuwa na mabadiliko yoyote. Alielekea chumbani na kujilza kitandani. Alikuwa amechoka sana kutokana na siku ndefu iliyokuwa na mambo mengi. Usingizi ulimpitia, alikuja kuzinduka asubuhi baada ya kusikia muito wa simu yake iliyokuwa kwenye mkoba wake.

Haraka haraka aliichukua simu na lakini kabla hajapokea ilikuwa imeshakatwa. Alitazama mpigaji alikuwa ni Wille, pia aligundua kuwa alikuwa amepigwa simu nyingi na Husna. Ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa Husna ulimshitua sana "Najaribu kukupigia sikupati, Samba yupo hapa".

Baada ya kusoma ujumbe huo haraka haraka alijaribu kumpigia lakini simu yake haikuwa ikipatikana. Aliangalia muda ulipotumwa ujumbe huo na kugundua kuwa ni usiku muda mfupi baada ya yeye na Wille kuondoka Club Montero. Wasiwasi ulizidi kuwa mkubwa. Alijaribu tena kupiga simu lakini haikupatikana. Wakati huo huo simu yake ikapata uhai tena na mpigaji alikuwa ni Wille.

"Hellen, habari za asbuhi" Wille aliongea baada ya simu kupokelewa. " Salama tu Wille, mimi sijambo sijui wewe huko" Hellen alijibu salamu huku akiwa tayari kumsikiliza. " Nimekupigia kujua kama ulifika salama tuliachana usiku mwingi" Wille Aliongea.

Hellen alitabasamu kidogo na kusema. " Asante sana kwa kujali. Nilichelewa sana kulala na pia nilikuwa nimechoka sana simu yako ndiyo imeniamsha usingizini. Hellen aliongea huku kimya kifupi kikipita.

"Hakuna shaka, sambamba na hilo kuna jambo nilikuwa nataka nikuulize. Yule binti shombe shombe wa pale Club Montero uliyekuwa ukiongea naye mnafahamiana? namaanisha ni nani yako" Hellen alitafakari kidogo kisha akasema.

"Kuna tatizo lolote, nafahamiana naye alikuwa rafiki mkubwa wa Walidi pamoja na Miliam, walikuwa walikiwa wakifanya kazi pamoja hapo. Naweza kusema ni rafiki yangu pia." Hellen alitoa maelezo ambayo yalifuatiwa na kimya kirefu kutoka kwa Wille.

"Pole sana Hellen, nasikitika kukutaarifu kuwa huyo binti amefariki dunia" Maneno ya Wille yalimfanya Hellen ahisi kizungu zungu, aliketi kitandani huku machozi yakitirirka mashavuni. Alikuwa haamini anachokisikia. Alishindwa aongee nini aliendelea kushikilia simu sikioni pasina kuongea chochote.

"Hellen, unisiikia?" Wille aliongea baada ya kimya kirefu kupita, alijua kuwa Hellen alikuwa akilia machozi. Alikuwa kwenye sintofahamu kubwa. "Imekuaje Wille maana sielewei unachonieleza, kifo chake kimesababishwa na nini?

"Inaonekana amegongwa na gari leo alfajiri wakati anatoka Club Montero, ameletwa kituoni na wasamaria wema kwa ajili ya PF3 ili apelekwe Hospitali lakini walikuwa wameshachelewa, alikuwa tayari amepoteza maisha. Nimemfahamu kwa kuwa niliona ukiongea naye. Pole sana Hellen. Nakusihi uendelee kuchukua tahadhari zote kwa kila unachofanya. Mimi nitakupigia baadaye" Wille aliongea kisha akakata simu.
******
"Chita utafanya utaratibu wa kufanya matengenezo ya hiyo gari ikiyotunika kwenye kumgonga yule shombe shombe, imebonyea kwa mbele. Hakikisha hii kazi inafanyika haraka iwezekanavyo ili kuweka hali ya usalama na kuondoa Kila aina ya ushahidi." Samba aliongea na kumfanya Faru anayanyuke kutoka kwenye kiti alipokuwa amejilaza akiendelea kuuguza jeraha la risasi.

"Ni nani amegongwa ?" Faru aliuliza kwa mshangao kidogo. "Nadhani unamfahamu yule shombe shombe Husna wa Club Montero. Tumelazimika kummaliza kwa kumgonga na gari. Kuna dalili zote kuwa anafahanu juu ya sisi kuhusika na mauji ya Walidi. Imebidi tummalize haraka sana kabla haijawa hatari zaidi" Samba aliongea huku akiwatazama Chita na Faru kwa zamu.

"Lakini amejuaje kuhusu hilo" Faru aliendelea kudadisi. Samba alitafakari kidogo kisha akasema. " Ni kuwa ili kubaini ni nani alimtorosha Miliam kutoka Club Montero siku ile nilimuomba Husna anipatie kumbukumbu ya kamera za usalama. Haikuwa ngumu kunipatia kwa vile najua ni muda mrefu ananitamani lakini pia nilimlipa pesa kwa kazi hiyo" Samba alinyamaza kidogo kisha akaendelea.

"Kupitia kumbukumbu za kamera za usalama alizonipa niliweza kujua kuwa Zomo ndiye aliyempenyezea ujumbe Miliam kupitia kwa Walidi na hatimaye akatutoroka. Hata hivyo nilikuwa nimeshajua kabla kuwa Zomo ananizunguka na anavujisha siri za kazi,kwa hiyo lilikuwa swala la muda kabla sijammaliza. Jana kwenye kuongea na Huyo Husna ndipo niligundua kuwa tayari ananishuku kuhusika na kifo cha Walidi au hata Miliam.".Samba alimaliza kutoa maelezo yake.

"Ni hatari sana kuendelea kufanya mauji ya watu wasiotuhusu. Najua wewe Samba ni kiongozi wetu lakini inabidi uwe makini hasa kwenye masuala ya mapenzi na mahusiano vinginevyo tutakuja kuangamia sote hapa." Faru alitoa angalizo kwa Samba huku akionekana kitoridhishwa na maelezo ya Samba.

"Jambo lingine la muhimu sana ni kuwa kwa sasa tuna upungufu wa nguvu kazi, kuna pengo kubwa lililoachwa na Zomo,Fadhili,Boni, Zabron na hata huyo Miliam. Nimeongea na Mzee kuhusu hilo, amenieleza kuwa yule dogo Zabron akimaliza kozi atakuwa na sisi lakini pia wataongezeka watu wawili au watatu kwa ajili ya kuongeza nguvu" Samba alimaliza kuongea na kuondoka kuelekea chumbani kwake.
*****
Asubuhi hii Mzee Damas alikuwa amepokea mgeni ambaye ni nadra sana kufika ofisini kwake tena bila taarifa, huyu si mwingine bali ni Steve Chami mtoto wa swahiba wake Amon Chami. Hakutegemea ugeni huu asubuhi mapema kiasi hiki. Alimkaribisha kwa bashasha kubwa. Mzee Damas amekuwa akimuhusudu sana kijana huyu kutokana na umahiri wake katika kusimamia shughuri za utendaji kazi wa kampuni ya DSM Motors.

"Karibu sana Steve, ni kitambo kirefu kimepita hujafika hapa ofisini kwangu. Karibu sana" Mzee Damas aliongea huku akionesha wazi kufurahia uwepo wa kijana huyu mtanashati.Wakati huo Steve aliketi kwenye kiti kilicho wazi mbele ya meza kubwa ya nadhifu mbele ya mzee Damas "

"Asante sana, pole na majukumu ya kazi, utaniwia radhi kwa kufika hapa mapema kiasi hiki tena bila taarifa" Steve aliongea huku akijiweka sawa kwa ajili ya mazungumzo na mzee huyu ambaye mbali na kuwa rafiki mkubwa wa baba yake lakini pia ni boss wake.

"Baba ninefika hapa kukupongeza wewe binafsi kutokana na juhudi zako hadi kufanikisha mkataba mkubwa wa uzalishaji na wenzetu wa Marekani. Ni hatua kubwa sana baba, kampuni inakua sasa.Ni jambo la kujivunia sana baba." Steve aliongea huku tabasamu pana likichanua usoni mwake. Ni dhahiri kuwa alikuwa mwenye furaha sana.

"Nashukuru sana Mwanangu, mimi pia najivunia sana ueltendaji wako wa kazi. Unafanya kazi nzuri sana. Sisi umri umeanza kututupa mkono, tunategemea nguvu na akili zenu kuendeleza tulichokianzisha kwa faida yenu hata wakati ambao sisi hatujiwezi tena au hatupo tena duniani" Mzee Damas aliongea huku akimtazama Steve usoni, ambaye alitikisa kichwa kuonesha kukubaliana na maneno yake.

"Mimi na baba yako ni marafiki wakubwa, tangu ni vijana mabarobaro mpaka leo tunakaribia kushika mkongojo. Urafiki huo inabidi tuurithishe kwenu watoto ili muuendeleze. Dokta Amani alikuwa hapa jana sikupata nafasi ya kutosha kuongea naye kuhusu hilo lakini ni muhimu sana. " Mzee Damas aliongea huku akimimina kahawa kwenye kikombe kidogo kwa ajili ya Steve.

Maneno ya Mzee Damas yalimkumbusha maneno aliyoambiwa na baba yake siku chache zilizopita kuwa anatakiwa kuimarisha mahusiano yake na Evelyn mtoto wa Mzee Damas aliyeko nchini Marekani. Aliona kabisa maneno ya mzee Damas ni msisitizo wa hilo.

"Ni kweli baba, tutajitahidi kuimarisha mshikamano mliouanzisha. Kuhusu kazi tunaendelea vizuri na nilongea na muhasibu na mtu wa manunuzi kuhusu vifaa vya matibabu. Tumeviagiza nchini Marekani na vitawasili kwa ndege ya mizigo. Vitamfikia Dokta Amani muda wowote kuanzia sasa."Walizungumza mambo mbali mabli hasa kuhusu kazi kabla Steve hajaaga na kuondoka.

Muda mfupi baada ya Steve kuondoka Amon Chami aliingia ofisini kwa mzee Damas. Hakuwa mchangamfu kabisa tofauti na alivyozoeleka. Baada ya salamu alienda kuketi kwenye nafasi yake.

"Nipo kwenye wakati mgumu sana ndugu yangu. Nadhani unakumbuka kuwa jana nilinza kazi ya kumtafuta mama yake na Steve, nimeenda hadi nyumbani kwao Tandika. Habari nilizozipata ni kuwa alishafariki. Kibaya zaidi ni kuwa hata aliyekuwa mume wake ni marehemu sasa. Kama haitoshi hata mtoto wake naye alishafariki" Amon Chami aliongea maneno yaliyomshangaza sana mzee Damas.

"Inawezekanaje kuwa familia nzima wote ni marehemu. Mbona sielewi kabisa unachosema Amon," Mzee Damas aliongea baada ya kutafakari alichoongea rafiki yake.

"Ni kama njozi lakini huo ndiyo ukweli, sijui nitamueleza nini Steve aneielewe. Ni kuwa kifo cha mtoto wao kilizua mshituko kwa baba yake akafariki kwa kihoro na baadaye mama yake naye akafuatia." Amon Chami alimaliza kutoa maelezo yake ambayo yalimchanganya sana mzee Damas.
ITAENDELEA click here to unlock the post

Mbarouk
Mbarouk @Mbarouk

RIWAYA: KIKAO USIKU WA MANANE (Sehemu ya 36)+18
MTUNZI&MWANDISHI: Sherally Mbarouk
Email: sherallymbarouk@gmail.com
Hellen aliagana na Wille akaingia kwenye taksi ile ile aliyokuja nayo na kuondoka. Wakati huo Wille naye aliondoka kwa kutumia gari lake alilokuja nalo. Mawazo yalikuwa mengi kichwani mwa Hellen, mazungimzo yake na Wille yalikuwa yamempa picha halisi ya mambo ya hatari kubwa iliyopo mbeleni endapo ataendelea kuwatafuta wahusika wa mauaji ya Miliam.

Alitazama saa yake ya mkononi na kugundua kuwa tayari ni usiku wa manane, alimuelekeza dereva wa taksi ampeleke Makongo juu. Alitaka kumjulia hali Profesa Laurian Mugisha kakitaka kulala bila kujua maendeleo ya afya ya mzee huyu daktari bingwa. Alijua sio hali ya kawaida kwake kuumwa kiasi cha kulala kitandani, haikiwahi kutokea kabla.

Hellen alikuwa na upendo mkubwa kwa Profesa Laurian Mugisha, amemfahamu tangu akiwa kigoli mpaka sasa ni mtu mzima. Amekuwa sehemu ya maisha yake katika nyakati zote. Alikumbuka mara ya kwanza kuonana naye alikuwa darasa la tano.Siku hiyo Profesa Laurian Mugisha alifika shuleni kwao saa nne asubuhi.

Hellen alikuwa anaendelea kucheza akiwa na wenzake kwani kulikuwa muda wa mapumziko. Alishangaa sana kuona gari likifika shuleni hapo ndani akiwemo mama yake na Mzee ambaye baadaye alikuja kufahamu kuwa ni Profesa Laurian Mugisha. Walienda moja kwa moja ofisini kwa Mwalimu mkuu .Hakujua hasa kiini cha safari ya mama yake na mzee huyo.

Aliporudi nyumbani, kwa mara nyingine tena alishangaa kumkuta mtu yule yule. Safari hii alikuwa anaagana na baba na mama Hellen baada ya mazungumzo ya muda mrefu. Hellen alikuwa na shauku kubwa ya kujua huyo mtu ni nani. Alimuuliza mama yake, alijibiwa kuwa huyo anaitwa Profesa Laurian Mugisha, kuwa amepata taarifa za uwezo wake mkubwa darasani hivyo amejitolea kumsomesha.

Zilikuwa ni habari njema kwake, alizipokea kwa mikono miwili na alijua kabisa kuwa sasa hali duni ya familia yake haitakuwa kikwazo tena kwake katika kusoma na kutimiza ndoto zake za kimaisha. Kuanzia wakati huo Profesa alikuwa mtu muhimu sana katika maisha yake. Alimpeleka kwenye shule za gharama kubwa na hata baada ya kumaliza masomo ya sekondari alimpeleka katika vyuo vikuu bora kabisa duniani huko Marekani na Uingereza.

Ni Profesa huyo huyo aliyemuingiza kwenye kazi za ukachero ndani ya idara ya usalama wa Taifa la Tanzania, kazi ambayo ameifanya kwa muda mrefu na kwa ufanisi mkubwa kutokana na mafunzo ya hali ya juu aliyoyapata nchini Marekani, Urusi, Cuba na Uingereza. Kazi ambayo imechukua sehemu kubwa ya maisha yake kiasi cha kumfanya asiishi maisha ya kawaida kama walivyo watu wengine.

Ukaribu wake na Profesa Laurian Mugisha umemfanya Hellen asione pengo la kifo cha baba yake kutokana na kuwa ametumia sehemu kubwa ya maisha yake akiwa naye kuliko alivyokuwa na baba yake mzazi. Alikuwa anaamimi Mzee huyu ni zaidi ya baba yake wa kumzaa, na sasa alikuwa anamtegemea katika kufanikisha upasuaji wa mama yake na hata kupona kwake. Hakuwa akiamini kabisa kuwa kuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hiyo zaidi yake.

Alishuka kwenye taksi na kutembea taratibu kuingia nyumbani kwa Profesa Laurian Mugisha. Geti lilifunguliwa akaingia moja kwa moja ndani. Alienda moja kwa moja hadi chumbani kwa Profesa na kumkuta Dokta Amani akiwa ameshilia dripu ya maji kwa ajili ya kumuwekea mgonjwa. Dokta Amani hakutegemea uwepo wa Hellen mahali hapo tena kwa muda huo, alitegemea kuwa atakuwa nyumbani akimtazama mama yake aliye mahututi kitandani. Alitaka kuongea jambo lakini Profesa akamkatisha kwa kusema.

"Ooh! Karibu sana Hellen, ni usiku sana sikutegemea uwe hapa sasa hivi" Hellen alimtazama Profofesa na kugundua kuwa alikuwa amedhoofika sana pamoja na kuwa alikuwa anajitahidi kuongea. Hellen aliangalia picha yake iliyotundikwa ukutani na kushangaa, hakuwa akijua kuwa Profesa ameweka hadi picha yake ukutani.

"Nisingeweza kupata usingizi bila kujua maendeleo ya afya yako." Hellen aliongea huku akikaa kwenye ncha ya kitanda. "Nakushukuru kwa kuja kuniona. Vipi mama yako anaendeleaje" Profesa aliongea kwa sauti dhaifu.

"Nadhani Dokta Amani atakuwa amekueleza Kila kitu kuhusu hali ya mama" Hellen aliongea huku akimtazama Dokta Amani ambaye muda huo aliondoka humo chumbani kuwapa nafasi ya kuzungumza..

"Amenieleza kila kitu. Kama nilivyokuwa nimeshakueleza siku za nyuma, ni daktari mzuri, ni kijana wangu atafanya kazi vizuri hatokuangusha." Profesa aliongea kwa shida.

"Sijawahi kuona umeugua kiasi cha kulazwa kitandani. Napata hofu sana ninapokuona katika hali hii. Unasumbuliwa na nini Prof." Hellen aliongea huku akisogea karibu ili aweze kumsikiliza vizuri.

"Nadhani unamfahamu Eliakim Mbano" "Ndiyo namfahamu, si ni yule waziri" Hellen alijawa na shauku kubwa ya kutaka kusikia maelezo ya ziada kuhusu mtu huyo. Alichokuwa anajua ni kuwa ni mmoja wa marafiki zake wakubwa na si mara ya kwanza kumsikia kutoka kwake.Pia ni mwanasiasa mashuhuri sana.

"Mimi ni daktari wake kwa miaka mingi, tangu akiwa barobaro mpaka leo. Kwa sasa yupo mbioni kuwania nafasi ya uongozi wa juu kabisa wa nchi. Ukaribu wangu na yeye sasa ni tishio kwa utawala uliopo madarakani. Pengine ndiyo sababu nipo hapa kitandani napigania uhai wangu." Maelezo ya Profesa Laurian Mugisha yalimchanganya sana Hellen. Alishindwa kabisa kuelewa uhusiano wa alichozungumza na kuugua kwake. Alitaka kuongea jambo lakini mlango wa chumba ukafunguliwa Dokta Amani akaingia.

"Ni usiku mrefu sasa, mimi naondoka. Nitapata wakati mwingine wa kuja kukuona" Hellen aliongea huku akitoka ndani ya chumba. Alikuwa na mambo mengi ya kuzungumza na Profesa Laurian Mugisha lakini uwepo wa Dokta Amani haukumpa uhuru wa kutosha. Hakuwa amepata majibu ya maswali aliyokuwa akijiuliza kichwani.

Wakati anakaribia mlango wa geti alisikia akiitwa.Alikuwa ni Dokta Amani.Alisimama kumsubiri. " Hellen, utaniwia radhi kwa kukatisha mazungumzo yako na Profesa. Hali yake sio nzuri kabisa, anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika. Lakini pia kama hutojali naomba nikusindikize, nikurudishe nyumbani. Ni usiku sana Hellen" Dokta Amani aliongea huku akimtazama Hellen kuanzaia kichwani hadi miguuni kwa msaada wa mwangaza wa taa.

Dokta Amani alikuwa ameshangazwa sana na urembo wa Hellen, tofauti na alivyomuona kabla. Alishindwa kuelewa kama ni Hellen yule yule au ni mwingine. Alijikuta akitumia muda mwingi kumkodolea macho.

"Asante Dokta kwa wema wako. Kwa sasa endelea kumuangalia Profesa. Usiwe na wasiwasi na mimi. Nitafika nyumbani salama. " Hellen aliondoka na kumuacha Dokta Amani akiwa amesimama wima. Aliianza kuhisi anavutiwa na binti huyu mrimbwende.
****
Ni usiku wa manane ndani ya Club Montero, Idadi kubwa ya watu walikuwa wanaendelea na starehe zao. Samba na Chita walikuwa wameketi kwenye nafasi zao wakiendelea kupata vinywaji. Pesa haikuwa kikwazo kabisa, walikuwa wamepokea kitita kikubwa kutoka kwa Mzee Damas.

Muda wote Samba alikuwa akiangaza huku na kule kujaribu kuona kama atamuona Husna, binti shombe shombe ambaye siku zote anautikisa moyo wake kutokana na uzuri wake. Kwa mbali aliweza kumuona sehemu ya vinywaji akiwa anaendelea kuhudumia wateja.

Haraka haraka alinyanyuka na kumfuata. Tofauti na siku zote, Husna hakuwa mcheshi kabisa. Hakuonekana kujali uwepo wa Samba mbele yake.Jambo ambalo lilimshangaza kidogo, si kawaida yake kuwa mpole namna hii hasa muda kama huo ambao kila mtu yuko kwenye kilele cha furaha ndani ya club hii kubwa na maarufu sana jijini Dar es Salaam.

"Husna,leo ninekuja hapa kwa ajili yako. Kula na kunywa chochote kwa gharama zangu. Pesa ipo kwa ajili yako" Samba alijitapa huku akikaa vizuri kwenye stuli ndefu na wakati huo alitoa burungutu kubwa la hela na kuiweka mezani kisha akamsogezea Husna ambaye alikuwa kimya akimtazama.

"Samba, nadhani unatafsiri mbaya sana kuhusu mimi. Hiyo pesa yako baki nayo. Sihitaji kabisa pesa yako" Husna aliongea huku akiirudisha pesa mikononi mwake. Samba alishangaa sana Husna kukataa kiasi chote hicho cha pesa, aliangaza huku na kule kuona kama kuna aliyeona jambo hilo kisha akairudisha pesa kwenye mfuko wa koti lake.

Husna alitazama kwenye meza alipokuwa amekaa Hellen pamoja na mwenzake lakini hakuwaona. Aligundua kuwa wameondoka muda mrefu kwani meza yao ilikuwa tayari imekaliwa na watu wengine. Alitaka kumuonesha Samba, mshukiwa wa mauji ya Walidi na Adili aliyekuwa anamtafuta.

Husna alikuwa ameanza kuamini kuwa Samba anahusika kwa namna moja ama nyingine na mauji ya Walidi kama alivyoelezwa na Hellen hasa akikumbuka kuwa alimfuata na kumpatia kiasi kikubwa cha pesa ampatie kumbukumbu za kamera za usalama na kesho yake Walidi akauawa.

Alimtazama usoni kwa sekunde kadhaa kisha akasema. " Samba mimi ni mtu mzima najua unachokitaka kwangu na sina sababu ya kukukatalia. Uko moyoni mwangu hata kabla mimi sijaingia moyoni mwako." Kusikia hivo Samba aliachia tabasamu hafifu huku akipiga fundo moja kubwa la pombe kali aina ya Snow"

"Kabla hatujafika popote, unaweza kunieleza siku ile ulichukua kumbukumbu za kamera za usalama kwa ajili gani, na je unafahamu chochote kuhusu kifo cha Walidi" Samba alishitushwa sana na swali hilo, alimtazama Husna kwa macho makali. Ni dhahiri kuwa hakuwa amefurahishwa kabisa na maneno yake.

"Husna, chunga sana ulimi wako. Unataka kusema kwamba mimi nimemuua Walidi? " Samba aliongea huku akinyanyuka na kuondoka eneo hilo huku Chita naye akimfuata kwa nyuma. Waliingia ndani ya gari na kuondoka haraka.
ITAENDELEA click here to unlock the post

Mbarouk
Mbarouk @Mbarouk

RIWAYA: KIKAO USIKU WA MANANE (Sehemu ya 35)+18
MTUNZI&MWANDISHI: Sherally Mbarouk
Email: sherallymbarouk@gmail.com

Dereva aliegesha gari sehemu ya maegesho mbele ya nyumba ya Profesa Laurian Mugisha, daktari bingwa wa magonjwa ya ubongo na fahamu. Baada ya kujiweka sawa Mheshimiwa Eliakim Mbano alitembea taratibu kuelekea ndani ya nyumba ya mzee huyu maarufu. Si mara ya kwanza kwake kufika hapa, ni kama nyumbani kutokana na ukaribu wa wao wa muda mrefu.

Alienda moja kwa moja chumbani na kumkuta Profesa akiwa amelala kitandani akionekana dhahiri kuwa hali yake ya afya si nzuri. Aliketi kwenye kiti pembeni yake na kumtazama kwa sekunde kadhaa.

"Karibu sana Mheshimiwa, sikujua kama utawahi namna hii" Profesa aliongea kwa shida baada ya kuona Eliakim Mbano amekaa kimya pasina kuongea chochote huku akiikazia macho picha moja iliyokuwa imetundikwa ukutani ndani ya chumba hicho.

"Unajua tangu nikufahamu sijawahi kuona umeunwa kiasi cha kulala kitandani. Ulivyonieleza kuwa unaumwa upo kitandani imenibidi nifupishe kikao ili niwahi kuona maendeleo yako." Eliakim Mbano aliongea huku akirekebisha shuka na kusogea karibu zaidi ili aweze kusikia kila neno kutoka kwake.

"Nakushukuru sana mwanangu" Profesa aliongea baada ya kukohoa kidogo kuweka sawa koo lake. "Nini hasa kinakusumbua Prof. Naangalia kama inawezekana nikupeleke Hospitali kwa uangalizi zaidi, mganga hajigangi ni bora uendelee na matibabu yako hospitalini" Maneno ya Eliakim Mbano yalimfanya Profesa Laurian Mugisha aachie tabasamu hafifu huku akimtazama Eliakim Mbano usoni.

"Nadhani kuna mambo mengi huyajui mwanangu. Nikiwa hapa ni salama zaidi kwangu na nitapona kuliko huko unakotaka niende" Hiyo kauli ilimshangaza sana Eliakim Mbano. Inawezekanaje mtu ambaye ni daktari bingwa anaogopa kwenda kwenye matibabu hospitalini. Hakuweza kupata majibu ya moja kwa moja nini anamaanisha.

Jambo moja analolijua kuhusu Profesa Laurian Mugisha ni kuwa ni mtu mwenye usiri mkubwa kuhusu maisha yake, nyumba yake ni nyumba yenye upweke siku zote kutokana na kuwa hana mke,mtoto wala ndugu wa karibu anayefahamika. Mara kadhaa amejaribu kumuuliza kwa nini iko hivo lakini hajawahi kupata majibu ya kueleweka.

"Kazi uliyonipa nilifanya imekamilika sasa" wakati Eliakim Mbano anajaribu kukumbuka alimpa kazi gani Profesa akainuka kidogo kitandani na kujivuta karibu kabisa na ncha ya kitanda ili awe karibu na Eliakim Mbano. "Kumbukumbu za taarifa zote zinazohusu ugonjwa wako tayari zimeondolewa kila sehemu" Eliakim alitikisa kichwa kuonesha kuridhishwa sana na taarifa hizo.

"Ni jambo la hatari sana nimefanya ndio maana nipo kitandani. Hiyo nafasi unayotaka kugombea ni sawa sawa na umetangaza vita na waliopo madarakani. Ongeza tahadhari zaidi.Nimefanya hivyo kwa sababu naamini pengine ukiwa kiongozi wa nchi hii utakuwa baraka kwa wananchi wanyonge utawapigania" Eliakim alijikuta kwenye wakati mgumu sana kutokana na maneno ya Profesa Laurian Mugisha. Aligundua kuwa pengine kuna jambo kubwa linaendelea na yeye hajui au pengine hataki kumwambia.

Wakati anaendelea kuwaza ulisikika muungurumo wa gari nje. Eliakim Mbano alitazama kupitia dirishani na kulitambua gari hilo kuwa ni gari la Profesa. Alishangaa sana, hakuwahi kuona mtu mwingine tofauti na yeye akilitumia gari hilo.Aliendelea kutazama kwa makini ili kuona ni nani huyo aliyefika na hilo gari.

Alishuka kijana mmoja mtanashati akiwa ameshikilia begi dogo mkononi. Mheshimiwa Eliakim Mbano alikuwa na shauku kubwa ya kumfahamu kijana huyo ambaye anaaminiwa na Profesa Laurian Mugisha kiasi cha kumpa gari lake au hata kumkaribisha nyumbani.Mlango wa chumba ulifunguliwa na huyo kijana akaingia ndani.Hakuonesha kujali uwepo wa Eliakim ndani macho yake yalienda moja kwa moja kwa Profesa aliyekuwa amejilaza kitandani.

"Shikamoo Profesa,vipi hali yako kwa sasa" Yule kijana ambaye baadaye alikuja kumfahamu kuwa ni Dokta Amani Dama, aliamsalimia Profesa huhu akiweka kiganja kwenye paji lake la uso kuangalia kiwango chake cha joto.

"Kwa sasa napata ahueni, leo nimetembelewa na mgeni hapa. Nadhani unamfahamu, ni bahati nzuri nyote mmekutana hapa"

"Ooh!, Shikamoo Mheshimiwa Waziri" Dokta Amani aliongea baada ya kugeuka na kumtazama Eliakim Mbano. "Utaniwia radhi sikukuzingatia nilipoingia humu ndani, mawazo yangu yote yalikuwa kwa Profesa" Aliongea huku tabasamu pana likichanua usoni mwake.

"Marahaba, wala hata usijali" Eliakim Mbano alijibu kwa kifupi, alitaka kuongea jambo lakini Profesa akamkatisha kwa kusema. "Huyu ni kijana wangu,anaitwa Dokta Amani Damas, ni mtoto wa swahiba wako Mzee Damas. Ni daktari mahiri sana tuko naye pale Hospitali ya taifa pia ni daktari wangu na familia yangu".

Hayo maneno yalimchnganya sana Eliakim Mbano. Hakuwa akijua kuwa Mzee Damas ana kijana mkubwa ambaye ni daktari wa kiwango cha kuaminiwa na Profesa Laurian Mugisha. Jambo lingine lililomshangaza sana ni kusikia kuwa ni Daktari wake na familia yake haliyakuwa hakuwahi kuona wala kusikia kuwa ana familia, alitafakari kidogo kisha akasema.

"Nimefurahi sana kukufahamu Dokta, Baba yako ni swahiba wangu mkubwa sana, kimsingi ni kama baba yangu mzazi au zaidi ya hapo. Aliokoa maisha yangu na ameendelea kuwa nguzo muhimu sana ya maisha yangu. Nilivyo leo na nitakavyokuwa kesho ni kutokana na uwema wake. Lakini nilikuwa sifahamu kama ana kijana mkubwa namna hii tena daktari bingwa".

Dokta Amani alimtazama Mheshimiwa Eliakim Mbano usoni na kutikisa kichwa kuonesha kukubaliana na maelezo yake. Alikuwa anaijua tabia ya baba yake ya kutotaka kuwasogeza watoto wake na marafiki zake. Hakushangaa kusikia kuwa huyu Waziri ni rafiki mkubwa wa baba yake kwani pia baba yake ni mfanyabishara na tajiri mkubwa sana anayefahamika na kuheshimika sana. Kilichomshangaza ni kusikia kuwa aliokoa maisha yake. "Hilo nitamuuliza baba, aliokoaje maisha yake na anahusikaje katika ustawi wa kiongozi huyu mkubwa serikalini"

Dokta Amani alichukua vipimo vya kitabibu na kuanza kumpima Profesa Laurian Mugisha kuangalia maendeleo yake. Haukupita muda mrefu Mheshimiwa Eliakim Mbano akaaga na kuondoka huku akiahidi kuja wakati mwingine kumjumia hali mgonjwa. Aliondoka akiwa na maswali mengi kichwani kuliko majibu. Alifikiria kukutana tena na Profesa Laurian Mugisha mara tu atakapopata ahueni ili aweze kumjibu maswali anayojiuliza kichwani.
*****
Karim aliamua kukubali kuwa yeye ndiye aliyemuua Adili kwa kumpiga risasi na pia ndiye aliyemuua Miliam kutokana na wivu wa kimapenzi. Aliona kabisa ni bora aende kufungwa jera kuliko kuuawa kikatiri ndani ya chumba hiki cha kutisha. Maelezo yake yaliandikwa huku bastola aliyokutwa nayo kikiwa ni kielelezo muhimu.

Alikuwa amaumia sana kutokana na kipigo kikali,haukupita muda mrefu baada ya kuchukua maelezo yake alipakiwa kwenye gari la Polisi chini ya ulinzi mkali na kupelekwa katika gereza la Ukonga lililopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam,moja kati ya magaereza mazito nchini Tanzania. Karim hakuamini kabisa kilichokuwa kinatokea katika maisha yake, alikuwa anaona labda ni ndoto yupo usingizini.
****
CID Wille ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwasiri ndani ya Club Montero na kwenda kuketi kwenye sehemu ya wageni maalum akimsubiri Hellen ambaye walikuwa wamekubaliana kukutana usiku huo ndani ya club hiyo maarufu sana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.

Walichagua kukutana ndani ya club hii kutokana na ukubwa wake na uwingi wa watu hasa muda wa usiku. Aliendelea kupata kinywaji huku akiwaza mambo mbali mbali, kubwa likiwa ni suala la Liberatha kuchukuliwa na watu wanaosemekana kuwa ni Polisi na kutokomea naye kusikojulikana mpaka wakati huo.

Akiwa anaendelea kuwaza na kuwazua alimuona Hellen akiingia na kwenda moja kwa moja kuzungumza na binti mmoja shombe shombe aliyekuwa amekaa sehemu ya mapokezi akiendelea kuhudumia wateja. Alimtambua Binti huyo kuwa ni mmoja wa wahudumu wa club hiyo kutokana na sare zake alizovaa, alionekana kufahamiana vyema na Hellen kutokana na namna walivyokuwa wakiongea kwa bashasha.

Baadaye kidogo Hellen alisogea alipokuwa ameketi Wille na kusimama mbele yake kabla ya kujiweka sawa na kuketi kwenye kiti kilichokuwa wazi. Wille alimtazama Hellen kama vile ndiyo mara ya kwanza kumuona pengine kutokana na namna alivyokuwa amependeza kupita kiasi.

Alivalia gauni fupi juu ya magoti lililoacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi huku akiachia nywele zake ndefu zikining'inia mgongoni usawa wa mabega. Wille alijitahidi sana kutoonekana amevutiwa na muonekano wa Hellen kwa siku hiyo.

"Karibu sana uketi Hellen" Wille aliongea na wakati huo Hellen aliketi huku akiachia tabasamu pana lilofanya meno yake yaliyopangiliwa vizuri kinywani yaonekane sambamba na vishimo vidogo kwenye mashavu yake.

Wille alimimina kinywaji kwenye bilauri iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya Hellen huku akimtazama usoni kwa macho ya udadisi. Alikuwa amegundua kuwa hakuwa sawa japoo alijilazimisha kuweka tabasamu usoni mwake mwake. Kimya kifupi kikipita wakati Hellen akipiga fundo kadhaa za kinywaji chake.

"Wille sitakuwa na muda mrefu wa kukaa hapa. Tutatumia muda mfupi sana kuzungumza kisha utamiruhusu niondoke. Siko sawa kabisa Wille. Nimeumizwa sana na kifo cha Miliam.Nilimuahidi kuwa nitamlinda lakini nimeshindwa kufanya hivyo sasa yupo ndani ya jokofu la hospitali" Hellen aliongea huku machozi yakijaa machoni.

"Pole sana, hupaswi kujilaum kwa hilo sio kosa lako" "Kinachoniuma zaidi ni. kuwa ameuawa kikatiri tena akiwa mjamzito" Hellen aliangusha kilio kikali kiasi cha kimshtua Husna aliyekuwa sehemu ya mapokezi na kumfanya asogee kwenye meza ya wawili hawa kutaka kujua kulikoni.

"Vipi Hellen kuna tatizo gani mbona unalia" Husna aliongea huku alimsogelea Kwa ukaribu zaidi. "Milliam amefariki, alipigwa risasi nyumbani kwake jana usiku" Husna aliweka mikono kichwani baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa Hellen. Zilikuwa ni habari mbaya sana kwake.Aliondoka huku akijizuia machozi yasimtoke.

Wille alichukua kitambaa na kumpa Hellen afute machozi. Aligundua kuwa alikuwa amumizwa sana na kifo cha Miliam kwani anavyomjua kwa uimara wake hakutegemea kumuona akimwaga machozi kiasi kile.

"Hellen unatakiwa kuwa imara sana katika kipindi hiki. Hawa ni watu hatari sana. Nadhani nilikueleza kuhusu Liberatha. Amechukukuliwa nyumbani kwake na watu waliojitambulisha kuwa ni askari usiku wa kuamkia leo lakini nimemtafuta vituo vyote vya Polisi bila mafanikio. Kwa hiyo sijui kama bado yu hai au la" Hellen alishitushwa sana na taarifa hizo, alijikuta akimkodolea macho bila kujua la kufanya.

"Wakati unanioigia simu nilikuwa hospitali ya taifa baada ya kupata taarifa kutoka kwa askari mwenzangu kuwa kuna mwili wa mwanamke umefikishwa hospitalini hapo. Nilijua pengine ulikuwa mwili wa Liberatha lakini haikuwa hivyo. Baadaye ndipo nikafahamu kuwa ulikuwa mwili wa Miliam."

"Nilipofuatilia nikagundua kuwa mwili huo umeletwa na askari wa kituo chetu. Sambamba na hilo wamemkamata Karim kama mshukiwa namba moja wa mauaji hayo" Maelezo ya Wille yalimchanganya sana Hellen.

"Wamemkamata Karim. Yupo wapi na yupo kwenye hali gani?" Hellen aliuliza huku akiwa na wasiwasi mkubwa. "Sikubahatika kumuona maana tayari amepelekwa Ukonga na kuna taarifa kuwa kesho atapandishwa kizimbani kusomewa mashitaka ya mauji ya Miliam na Adili. Inaonekana amekiri kuhusika"

"Mungu wangu!" Hellen aligubikwa na wasiwasi mkubwa juu ya mustakabali wa Karim.Alitafakari kidogo kisha akamtazama Wille na kusema. "Karim hausiki na mauji ya Miliam, Miliam alikufa mikononi mwangu. Nilifanya jitihada zote za kuokoa maisha yake lakini ilishindikana, alikuwa amepigwa risasi ya shingo. Nilijaribu kupambana nao lakini kipaumbele changu kikawa kumuokoa Miliam, niliishia tu kumneruhi mmoja kwa risasi ya bega" Wille alishangazwa sana na maelezo ya Hellen, alizidi kuwa na maswali mengi kuliko majibu.

"Wakati anapigwa risasi alikuwa wapi" Wille aliuliza huku alichukua chupa ya pombe kali iliyokuwa mbele yake na kupiga fundo tatu mfululizo. Ni wazi kuwa alikuwa anaendelea kuchanganwa na kila anachokisikia kutoka kwa Hellen.

"Baada ya kuonana na wewe mara ya mwisho nilimuhoji Miliam na kumuuliza kuwa anaweza kufahamu mtu wa karibu na Samba ili tumtumie kumpata. Akanieleza kuwa Kuna mtu anaitwa Zomo huyo ni kundi Moja na Samba na alikuwa na anapajua kwake kwa vile walikuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa siri" Hellen aliongea.

"Umemtaja Zomo, huyo Zomo namfahamu. Nilikuwa najiuliza mara nyingi kwa nini jina la Miliam halikuwa geni kabisa maskioni mwangu na hata mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa usiku wa mkesha wa mwaka mpya akiwa na huyo Miliam aliyemtambulisha kama mpenzi wake. Namfahamu kwa sababu mara nyingi sana anakuja pale kituoni, ni maarufu pale" Wille aliongea huku akimtazama Hellen Usoni.

"Kwa hiyo mlifanikiwa kumpata Zomo" "Hapana, habari tulizozipata kwa majirani ni kuwa amefariki siku kadhaa zilizopita na jambo la kushangaza ni kuwa tulikuta nyumba yake ikiteketea kwa moto. Nilikuwa nimemwacha Miliam kwenye gari.Niliporudi ndipo nilikuta tayari amepigwa risasi. Nilimkimbiza nyumbani kwake kwa ajili ya huduma ya kwanza ,bahati nzuri nilimkuta Karim tukajaribu kupigania uhai wake lakini tulishacbelewa jeraha lilikuwa baya na alikuwa amepoteza damu nyingi" Hellen alipangusa machozi.

"Muda mfupi baada ya Miliam kufariki nyumba ilizingirwa na askari ambao walikuwa waneniungia mkia tokea kwa Zomo. Niliamua kutoroka na kumuacha Karim. Alikuwa bado ana kihoro". Wille alitikisa kichwa kuashiria kukubaliana na maelezo ya Hellen.

"Inaonekana moja kwa moja kuwa mauji ya Zomo yanahusiana moja kwa moja na mauji ya Miliam na bila shaka muuaji ni huyo huyo. Nitafuatilia kujua zaidi" Wille aliongea huku akionekana kuwa na mambo mengi kichwani.

"Nakubaliana na wewe kuwa muuaji ni huyo huyo. Kuna jambo moja sikuwa nimekwambia. Samba na Miliam pia walikuwa na mapenzi ya siri, mafahari wawili hawakai zizi moja. Inawezekana kuna namna walihitilafiana, sitolala usingizi mpaka nihakikishe nampata huyo Samba na wakubwa zake, naamini ndiye anayeendeleza haya yote. Kwa sasa kuna sehemu natakiwa kwenda kisha nirudi nyumbani kupumzika, tutazidi kuwasiliana Wille. Nakushukuru sana na uwe makini"
Hellen aliongea huku akijiandaa kuondoka.

"Kabla sijaondoka, sasa Karim tunamsaidiaje" "Kwa sasa itakuwa ngumu sana kumsaidia kwa sababu anapelekwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.Amekiri na kibaya zaidi amekutwa na siraha ndani" Wille aliongea huku akimtazama Hellen usoni.Hellen alitafakari kidogo kisha akasema.

"Hiyo siraha aliyokutwa nayo ni ya kwangu. Mimi ndiye niliyempatia Miliam hiyo bastola kwa ajili ya kujilinda awapo nyumbani. Nasikitika kuwa Karim ameingia kwenye matatizo makubwa kiasi hiki bila hatia kabisa" Wille aliwaza mambo mengi Kwa wakati huo.

"Tutaangalia namna ya kumsaidia, kwa sasa inabidi kufahamu kuwa kwa sasa maisha ya kila mmoja wetu yapo hatarini. Zidisha umakini na tahadhari kubwa. Ukikwa na tatizo lolote nifahamishe haraka sana, Mimi nipo kwa ajili yako Hellen" Wille aliongea na wakati huo wote wakainuka na kuondoka ndani ya club hii ambayo watu walikuwa wanazidi kuongezeka kadiri muda ulivyozidi kwenda.
ITAENDELEA click here to unlock the post

Mbarouk
Mbarouk @Mbarouk

RIWAYA: KIKAO USIKU WA MANANE (Sehemu ya 34)+18
MTUNZI&MWANDISHI: Sherally Mbarouk
Email: sherallymbarouk@gmail.com

Amon Chami aliingia kwenye gari lake la kisasa kabisa aina ya Nissan Patrol na kunuelekeza dereva wake kuwa wanaelekea Tandika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Aliketi kwenye kiti chake na kufunga mkanda huku akijitahidi kuvuta kumbukumbu za nyumbani kwa mama Steve.

Alikumbuka miaka mingi iliyopita aliingia kwenye mahusiano naDiana, binti mrembo ambaye ni mama Steve anayemtafuta sasa,ilikuwa ni miaka michache baada ya kuingia Tanzania akitokea nchini Uganda akiwa na rafiki yake Mzee Damas aliyekuwa ameachana na jeshi la wananchi baada ya vita ya Uganda.

Mwanzoni yalikuwa ni mahusiano yaliyojaa mapenzi moto moto lakini. Mambo yalikuja kuharibika baada ya Amon Chami kupata kiasi kikubwa cha pesa kilichotokana na mzigo mkubwa wa dawa za kulevya aina ya Cocaine walizouza baada ya kumgeuka raia wa china aliyekuwa amewaagiza mzigo huo kutoka nchini Pakistan ili waupeleke nchini Afrika ya kusini.

Baada ya vita hali ya maisha ilikuwa ngumu kwa watu wengi akiwemo Amon Chami na rafiki yake mzee Damas hawakuwa kabisa na kipato cha kutosha kutokana na kuwa Mzee Damas alikuwa ameamua kutorudi tena jeshini.

Siku moja walikutana na raia wa wawili wa kichina Liam Mee na Ching Li waliokuwa, wahandisi waliokuwa wamemaliza kujenga reli ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zanzibar miaka michache iliyopita. Wachina hao waliwaeleza Amon Chami na mzee Damas kuwa mmoja wao anaondoka kurudi nchini china siku si nyingi na mwingine ataondoka siku chache zijazo lakini kabla ya hapo kuna mzigo anataka aupeleke nchini Afrika ya kusini hivyo wanahitaji washirikiane nao kwenye kazi hiyo yenye malipo makubwa.

Hizo zilikuwa ni habari njema sana kwa Amon Chami na Dams wakiamini kuwa sasa watakabiriana vilivyo na ukata mkubwa uliokuwa unawakabiri. Walielezwa kuwa watatakiwa kusafiri na Liam Mee kuelekea nchini Pakistan kisha watapewa huo mzigo na kisha yeye atabaki nchini China wao watarudi na mzigo nchini Tanzania na kumkabidhi Ching Li ambaye atapeleka huo mzigo nchini Afrika Kusini.

Walikibaliana na Kila kitu kutoka kwa wachina hao kisha wakalipwa malipo ya awali huku wakikubaliana kulipwa kiasi cha pesa kilichosalia wakirejea nchini. Amon Chami aliipokea fursa hiyo kwa mikono miwili huku akiichikulia kama baraka iliyotokana na habari njema aliyokuwa amapewa na mpenzi wake kuwa ni mjamzito. Baadaye walikuja kufahamu kuwa kazi yenyewe itakuwa kazi ya hatari ya kusafirisha biashara haramu ya dawa za kulevya.

Hawakuona sababu tena ya kushindwa kukamilisha kazi hiyo yenye hatari nyingi. Taratibu zote za safari zilikamilika ,walisafiri pamoja na Liam Mee kupitia hadi nchini China katika Jiji la Xinjiang. Pamoja na kukaguzi mkubwa katika viwanja vya ndege Liam Mee aliwahakikishia kuwa watafanikiwa katika safari yao.

Kutoka Xinjiang waliondoka kwa basi kupitia barabara ya ushirikiano kati ya Pakistan na China iitwayo Karakoram Highway iliyokuwa imezinduliwa siku si nyingi. Safari ya zaidi ya saa ishirini hadi Khunjerab nchini Pakistan ambapo walichukua mzigo huo.

Walifanikiwa kurudi jijini Dar es Salaam na mzigo wa Cocain. Siku ya kumkabidhi Ching Li ndiyo siku hiyo walimgeuka na kumpiga risasi yeye na walinzi wake kisha wakatokomea na mzigo wote ambao baadaye waliuuza. Na huo ndio ulikuwa mwanzo wao wa kuingia kwenye mtandao mkubwa wa dawa hatari za kulevya duniani. Biashara ambayo imewapatia imaarufu mkubwa na ukwasi wa kupindukia.

Siku moja mpenzi wake Diana alikuta begi lenye dawa za kulevya chumbani, jambo ambalo liliibua mzozo mkubwa baina na wakati huo walikuwa na mtoto mchanga ambaye ni Steve.

Katika ugomvi huo Diana aliondoka na kurudi kwao Tandika katika na kama haitoshi aliahidi kufikisha habari hizo kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Jambo ambalo Amon Chami alijua kabisa ni hatari kwa usalama wake. Siku hiyo hiyo usiku Amon Chami aliibuka nyumbani kwa Diana Tandika akiwa na bunduki na kuondoka na mtoto wake mchanga Steve huku akimtishia Diana kuwa asithubutu kujaribu kumtafuta au kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama atampoteza kabisa mtoto na yeye hatobaki salama. Huo ndio ulikuwa mwisho wa kuonana wawili hawa. Ni miaka mingi sasa imepita sasa.

"Bosi tuneshafika Tandika" Sauti ya dereva ilimuibua Amon Chami kutoka kwenye lindi zito la mawazo. Walipita mitaaa kadhaa hadi walipofika kwenye nyumba moja ambayo ilionekana dhahiri kuwa inehamwa muda mrefu haikaliwi na watu.

"Simamisha gari hapa" Amon Chami aliongea huku akitazama nyumba Ile kwa umakini mkubwa "Ni hapa". Alishuka kwenye gari na kutazama nyumba ile kwa dakika kadhaa, ilikuwa imefungwa kwa kufuri.

Akiwa anaendelea kuwaza cha kufanya, mlango wa nyumba ya jirani ukafunguliwa na kutokea mama mtu mzima ambaye alikuwa anamsindikiza mjukuu wake kwenda shule.

"Mama shikamoo" "Marahaba, mwanangu, hujambo". Aliongea yule mama bila kumtazama Amon Chami usoni.
"Mama, tafadhari naomba nikuulize" Amon Chami aliongea huku akitafakari akimtazama yule mama ambaye alikaa tayari kumsikiliza.

"Naomba kujua wenyeji wa hii nyumba nimewakuta?" Yule mama alimtazama Amon Chami kwa macho ya udadisi kisha akasema.

"Mwali wa hii nyumba amefariki, baada ya binti yake kufariki mume wake naye akafariki, unenikumbusha uchungu mwanangu namkumbuka Diana" Maneno hayo yalimchoma kama mkuki moyoni. Amon Chami alihisi kizungu zungu. Haraka haraka bila hata kuagana na huyo mama aliingia kwenye gari na kuamuru waondoke eneo hilo.
******
Zilikuwa zimesalia siku mbili kabla Mheshimiwa Eliakim Mbano hajafanya kikao cha siri na viongozi wa chama chake cha PIP, Makamo mwenye kiti Mzee Jaffar Mohamed na katibu Samson Mayemba, aliamua kutumia asubuhi hii kutafakari kwa kina maelezo aliyoyapata kuhusu Jenerali Marco Lema. Hakutaka kupuuzia habari hizo.

Alichukua simu yake ya kiganjani na kupekua majina kadhaa hadi alipolifikia jina la Katibu Bariki, huyu ni kijana anayemuamini sana ambaye pia ni katibu wake kwenye ofisi ya Mbunge jimboni.

Baada ya mazungumzo mafupi wakikubaliana kukutana kwa mazungumzo zaidi katika hoteli Capriacano inayomilikiwa na mzee Damas. Alikuwa ameshamaliza kupata kifungua kinywa hivyo alijiweka sawa akavalia suti nadhifu nyeusi na tai nyekundu kisha akaelekea kwenye gari lake na kumuelekeza dereva wake wanapoelekea.

Akiwa amekaa kwenye nafasi yake nyuma ya dereva ndani ya gari hii ya kisasa aina Toyota VX V8 maalum kwa ajili ya kubeba mawaziri na viongozi wa ngazi za juu serikalini, Eliakim Mbano alikuwa akiwaza mambo mbali mbali, kubwa likiwa ni muelekeo wa kuitimiza ndoto zake za kuliongoza taifa la Tanzania. Aligutushwa kwenye lindi la mawazo na simu yake ya kiganjani.

Alipotazana mpigaji aligundua kuwa ni Daktari wake Profesa Laurian Mugisha. Haraka haraka alibonyeza kitufe cha kupokelea na kuweka simu sikioni tayari kwa kuzungumza naye.

"Shikamoo Profesa" Eliakim Mbano alianza kwa salamu baada ya kuwa hasikii vizuri sauti ya upande wa pili. "Marahaba hujambo Mheshimiwa" Profesa alisika akiongea kwa shida.

"Nimekupigia kukufahamisha kuwa Jana ulitakiwa kufanya vipimo kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa afya yako lakini mimi afya yangu sio nzuri nipo kitandani. Nitafanya hivyo nikitengamaa" "Sawa Prof. Nashukuru sana, naingia kwenye kikao kifupi baada ya hapo nitafika hapo nyumbani kwako kikujulia hali". Baada ya mazungumzo hayo simu ilikatwa huku Eliakim Mbano akitazama kwenye kitabu anachokitumia kiandika mambo yake muhimu na kugundua kuwa ni alichoongea Profea ni kweli.

Wakati huo aligundua kuwa tayari gari imeshafika kwenye maegesho ya wageni maalum ndani ya Hoteli Capriacano moja ya hoteli maarufu sana yenye hadhi ya nyota tano.Alijiweka sawa na kuteremka kisha akatembea kuelekea sehemu ya mgahawa ambapo alimkuta Katibu Bariki tayari ameshafika.

Walisalimiana kwa bashasha huku Mheshimiwa Eliakim Mbano akiketi kwenye nafasi yake. "Bariki naona inazidi kunawiri nini siri ya mafanikio yako" Eliakim Mbano alitania na wote wakaangua vicheko.

"Bariki wewe ni kijana mahiri sana, Nimefanya kazi na wewe kwa muda mrefu, hujawahi kuniangusha.Uwezo unao wewe ni mahiri sana Bariki" Mheshimiwa Eliakim Mbano aliongea, sifa ambazo sio mara ya kwanza kuzisikia kutoka kwa bosi wake,kimya kifupi kilipita,Mheshimiwa Eliakim Mbano alichukua kikombe cha kahawa na kunywa kidogo kisha akamtazama Bariki na kusema.

"Kuna jambo moja nilikuwa sijakushirikisha hapo kabla, nakusudia kugombea Urais katika uchaguzi mkuu unaokuja, hivyo hiki ni kipindi cha kufanya kazi usiku na mchana mara dufu kuliko siku zote. Nahitaji ushirikiano wa hali ya juu sana kutoka kwako" Bariki hakushangaa sana kwa taarifa hizo kwani amekua akisikia tetesi hizo kwa muda sasa. Alitikisa kichwa kuonesha kukubaliana na kila kitu.

"Unakumbuka nilikupa kazi ya kumchunguza Monica. Ile kazi uliifanya kwa ufanisi mkubwa. Sasa kuna huyu mtu anaitwa Marco Lema. Nahitaji ufuatilie nyendo zake nipate taarifa za kina humhusu. Kazi hiyo ifanyike kuanzia sasa majibu yake niyapate haraka. Yote tuliyozungumza hapa ni siri kati yetu. Sina wasiwasi wowote na wewe kuhusu hilo.Zingatia yote, nakutakia kazi njema"

Kilikuwa ni kikao kifupi sana. Waliagana, Mheshimiwa Eliakim Mbano akaingia kwenye gari na kumuelekeza dereva wake kuwa wanaelekea kwa Profesa Laurian Mugisha Makongo juu katika nyumba za Maprofesa na wahadhiri wa chuo kikuu.
*****
Baada ya Samba kumaliza mazungumzo na mzee Damas aliondoka na kwenda kuungana na wenzake Chita na Faru ambaye alikuwa anaendelea kuuguza jeraha kubwa la risasi katika bega lake. Samba hakuwa amefurahishwa kabisa kuona bado taarifa za kila anachofanya zinamfikia mzee Damas bila ruhusa yake.

Aliingia kwenye makazi yake ambayo ni makazi ya siri kati yake, Faru na Chita Huku akiwa na begi kubwaa jeusi mkononi. Huwa haruhusu mtu yeyote kufika hapo kwa ajili ya usalama tofauti na Chita na Faru. Pamoja na mapenzi yake kwa Miliam lakini hakuwahi kumleta hapo nyumbani kwake.

Alienda moja kwa moja na alipolala Faru na kutazama maendeleo ya jeraha lake kisha akafungua jokofu na kutoa chupa kubwa ya mvinyo na kuiweka mezani. Alionekana kuwa na mawazo mengi kichwani.

"Nimetoka kukutana na wazee sasa hivi. Wamefurahishwa sana na kazi ya jana usiku." Samba alianzisha mazungumzo huku akinyanyuka tena na kuchukua begi kisha akalifungua na kutoa maburungutu mengi ya pesa na kuyamwaga mezani.

"Hii pesa yote ni kwa ajili ya kula tu, kusherehekea kazi nzuri ya jana usiku" Samba aliongea na kuibua shangwe kubwa kwa Faru na Chita.

"Hata hivyo Kuna angalizo nataka nitoe hapa, inaonekana taarifa za kila tunachofanya bado zinavuja. Hatuko salama kwa asilimia zote inaonekana kuna. Ikitokea kuna mchezo mchafu unafanyika adhabu yake kila mmoja wetu anaijua". Samba aliongea kwa kumaanisha kabisa anachokisema.

Kimya kirefu kilipita, Samba alimimina mvinyo kwenye bilauri hadi pomoni kisha akabugia yote bila kupumzika. "Unajua Zomo alikuwa mshenzi lakini Hellen alikuwa mshenzi zaidi. Aliamua kutembea na sote mimi na Zomo. Mimi huwa sisalitiwi hata angejificha wapi ningemmaliza." Samba aliwashangaza sana Chita na Faru, hawakuwa wakijua kabisa kama Samba na Zomo wote walikuwa kwenye penzi na Miliam.

"Chita unachukua muda mrefu sana kummaliza yule mzee, unatukosesha pesa. Ongeza kasi katika utendaji wako wa kazi maana tupo nje ya muda. Ukitoka kwenye kwenye viwanja vya golf leo tunatakiwa kwenda club Montero kufurahia maisha. Kuna yule shombe shombe Husna nammezea mate muda mrefu leo natakiwa kuongea naye ki utu uzima. Wewe Faru utaendelea kuuguza jeraha lako hapa hatuwezi kuongozana na mgonjwa kwenye starehe" Samba aliongea. click here to unlock the post

Mbarouk
Mbarouk @Mbarouk

RIWAYA: KIKAO USIKU WA MANANE (Sehemu ya 19)+18
MTUNZI&MWANDISHI: Sherally Mbarouk
Email: sherallymbarouk@gmail.com

Karim alirejewa fahamu na kujikuta amelala chini kwenye chumba kidogo chenye mwanga hafifu, harufu mbaya na hewa nzito. Alijitahidi kunyanyuka lakini alishindwa na kuanguka chini sakafuni, alikuwa na maumivu makali sana shingoni, bega na kichwa. Aligundua kuwa alikuwa na jeraha kubwa kwenye goti la mguu wake wa kushoto. Uso wake ilikuwa unevimba kutokana na kipigo kikali alichokipata usiku.

Alivuta kumbukumbu ya kilichotokea, haraka haraka aligundua kuwa alikuwa mahabusu ya peke yake. Hofu kubwa iligubika moyo wake. Alikumbuka kila kitu kilichotokea kabla hajapoteza fahamu. Machozi yalianza kutiririka mashavuni alipogundua alipokumbuka kuwa hatomuona tena mpenzi wake Miliam katika uso wa dunia. Aliumizwa sana na kifo chake, hakutarajia kabisa kuwa atauawa kikatiri namna ile.Maswali mengi yalimzonga kichwani.

Wakati anaendelea kujiuliza ni kina nani wamemuua Miliam kikatiri namna ile na kwa nini wafanye hivyo, mlango wa chuma wa chumba hicho ukafunguliwa wakatokea askari wanne wenye bunduki kisha wakamfuata pale alipokuwa amelala wakamfunga pingu mikononi kisha wakamnyanyua na kuondoka naye bila kuzungumza naye chochote.

Alipotolewa ndani ya kile chumba aligundua kuwa vilikuwepo vyumba vingine vingi kama hivyo vikiwa na washukiwa wengine wa matukio mbali mbali ya uharifu, aligundua kuwa kuna vymba vingine vingi kama hivyo na ni chini kabisa ya ardhi. Yalikuwa ni mazingira ya kutisha sana. Karim hakuwahi kufikiria kuwa siku moja anaweza kujikuta katika mazingira ya hatari na ya kutisha namna ile.

Alipelekwa hadi kwenye chumba kingine kikubwa kisicho na dirisha kabisa lakini kina kiti na meza ndogo. Alikalishwa kwenye kiti akaongezewa pingu katika miguu yote na kumfanya atulie tuli kwenye kiti pasipo kujitingisha. Taa ikawashwa akakutanisha macho na askari mmoja mrefu mweusi na mwenye mwili wa miraba minne akiwa ameketi kwenye kiti nyuma ya meza huku akimtazama Karim kwa macho makali sana.

Wale askari wanne walikaa pembeni bila kuzungumza neno lolote. Ni dhahiri kuwa hicho kilikuwa chumba cha mahojiano.Kinya kirefu kilipita Karim akiwa hajui hatima yake mbele ya watu hawa ambao walionekana kabisa kutokuwa na hata chembe ya mzaha katika nyuso zao.

"Karim, una bahati kubwa sana kuendelea kuwa hai mpaka muda huu" Yule mtu aliyeketi mbele yake aliongea huku Karim akipatwa na mshangao mkubwa asijue watu hawa wamefahanuje jina lake.

"Bado una nafasi ya kutoka humu ndani kama ulivyonigia endapo utaonesha ushirikiano katika kila utakachoilizwa. Tofauti na hapo mzee Momo na mke wake mama Karim wataweka turubai la matanga huko kwenu Misungwi." Ni maneno yaliyomchanganya sana Karim. Alizidi kushangaa namna hawa watu wamemfahamuje kwa undani namna ile hadi kujua kwao.

"Tumekutafuta kwa muda mrefu sana lakini hatimaye tumekupata leo. Hakika mbio za sakafuni huishia ukingoni." Yule mtu alizidi kuongea huku akiachia kicheko kidogo cha kujilazimisha.

"Sasa nataka ueleze kwa nini ulimuua rafiki yako Adili. Pia ukishajibu hilo swali utasema ni kwa nini umemuua Miliam. Una muda mchache sana wa kutoa hayo majibu. Tafadhali sana usijaribu kuleta aina yoyote ya utani katika majibu yako"

Yule mtu alishika kitabu na kalamu tayari kwa kuandika maelezo. Karim alishindwa aongee nini, alikuwa yeye hakumuua Adili na kibaya zaidi hakuwa akijua hata aliyehusika na kifo chake. Alikuwa haamini kabisa hisia zake kuwa huenda Hellen amehusika na kifo cha Miliam hivyo hakuwa tayari kumtaja popote.

"Mimi sihusiki kwa namna yoyote na kifo cha Adili. Pia sihusiki na kifo cha Miliam" Karim aliongea kwa sauti dhaifu. Maneno hayo yaliwaibua wale askari waliomleta mule ndani. Kofi zito lilitua usoni mwake na kumfanya aone giza kwa sekunde kadhaa. Kabla hajakaa sawa alipigwa ngumi ya pua ikiyompekea hadi chini akibilingita kwenye kiti alipofingwa.

Walimnyanyua na kumrudisha tena kama mwanzo. Damu nyingi zilikuwa zinamtoka puani na mdomoni. Alipiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna aliyetokea kumsaidia. Hali ilizidi kuwa tete ndani ya chumba hiki cha mahojiano. Karim alikuwa anakikaribia zaidi kifo kuliko uhai.

Kilio cha Karim kilikatishwa na askari wawili walioingia kwenye chumba hicho wakiwa wanamkokota mtu ambaye alionekana dhahiri kuwa alikuwa na hali mbaya kutokana na kipigo. Mwili mzima ulijaa damu. Aliikuwa akihema kwa tabu.
Yule mtu aliyekuwa akimuhoji Karim alimsogelea yule mtu aliyeletwa na kumyanyua kisha akamlaza mbele ya Karim.

Kimya kifupi kilipita Karim akimtazama huyo mtu kwa wasiwasi mkubwa. Haukupita muda mrefu alitapatapa na kujinyoosha kisha akatulia tuli. Alikuwa amekata roho mbele yake. Karim aliangua kilio. Alijua kabisa asipokuwa makini na yeye atapoteza maisha.

"Mkuu nadhani huyu anatupotezea wakati. Tumalizane naye sasa hivi" kwa mara ya kwanza wale askari waliongea huku wakimfuata na kumfungua pingu, wakamvua shati na suruali kisha wakaunganisha na kufunga juu kwenye kenchi. Wakamnyanyua na kumfunga shingoni. Karim alijua kuwa kinachofuata sasa ni kumnyonga. Alipiga kelele bila mafanikio, hakuna aliyemsikiliza.
*****
"Mimi naondoka naenda kufanya maandalizi kwa ajili ya upasuaji. Nimempa Nasra maelekezo yote ya nini cha kufanya mpaka pale nitakaporejea. Sitokawia kurudi" Dokta Amani aliongea huku akimtazama Hellen usoni"

"Asante sana Dokta.Tayari nimeandaa kifungua kinywa, umefanya kazi usiku kucha. Sio vyema uondoke bila kupata chochote" Hellen aliongea huku akimuongoza Dokta Amani kuelekea kwenye meza ya chakula.

Dokta Amani aliketi kwenye meza iliyokuwa na aina mbalimbali ya vitafunwa na chai nzito ya maziwa. Alimtazama Hellen wakati akimimina chai kwenye kikombe. Alitaka kuongea jambo lakini akakatishwa na sauti ya Hellen.

"Nimeona hukuja na gari, unaweza kutumia moja wapo ya magari yangu " Dokta Amani alimtazama Hellen na kuachia tabasamu hafifu kisha akasema.

"Wala usijali, tayari nimempigia simu mtu wa taxi naamini atafika hivi punde" Hellen alibaki kimya huku akimtazama Dokta Amani kwa macho ya udadisi.

"Asante sana Dokta kwa kupigania uhai wa mama yangu" Hellen aliongea, Dokta Amani alimtazama Hellen bila kusema chochote kisha akashika begi lake dogo na kuondoka.

Baada ya Dokta kuondoka Hellen alielekea na kwenye chumba cha matibabu na kumsogelea Nasra aliyekuwa akimalizia kutundika dripu ya maji kwa ajili ya mgonjwa. Alimtazama kwa nukta kadhaa kisha akasema.

"Nasra ulifanya kosa kubwa sana kutuhusu mtu aingie ndani ya nyumba bila ruhusa yangu tena nikiwa sipo.Kosa kama hilo linaweza kugharimu maisha yetu sote hunu ndani. Unaweza kunieleza Dokta aliingiaje humu ndani?" Nasra alishangaa sana kusikia maneno hayo. Alichokuwa anajua ni kuwa kulikuwa na mawasiliano kati yake na Profesa Laurian Mugisha hivyo ndiyo maana Dokta Amani aliweza kufika hapo nyumbani.

"Mimi baada ya kukutafuta wewe bila mafanikio huku hali ya mama ikiendelea kuwa mbaya ghafla nilisikia muungurumo wa gari nikajua bila shaka ni wewe umefika, lakini nilipoangalia vizuri niligundua kuwa ni gari la Profesa hivyo nikaruhusu liingie. Nilishangaa sana kuona sio yeye lakini pia sikuona sababu ya kumzuia baada ya kujitambulisha kuwa amatumwa na Profesa mwenyewe" Nasra alimaliza kutoa maelezo yake ambayo yalimfanya Hellen avute pumzi ndefu kisha akasema.

"Ina maana alikuja na gari ya Profesa, Hellen aliongea kwa mshangao mkubwa kisha akaenda kuchungulia kwenye maegesho ya magari na kuona gari ya Profesa Laurian Mugisha ikiondoka sehemu ya maegesho.

"Nisamehe sana Nasra, jana ilikuwa siku ndefu sana kwangu" Hellen aliongea huku akishindwa kuelewa ni kwa nini muda wote hakuwa ameliona gari hilo aina ya Land Cruiser Defender toleo la zamani ambalo Profesa Mugisha amekuwa akilitumia kwa miaka yote tangu amfahamu. Nasra alimtazama Hellen kwa udadisi mkubwa, alitaka kuongea jambo lakini akasita baada ya simu ya Hellen kupata uhai, mpigaji alikuwa ni CID Wille.
*****
Mzee Damas aliingia ofisini kwake mapema sana zaidi ya siku zote. Alichukua simu yake ya kiganjani na kumpigia Samba kisha akampa maelekezo kuwa wakutane hapo ofisini baada ya masaa mawili. Mlango wa ofisi ulifunguliwa akaingia Dokta Amani. Mzee Damas aliweka simu yake mezani tayari kwa kumpokea kijana wake.

"Shikamoo baba" Dokta Amani alisalimia huku akishikana mkono na baba yake huku nyuso za bashasha zikitawala kwa wote wawili.

"Marahaba Dokta, karibu sana. Sikujua kama utawahi namna hii. Mimi nimeamua kufika hapa mapema zaidi kuliko kawaida ili nisionekane sijui kutunza muda" Mzee Damas aliongea huku vicheko vikitawala ndani ya ofisi hii maridadi.

"Ni kitambo kirefu kimepita sijakutembelea ofisini baba, leo nimesema nifike hapa tena alfajiri kabisa. Najua una majukumu mengi sana baba.Utaniwia radhi kwa kukuamsha mapema namna ile baba" Dokta Amani aliongea huku akifurahia umaridadi wa ofisi hiyo ya kisasa kabisa.

"Usiwe na shaka mwanangu. Nadhani unafahamu kuwa wewe ni kipaumbele changu namba moja, bila shaka natakiwa kuwepo muda wowote ukinihitaji. Na umefanya vizuri kufika hapa ofisini, ni wakati wa wewe kuanza kumtembelea ofisi zangu zote kila wakati kwa sababu mimi umri wangu sasa umeanza kunitupa mkono nitakapokuwa sipo wewe ndiye utakayevaa viatu vyangu" Mzee Damas aliongea huku akimtazama Dokta Amani ambaye alitikisa kichwa kuonesha kukubaliana na maelezo ya baba yake.

Kimya kifupi kilipita, Dokta Amani alikohoa kidogo kusawazisha koo lake kisha akasema. "Baba sitokuwa mkaaji sana hapa nitajielekeza moja kwa kwa moja kwenye kiini cha ujio wangu" Alinyamaza kidogo kisha akaendelea.

"Baba nimekuja kwako nahitaji msaada. Nina mgonjwa yuko mahututi natakiwa kumfanyia upasuaji mkubwa wa ubongo ndani ya saa ishirini na nne kuokoa maisha yake. Kuna orodha ya vifaa hapa nimeileta kwako nivipate ili niweze kumsaidia" Dokta Amani aliongea huku akamkabidhi orodha ya vifaa.

Mzee Damas alitazama Ile orodha, tofauti na matarajio ya Dokta Amani hakuonekana kushitushwa na orodha hiyo pamoja na kuwa na vifaa hivyo vilikuwa ni vya gharama sana na vinaagizwa kutoka nje.

"Hii orodha nimeiona, ni ghari" Mzee Damas aliongea huku akitafakari kidogo kisha akachukua simu ya mezani na kubonyeza namba kadhaa kisha akasema simu sikioni kwa ajili ya mazungumzo.

Alitoa maelekezo kwa mtu ambaye bila shaka ni muhasibu wa kampuni yake na kumwambia kuwa anatumiwa aordha ya vifaa kwa ajili ya matibabu na vinahitajika haraka iwezekanavyo ndani ya masaa ishirini na nne hivyo afanye taratibu zote za manunuzi vipatikane bila kuchelewa.

Dokta Amani alishindwa kuzuia furaha yake kwa kile alichokuwa anasikia na kujikuta ananyanyuka kumkumbatia baba yake kwa furaha.

"Baada ya kumaliza kutumia hivyo vifaa utavigawa kwenye Hospitali zenye uhaba kwa ajili ya kusaidia watu wengine" Mzee Damas aliongea. Dokta Amani anamjua baba yake kwa kuwa mtu mwenye roho nzuri na mtu wa kujitolea kwa watu wenye uhitaji lakini hakujua kama ni kwa kiwango hiki. Hakukaa muda mrefu aliaga na kuondoka.

Muda mfupi baada ya Dokta Amani kuondoka Aliingia Amon Chami. Alienda moja kwa moja na kuketi kwenye kiti kilichokuwa wazi. Alionekana kabisa hakuwa na bashasha kama alivyozoeleka.

Mzee Damas alinyanyuka na kuchukua kikombe vikombe viwili vidogo vya kahawa na kumimina kisha akamkabidhi Amon Chami.

"Unaonekana unechoka sana Chami, mbona umechoka mapema namna hii,sio kawaida yako." Mzee Damas alianzisha mazungumzo huku akimtazama swahiba wake kwa macho ya udadisi.

"Sikupata hata lepe la usingizi ndugu yangu. Jana usiku mwanangu Steve alianzisha jambo ambalo lilinishangaza sana." Amon Chami alikunywa kahawa kidogo kisha akaendelea. "Anataka kujua ni wapi alipo mama yake. Inaonekana maelezo yote anayoyajua siku zote kuhusu mama yake haayaamini tena, amesisistiza anamtaka mama yake nimechanganyikiwa sana" . Mzee Damas alishitushwa sana na taarifa hizo hakutegemea kabisa habari hizo kuibuka kwa wakati huo.

"Nadhani sitokuwa na namna zaidi ya kumuonesha alipo mama yake. Wasiwasi wangu ni endapo atakuwa tayari amefariki dunia maana ni miaka mingi imepita sasa tangu nilipomnyanga'anya mwanangu" Amon Chami aliongea huku akizama kwenye lindi zito la mawazo.Alishindwa kabisa aanzie wapi kumtafuta mwanamke huyo.

"Nataka nianze mara moja kujua alipo huyo mwanamke. Hili nataka nilianze haraka iwezekanavyo. Kwa leo utasogeza mbele kikao chetu, pengine tutakifanya kesho ili nishughurikie hili". Amon Chami aliongea huku akiungwa mkono na Mzee Damas. Haukupita muda mrefu akaaga na kuondoka.

Mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na safari hii aliyeingia ni Samba. Alikuwa ndani ya muda waliokubaliana. Baada ya salamu alienda kuketi kwenye kiti kilichokuwa wazi.

"Samba mmefanya kazi nzuri sana kummaliza yule binti. Ni kazi nzuri sana imefanyika. Bila kufanya hivyo alikuwa anahatarisha usalama wetu sote hapa, inaonekana alishaanza kutumika na wabaya wetu. Kwa hili unahitaji pongezi kubwa wewe na vijana wako. Kuna kiasi cha pesa mtapokea muda wowote kuanzia sasa. Hizo pesa ni mahususi kwa ajili ya kusherhekea kazi nzuri mliyoifanya" Mzee Damas aliongea huku akionesha wazi furaha yake.

Samba aliendelea kusikiliza huku akishangaa ni wapi amepata taarifa kuhusu kifo cha Miliam. Alijua kabisa huenda bado kuna mtu au watu ambao bado wanamzunguka kwenye kazi zake au wanamfuatilia kila hatua anayopita. "Kumbe pamoja na kumuua Zomo bado kuna kazi chafu unaendelea dhidi yangu". Samba aliwaza.
ITAENDELEA click here to unlock the post