Pinned Post

Ulimwengu ulinipa kisogo, mme wangu akachagua kuniacha nikiwa katika nyakati ngumu za maisha, wakati huohuo nikiwa na mtihani mzito wa kulea mtoto mwenye changamoto ngeni nisiyoifahamu iitwayo Usonji!

Nilichagua kutokata tamaa na kutokatishwa tamaa kwa juhudi na bidii niliyoiweka. Licha ya kuitwa majina ya ajabu, na watu kunidhania kuwa hata mchawi, nilichagua kusimama kwa ajili ya maisha ya mwanangu.

Nyakati ngumu nilizopitia kwa kuvumilia na kujibidiisha ndizo zilizonitengeneza na kunifanya nilivyo leo.Nimefanikiwa kusaidia na kuwa sehemu ya watu wanaogusa maisha ya maelfu ya watoto wenye usonji kwa kuanzisha taasisi iitwayo Living Together Autistic Foundation (Li-TAFO) ili kutetea haki za watoto wenye Usoji na kutoa huduma za msingi wanazozihitaji kwa ajili ya maisha yao.

Nimeandika kitabu hiki ili kuwatia moyo wamama (wazazi/walezi) wote wanaopitia nyakati ngumu katika kulea watoto wao wenye changamoto ya Usonji kwa ujumbe wa moja kwa moja wa kujikug’uta mavumbi na kuinuka tena ili waibue vipawa vya watoto wao walioaminiwa na Mungu katika kuwakuza.

Ni maombi yangu kwamba Kitabu hiki kilete faraja katika safari yako na kikawe chanzo cha matumaini mapya, nguvu na uvuvio wa kushinda
kila changamoto ambayo iko katika njia yako.

Ikiwa una mtoto mwenye usonji, ni vyema ujue kwamba hauko peke yako, Mungu bado anakuamini na kujua kwamba utashinda na kuchomoza kwa hazina zote ambazo Mungu ameweka ndani ya huyo mtoto.

Naamini nakala ya kitabu hiki haipo katika mikono yako kwa bahati mbaya. Kupitia kitabu hiki, mimi ni mwakilishi tu wa wamama/walezi
wengi wenye changamoto zilizo nzito zaidi kuliko hata yangu.

Karibu katika Safari ya Maisha ya Ushindi ya Mama na Mtoto Mwenye Usonji.

Kitabu hiki ni sehemu ya harambee ya kuwezesha watoto wenye usonji Tanzania kuweza kupata bima ya afya.

Bofya "kitufe" hapo chini, kisha fata maelezo ,ili kununua kitabu hiki. Ahsante. click here to unlock the post