clubzila |
    View all
  • Explore
  • Login
  • Getting started
0%
Syaga James

Syaga James

Active Relationship & Marriage Consultant

Get access Tsh10,000.00/mo Tip
Facebook
Twitter
WhatsApp
Email
Text message
Copy link
  • 3 Posts
  • 2 Photos
  • 1 Videos
  • 0 Audio
  • 0 Files
About me

5 Likes Kenya Member since 11 Mar, 2025 Relationship & Marriage Consultant | Helping couples build strong, lasting connections | Passionate about guiding love and harmony | DM for advice

#Mahusiano
© 2025 clubzila |
  • Terms of Service
  • Privacy
  • About us
  • How it works
  • Cookies Policy
  • Support
  • Contact us
  • Blog
  • English
    English EspaΓ±ol

Pinned Post
Syaga James
Syaga James @syagajames

Facebook
Twitter
WhatsApp
Text message

Pinned Post
Syaga James
Syaga James @syagajames

SIRI ZA MITANDAO YA KIJAMII click here to unlock the post

You must subscribe to view this post.
  • 1

1
Facebook
Twitter
WhatsApp
Text message

Pinned Post
Syaga James
Syaga James @syagajames
Akimbo alidhani ndoa ni mwanzo wa furaha, lakini kwake, ndoa iligeuka kuwa jinamizi la mateso. Kila siku ilikuwa mapambano ndani ya nyumba ya mama mkwe wake, Mama Nkechi. Nyumba ambayo ilitakiwa kuwa kimbilio la upendo ilijaa maneno makali, fedheha,yote kwa sababu hakuwa amejaaliwa kupata mtoto.

Mateso yalianza taratibu,maneno ya kejeli kutoka kwa Mama Nkechi kuhusu jinsi nyumba ilivyo kimya bila sauti ya  watoto. Lakini kadri muda ulivyosogea, kauli hizo zilianza kuwa kali na za kuumiza zaidi.

"Wewe kazi yako ni kulala na kupaka vipodozi! Hivi ndivyo mke anapaswa kuwa?" Mama Nkechi alimtupia maneno, sauti yake ikiwa kubwa kiasi cha majirani kusikia. Akimbo alisimama mbele ya kioo, akiutazama uso wake kwa huzuni. Kupaka vipodozi kulimpa faraja, njia ya kuficha maumivu na kutokujiamini ambayo Mama Nkechi alimjengea.

"Huna maana yoyote! Huwezi hata kunizalia mjukuu," Mama Nkechi aliendelea kumshambulia kwa maneno.

Mumewe Akimbo, Obinna, alikuwa anaamka mapema kila asubuhi kujiandaa kwenda kazini, huku Akimbo akibaki kitandani, mzigo wa matumaini yake yaliyoshindwa ukimlemea. Mama Nkechi alikuwa anaamka alfajiri, anagongesha vyombo kwa sauti kubwa anapokuwa anaandaa kifungua kinywa kwa mwanae. Kila mlio wa sufuria ulimkumbusha Akimbo jinsi anavyoonekana kuwa mzigo.

"Huwezi hata kuamka kumpikia mumeo chai ya asubuhi?" Mama Nkechi alimtupia maneno kwa dharau kila alipopita karibu na chumba cha Akimbo.

 "Wewe ni mvivu, kama mabinti wote wa siku hizi. Hivi una mchango gani kwenye  ndoa hii?"

Akimbo alijitahidi kuvumilia. Alilala kitandani usiku kucha, machozi yakimtiririka usoni, akamuomba Mungu ampe mtoto, ili awe kuyamaliza mateso yake. Lakini maombi yake hayakujibiwa, na kila siku, kejeli na dharau viliongezeka.

Mama Nkechi hakuishia kwenye matusi pekee. Alimnyima Akimbo hata maji ya kunywa. 

"Usiguse hayo maji!" aliwaka kwa hasira. 

"Huwezi kula wala kunywa ndani ya nyumba hii mpaka uniletee  mjukuu. Unadhani unaweza kuishi hapa bure?"

Akimbo, mwenye njaa na kiu, alisimama kimya, machozi yakimtiririka huku akiona glasi ya maji ikinyakuliwa kutoka mikononi mwake. Alijihisi kama mfungwa ndani ya ndoa yake.

Usiku ulikuwa mbaya zaidi. Akimbo hakuweza kulala. Na mara chache alipofanikiwa kuzama usingizini, Mama Nkechi alimpigia kelele au hata kummwagia maji ya baridi usoni.

 "Amka, mwanamke usiye na maana!" aliunguruma. 

"Unawezaje kulala wakati kijana wangu hana mtoto? Umeiletea aibu hii familia."

Mateso haya yalizidi kuwa magumu. Mama Nkechi alianza kumdhalilisha Akimbo mbele ya mumewe, Obinna, lakini Obinna alikaa kimya, hakuingilia kati. 

"Nitamtafutia mwanangu  mwanamke mwingine," Mama Nkechi alitishia siku moja, uso wake ukiwa umejaa hasira. 

"Mwanamke kamili, mwenye uwezo wa kunizalia wajukuu."

Moyo wa Akimbo ulivunjika. Alishawahi kusikia vitisho kama hivyo, lakini safari hii vilionekana kuwa halisi. Kesho yake, Mama Nkechi alirejea kutoka kijijini akiwa na binti mdogo aliyeitwa Nyakunzila.

"Huyu ndiye aina ya mwanamke kijana wangu anamhitaji," alitangaza kwa majivuno. 

"Ni mwenye nguvu, mwenye bidii, na atanizalia wajukuu."

Akimbo alihisi dunia inamkimbia. Fedheha ilikuwa kubwa. Mama Nkechi alianza kumtambulisha Nyakunzila kama mke halali. Binti huyo alimtazama Akimbo kwa dharau, kana kwamba tayari alikuwa ameshinda vita.

Lakini mambo yalianza kushangaza. Siku moja, Mama Nkechi alitangaza kwa furaha kuwa Nakunzila alikuwa na ujauzito.

"Hatimaye!" Mama Nkechi alishangilia, akacheza kwa furaha. 

"Mjukuu wangu anakuja! Hivi ndivyo mwanamke wa kweli anavyopaswa kuwa. Si kama wewe, Akimbo!"

Akimbo alihisi kama chatu amemmeza. Aliwezaje kuwa mjamzito kwa haraka hivyo? Alijiona kama ameshindwa kabisa.

Lakini ghafla, ukweli ulidhihirika. Wakati Mama Nkechi na Nyakunzila walipoenda hospitali kwa ajili ya vipimo vya kawaida, daktari alifafanua jambo la kushangaza.

Nyakunzila alikuwa tayari ana ujauzito wa miezi mitatu!

Mzozo mkubwa ulitokea nyumbani. Ilikuwaje awe mjamzito kwa miezi mitatu wakati nyumbani hapo alikuwa na mwezi mmoja tu?

Akiwa amejawa hofu, Nyakunzila alikiri ukweli. 

"Mimba hii si ya Obinna," alilia kwa sauti dhaifu. 

"Nilipata mimba nikiwa kijijini kabla sijaletwa hapa. Mpenzi wangu wa zamani ndiye baba wa mtoto."

Nyumba ilitetemeka kwa mshangao. Mama Nkechi, akiwa amedhalilika kabisa, alinyamaza. Uso wa Obinna ulijawa na hasira kali alipomtazama mama yake.

"Ondoka," alisema kwa sauti kali isiyo na huruma. 

"Wewe na huyu binti, tokeni kwenye nyumba yangu. Siwezi kuamini kuwa umenifanyia haya."

Mama Nkechi, akiwa ameanguka na mpango wake kuvunjika vipande vipande, hakuwa na budi ila kuondoka tu, akamkokota binti aliyetamba nae..

Wiki moja baadaye, kabla ya hali kutulia kabisa, Akimbo alianza kuhisi mabadiliko mwilini mwake. Kwa hofu na matumaini yaliyofifia, alienda hospitali. Alipata habari ambayo hakuitarajia,alikuwa mjamzito.

Obinna, akiwa na furaha isiyo na kifani, alimkumbatia Akimbo, machozi ya furaha yakitiririka usoni mwake. 

"Tutakuwa wazazi," alishusha pumzi nzito ya faraja. 

"Baada ya haya yote, hatimaye tutakuwa na familia yetu."

Moyo wa Akimbo ulijaa shukrani. Baada ya mateso yote, machozi yote, na fedheha zote, aliuvuka moto wa majaribu akiwa mwenye nguvu kuliko mwanzo. Sasa, nyumba ile iliyokuwa huzuni ilijaa upendo na tumaini jipya.

π—¨π—π—¨π— π—•π—˜ π—ͺπ—”π—‘π—šπ—¨ π—žπ—ͺπ—”π—žπ—’ 𝗠π—ͺπ—”π—‘π—”π— π—žπ—˜ π—¨π—‘π—”π—¬π—˜π—¦π—’π— π—” π—›π—œπ—œ:
Najua moyo wako unatamani sana kubeba mtoto wako, na safari hii inaweza kuwa ngumu na yenye changamoto. Lakini kumbuka, kila kitu kina wakati wake, na wewe ni shujaa wa safari hii. Mungu hajachelewa, na baraka zako zinakuja kwa wakati wake muafaka. Endelea kuwa na imani, jipe moyo, na endelea kujiandaa kwa furaha inayokuja. Unastahili kila mema, na usipoteze tumaini..
Mwisho.

4 1
Facebook
Twitter
WhatsApp
Text message

Fill Your Details
Login with Google
or
Forgot Password?
    Don't have an account?
    Two-Step Authentication
    We have sent you a code to your email
    Resend code