UMAFIA KIGOMA

In the entire animal kingdom, a human is a very complex animal.

Of all the animals in the kingdom, instead of being equipped with the capabilities of distinguishing good deeds from evil ones, a human can perform very unimaginable mayhem on his fellow without any sense of amnesty.

For swahili audience, Binadamu ni kiumbe kisichotabilika! Ingawa kati ya wanyama wote, binadamu amepewa uwezo wa kutambua mema na mabaya, mnyama huyu anaweza kuishangaza dunia kwa kuyenda kitendo cha kinyama kisichotarajiwa dhidi ya binadamu mwenzake.

Sunday 3rd July, 2022 KAGANZO VILLAGE KAKONKEMWE HAMLET MWANDIGA WARD KIGOMA Wanandoa wawili wanaamka asubuhi hii kwa ajili ya sala ya asubuhi. Wanandoa hawa ni Olida Sauli Mkunze na mumewe Ezekiel Cheche.

Ilikuwa ni kawaida kwa wanandoa hawa kuwa, kabla ya kuanza kwa sala, Olida alikuwa akienda kumuamsha dada yake aitwaye Tilifela Toyi aliyekuwa akiishi nyumba ya jirani tu na kwao, ili wajumuike naye kwenye sala.

Huyu Tilifela, alikuwa akiishi na mtoto wake wa kiume aitwaye January. In a nutshell, January ni kijana shababi mtu mzima ambaye alikuwa ameshaoa hivyo aliishi na mkewe kwenye nyumba ya mama yake.

So, asubuhi hii kama kawaida, Odila akawa ameenda kwenye nyumba ya dada yake ili amuamshe kwa ajili ya sala ya asubuhi.

She only ended into disappointment! Olida alipofika nje ya nyumba akapaza sauti kumuita dada yake.

Hakuitikiwa!

Odila akasogelea mpaka kwenye dirisha la chumba alichokuwa analala dada yake. Akaita tena sana! She only met a dead silence.

Hakuitikiwa tena! Hii haikuwa kawaida! Siku zote Olida alikuwa akimkuta dada yake yuko macho hivyo kutotumia nguvu kubwa kumuamsha

Sasa Olida ikamlazimu asogelee mlango mkuu wa kuingilia ndani ya nyuma

Akakuta mlango ukiwa haujafungwa kwani ulifunguka mara tu alipousukuma. Hapa ndipo Olida akapokelewa na tukio la kuogofya.

Tilifela Toyi, dada wa Olida alikuwa amelala katikati ya dimbwi kubwa la damu huku mwili wake ukiwa bila dalili yoyote ya uhahi.
(SUBSCRIBE HAPO CHINI KUSOMA MAKALA KAMILI NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA ) click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

THE LAWYERS

Sometimes March 2013 Wakili Fatuma Karume alisafiri kutoka Dar kwenda mkoani Kilimanjaro.

Wakili huyu alikuwa amesafiri akiwa amebeba nyaraka furani ya muhimu.

Nyaraka ile alikuwa anaenda kumsomea na kumkabidhi mzee fulani aliyefahamika kwa jina la Juma Actually, Mzee Juma naye alikuwa ni wakili ambaye sasa amestaafu akiwa amefanikiwa kurithisha taaluma hiyo pia kwa mwanae ambaye alikuja kuwa ni wakili maarufu sana mkoni Arusha.

Fatma hakujua kama nyaraka aliyobeba ingeleta taflani kubwa ndani ya familia ya Mzee Juma. Fatma aliwasili nyumbani kwa ambako alikuta waombolezaji ambao walikusanyika baada ya kusambaa taarifa za msiba za mmoja wa watoto wa Mzee Juma.

Fatma alitegemea kuikuta hali hii nyumbani pale na hata safari yake ilitokana na yeye kupata taarifa hizi. Fatma alikuwa amebeba nyaraka ambayo ulikuwa ni wosia wa marehemu mtoto wa Mzee Juma aliouandika mbele ya wakili Karume enzi za uhai wake.

Baada ya Fatma kukaribishwa na kutoa pole kwa wafiwa, akafungua wosia ule na kuanza kumsomea mzee Juma.

Hapa ndipo utata ulipoanzia.. Ukiachana na mambo mengine yaliyokuwemo ndani ya wosia, marehemu aliagiza kuwa mauti yakimkuta, azikwe kijijini Momela wilayani Arumeru.

Mzee Juma aliposomewa eneo hili, ghafla akageuka mbogo Akajiapiza kuwa kama mwanae hatazikwa nyumbani kwake Marangu, hatashiriki maziko.

Jambo hili likaibua sekeseke kubwa pale msibani huku minong’ono ikianza kuenezwa. Kuwa marehemu mwanae hakuwa kwenye mahusiano mazuri na baba yake siku za mwisho za uhai wake.

Baba na mtoto wakiwa hawaongei kwa zaidi ya miaka miwili hadi mauti yanamkuta mtoto huyu.

Mzee Juma ambaye alishikilia rekodi ya kuwa wakili wa kwanza kuapishwa baada ya uhuru wa Tanganyika, alikuwa ni mtu wa misimamo mikali ambaye alijijengea heshima kubwa miongoni mwa watu mashuhuri nchini

Nini ilikuwa shida baina ya Mzee huyu na mwanae?

(SUBSCRIBE HAPO CHINI KUSOMA MAKALA KAMILI NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA ) click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

THE ASSASIN

Kitendo cha mtu huyu kuingia bila kupiga hodi kwenye ofisi yake ya mapokezi,kilimshitua binti huyu.

Mwonekano wa mtu huyo ulimfanya binti huyo aamini huyu si mgeni wa ofisi yake bali amekosea njia kwani ilikiwa ni mara ya kwanza kumuona mtu yule Binti akagundua jambo lingine Sura ya mgeni yule haikuwa ya kiungwana.

Alionekana kutoyafurahia maisha kwa ujumla Binti akabaki akimtazama mgeni huyu akisubiri kuombwa msamaha wa kukosea ofisi Haikuwa vile! "Jimmy yupo?" Aliuliza mgeni yule bila ya salamu Ikawa zamu ya binti kushangaa Mtu anayeuliziwa na mgeni huyu wa ajabu alikuwa ni bosi wake.

Hakufanana na mtu anayeweza kufahamiana na bosi wake hadi kumtaja kwa wepesi kama anamuongelea muhuni tu wa mtaani.

"Jimmy yupo?" Mgeni akauliza tena

Binti:"Kwani wewe nani?"

Mgeni: "Kwa hiyo yupo?"

Binti: "Yupo lakini ana kikao"

Mgeni: "Mwambie Leno yupo hapa"

Binti: "Akiwa kwenye kikao hataki kupigiwa simu wala kufuatwa"

Mgeni huyu mwenye macho mekundu kama aliyechelewa kulala na kuwahi kuamka akamtizama binti machoni kisha akatamka:- "Kwa hiyo huendi kumwambia?"

Swali lile lilimtisha binti aliamini kuna hatua atakayochukua mgeni yule endapo atashindwa kwenda kumuita bosi wake

Binti: Ngoja nikamwambie

Msichana yule akaelekea ilipo ofisi ya bosi wake Jimmy Kizota, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ilipo ofisi ya binti huyu alikuwa amemaliza kuongea na simu wakati binti huyu anaingia ofisini mwake.

Akampasha juu ya mgeni wa ajabu aitwaye Leno Sura ya Jimmy ilajenga Nuru Akamwambia binti huyu aitwaye Zakia kuwa alimtarajia Jimmy akamuagiza Zakia akamuandalie chai mgeni yule na amwambie amsubiri.

Zakia akarudi na kumkuta yule mgeni kasimama palepale

Zakia: Anasema umsubiri

Leno: Atatoka baada ya muda gani?

Zakia: Nadhani hatachelewa, nikuandalie chai au kahawa?

Mgeni akamshangaza tena Zakia

Leno:Nataka urudi tena ofisini kwake!

Zakia:Si nimekuambia ana kikao?

Leno akaongea kwa utulivu "Ni juu yako kuamua, kwenda au kutokwenda, nataka ajue tu zikipita dakika tano kama hajatoka, naondoka"

Zakia bila kupenda akarudi ofisini kwa bosi wake na kumpasha habari hii mpya Zakia alitegemea bosi wake angetoa jibu la kifedhuli alirudishe kwa mgeni huyu asiye muungwana Akashangaa bosi wake anajibu:- "Sawa nimeelewa, huyu mtu namjua mwenyewe" Akamuamuru Zakia amruhusu aingine ofisini kwake.

Jimmy Kizota na Leno Kanaga walijuana tangu utotoni jijini mwanza.

Wakasoma darasa moja shule ya msingi Nyegezi Jimmy ambaye ni mpole ndiye aliyenufaika kuwa rafiki wa Leno mwanafunzi nunda Wanafunzi manunda waliogopa kumgusa Jimmy kwa sababu ya ukaribu wake na Leno Walipomaliza shule ya msingi wakapotezana

Jimmy alipofaulu na Leno kufeli Miaka ikasogea Jimmy akajiunga chuo kikuu cha Dar es salaam Huku akisikia Leno alijiendeleza kielimu mkoani Shinyanga hadi kidato cha nne

Baadae akasikia ameajiriwa na JWTZ mkoani Tabora Miaka ikasogea Jimmy akafungua kampuni ya dawa za kusafisha maji

Akasikia Leno alifukuzwa jeshi akihusishwa na uporaji Fedra katika benki moja Tabora Tukio hilo lilitikisa na kuwa Habari ya mjini Leno akakutwa na hatia na kufungwa miaka 15 Miaka ikakatika Jimmy akafiwa na baba yake Mwanza Msibani akakutana na Leno.

Jimmy akaambiwa Leno amekuwa jambazi aliyekubuhu akishirikiana na wanajeshi waasi wa Burundi wakiteka mabasi na kupora abiria Miezi michache baadae Jimmy akasikia Leno amekuwa muuaji wa kukodi jijini Kampala

Ikapita miaka miwili bila Jimmy kupata habari za Leno Haikumsumbua kwa kuwa hakuwa na mpango nazo Ni mpaka Jimmy alipopata shinikizo fulani ndio akaanza kumtafuta Leno Jimmy akamtafuta Leno hadi akakaribia kukata tamaa Ndipo akatonywa Leno kaonekana Mwanza Jimmy akapata mawasiliano ya Leno Akampigia simu kumtaka afanye hima kuja Dar kwani kuna kazi ya donge nene anataka kumpatia

Jimmy hakumweleza ni kazi gani na aliahidi kufanya hivyo Leno akifika Dar Jimmy akamtumia Leno nauli Pia akampangia hoteli atayofikia maeneo ya Mwenge Leno alifika Dar kwa basi usiku bila kumuona Jimmy stand kumpokea Akampia simu Jimmy Jimmy akamuelekeza akodi Taxi aende Mwenge kwenye hoteli aliyompangia Akamtajia majina mawili aliyoaandikisha ayataje apewe chumba Katika majina yale hakukuwa na hata jina moja la Leno Jimmy akamsisitiza Leno asitaje jina la Leno popote.

Leno alipofika Mwenge na kupewa chumba akampigia tena simu tena Jimmy kumtaarifu amefika Jimmy: "Kesho saa nne asubuhi tuonane ofisini kwangu" akamwelekeza ilipo Hii ndio ilikuwa sababu ya mgeni huyu kufika ofisini hapa Leno aliingia ofisini kwa Jimmy wakatazamana usoni Mwonekano wa Leno ulimshtua Jimmy Leno aliyemwangalia siye yule aliyesoma naye darasa moja Nyegezi Primary school

Huyu alikuwa ni Leno mwingine Sura yake ilijieleza kila kitu Sura ya jambazi na muuaji aliyekubuhu! Leno aliupongeza uamuzi wa waliomtuma kumtafuta Leno Kuwa Leno alikuwa ni mtu sahii aliyehitajiwa. "Karibu kiti Leno" Jimmy akavunja ukimya Leno akaketi

Jimmy: Karibu Dar

Leno: Nimekuja Dar kwa ajili ya wito wako, hebu nieleze umeniitia?

Jimmy akajua Leno hapendi Blah Blah "Nina taarifa zako Leno" Jimmy akavunja ukimya

Leno: Taarifa zipi?

"Umekuwa Assasin" Jimmy akampasukia Leno Tofauti na alivyotarajia kuwa kauli ile ingemshitua Leno,

Leno alibaki akimkodolea macho bila tashwishwi yoyote "Nieleze ulichoniitia"

Leno akamwambia Jimmy

Jimmy: Naitaji taaluma yako ya uuaji kuna donge nono ukiitumia taaluma hiyo hapa Leno akaendelea kumtazama bila dalili ya kujibu lolote

Jimmy: Kuna milioni 20 ziko mezani zikikusubiri ufanye kazi hiyo Leno akamtazama Jimmy kisha akauliza "Unataka nifanye nini?"

Jimmy: Kuna mtu nataka azimishwe

Leno: Yuko wapi?

Jimmy: Hapahapa Dar

Leno: Anahusika na nini?

Jimmy: Ni mfanyabiashara

Leno: Mkubwa?

Jimmy: Si sana ila maarufu

Leno:Anatembea na ulinzi

Jimmy: Ndiyo Leno:Anajihusisha na siasa?

Jimmy: Hapana Usaili ukaendelea

Leno: Anaonekana adharani

Jimmy: Hapana

Leno: Anajua anawindwa auwawe?

Jimmy: Kwa hili hajui

Leno: Anajua kama ana adui?

Jimmy: Anajua ndio maana anatema na ulinzi

Leno: Ni adui yako?

Hapa Jimmy akasita kisha akajibu "ndiyo" Kusita huku kukaonekana na Leno

Leno: Anajua ipo siku utakuja kumuua?

Jimmy: Ndiyo

Leno: Unadhani ipo siku anaweza kukuua?

Jimmy: Ndiyo Leno akatafakari kwa muda kisha akasema "Nahitaji milioni 30, 15 kabla na 15 baada ya kazi"

Jimmy: Nyingi sana Leno:(Huku akiinuka) Tafuta mtu mwingine

Jimmy: Subiri Jimmy: Sawa nimekubali

Leno akaomba apewe wiki moja arudi Mwanza akirudi atakuwa tayari kwa kazi Wakakubaliana atachukua advance akirudi ila apewe nauli ya kwenda na kurudi Mwanza Leno akamtaka Jimmy akirudi awe na taarifa zote kumuhusu anayetakiwa kuzimishwa

Baada ya wiki Leno akarudi Dar bila kumtaarifu Jimmy Safari hii alijitafutia hoteli nyingine tofauti na aliyopangiwa na Jimmy Hata jina aliloandikisha hotelini lilikuwa bandia Akaenda kwa kushtukiza ofisini kwa Jimmy

"Umekuja lini" Jimmy aliuliza

Leno: Tuanzie tulipoishia Jimmy kwanza alimpigia simu Zakia kumwambia kutoruhusu mtu yeyote aingie ofisini kwake Kikao kikaanza Jimmy akampa Leno picha ya mtu anayetakiwa kuuwawa, Leno akaitazama na kuitia mfukoni Usaili ukaanza tena

Leno: Analindwa na walinzi wangapi?

Jimmy: Wanne (Dereva anayemwendesha na mlinzi mwingine mmoja ambao wanakuwa kwenye gari lake, wengine wawili ni dereva na mlinzi wanaokuwa kwenye gari inayowasindikiza)

Jimmy akampa picha ya hali ya ulinzi nyumbani kwa target

Leno: Nani atanipeleka kwenda kuona nyumba anayoishi?

Jimmy: Nitakupeleka

Leno: Nahitaji pia kumuona binasfi huyu mtu

Jimmy: Hilo usijali, nitakupeleka mwenyewe kukuonesha

Leno alamwangalia Jimmy kisha akamuuliza "Nani yuko nyuma ya mpango huu?"

Jimmy: Unamaanisha nini?

Leno: Namaanisha aliyeamuru mtu huyu auwawe

Jimmy: Ni mimi mwenyewe

Leno akatoa tabasamu la karaha kisha akasema "Huonekani kutoa amri hiyo!

Mambo kadhaa yanathibitisha unatumiwa"

Leno: Unakumbuka uliniambia kuwa wewe na mtu huyu ni maadui?

Jimmy: Ndiyo Leno: Na uadui wenu ndio unaopelekea kutaka huyu mtu auwawe?

Jimmy: Ndiyo

Leno: Kama ni adui yako, unakuwa vipi tayari kwenda kunionesha, ina maana hakujui?

Jimmy akawa bubu Leno akaongeza swali, "Lakini pia, inakuwaje mwenzio ajitambue ana adui akajiwekea ulinzi na wewe adui wake usiwe na ulinzi wowote?

Jimmy akatoa macho kama anasoma talaka Leno akazidi kumpasukia Jimmy

Leno: Huna ulinzi wowote hapa ofisini na naamini hata nje hapa. Usiniambie hujui hatari inayokukabili kama kweli huyu ni adui yako.

Huwezi kukubali kunilipa milioni 30 alafu ukafanya ujuha huu. Huonekani kuchezwa na machale yotote. Mtu anayewindwa haishi hivyo" Leno akapasuka

Leno: Nina hakika unatumika katika mpango huu na anayekutuma hataki ajulikane. OK hilo si tatizo langu, nilichotaka kukuonesha ni kwamba mimi sio mtu niliyezubaa, mkawa na wazo baadae mnizike pesa yangu ya kumalizia. Sitajali kujuana kwetu, nitakushukia na kukushughulikia! Ingawa ofisi ile ilikuwa na kiyoyozi, Kijasho chembamba kilimtoka Jimmy Akajitutumua na kujibu "Hakuna atakayekudhulumu, Inaonekana huniamini?"

Leno: Kwenye pesa simwamini mtu yeyote hata mimi mwenyewe

Jimmy: Kwa hiyo utafanya kazi ?

Leno: Ukinipa advance nafanya

Jimmy akafungua kabati na kutoka mkoba uliojaa mabunda ya pesa

Leno akaufungua akawa anahesabu mabunda

Leno: Lini utanipeleka kwenye nyumba ya target pamoja na kumwona yeye mwenyewe?

Jimmy: Leo usiku nitakupeleka ukamwone

Leno: Wapi Jimmy: Kwenye casino yake maarufu nadhani unaifahamu

Leno: Inaitwaje? Jimmy: Casino Afrikando

Leno: Naisikia, Yeye ndiye mmiliki?

Jimmy: Ndiyo, Nakuonya usimchukulie poa kwa kuwa mmiliki. Ni mtu hatari na mafia wa kutupwa

Leno: Anaitwaje?

(SUBSCRIBE HAPO CHINI KUSOMA MAKALA KAMILI NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA ) click here to unlock the post

15th November 2002

7:30 AM Dar Es Salaam,

Muda huu, Asubuhi hii, wafanzakazi wengi ndio huwa wanaripoti maofisini mwao baada ya kupambana na foleni za barabarani zisizoisha

Ndivyo ilivyokuwa kwa wafanyakazi wa CRDB benki tawi la Azikiwe

Uzi

AZIKIWE ROBBERY

Wafanyakazi wa benki hii walikuwa ndio wanaingia kazini asubuhi hii

Kwa taratibu za Operation za benki, huwa kuna wafanyakazi wanaondoka na ufunguo wa benki

Usishangae nikikuambia kuwa benki inafunguliwa kwa zaidi ya funguo moja

Na hizi funguo hukaa kwa watu tofauti

So ingawa mtu ataondoka na funguo,

Yeye pekee hataweza kufungua lango la benki mpaka awepo mwingine mwenye funguo nyingine.

Hivyo hawa wakaao na funguo hutakuwa kuwahi mapema sana kila siku.

Mara nyingi huwa ni Managers au wasaidizi wao

So ingawa mtu ataondoka na funguo,

Yeye pekee hataweza kufungua lango la benki mpaka awepo mwingine mwenye funguo nyingine.

Hivyo hawa wakaao na funguo hutakuwa kuwahi mapema sana kila siku.

Mara nyingi huwa ni Managers au wasaidizi wao

Kama ilivyo kwa lango la kuingilia benki, Hata wanaokaa na funguo za strong room huwa ni watu tofauti kila mtu akiwa na funguo yake.

Asubuhi hii wakaingia pale watu watatu kupitia mlango wa Staffs wa Benki

Watu hawa walikuwa na taarifa sahii kwa wakati sahii.

Walijua wateja wa benki huruhusiwa kuanza kuingia saa 2 asubuhi

Hivyo kwa muda ule wangewakuta tu wafanyakazi pekee ndani ya benki

Ni kwamba muda huo waliingia majibaba watatu wakiwa wamevaa sare kama za wafanyakazi wa benki ile.

Zaidi ya yote majibaba haya yote yalikuwa yameshikilia bastola mikononi mwao.

Pale amri ikatolewa wafanyakazi wote walale chini

Kisha wakata majina ya watu wawili wasimame

Naam!

Walitangaza kuwa, kati ya watu waliolala kama kuna mtu anaitwa BOAZ na mwenzake aitwaye MWANGOMELA wasimame haraka

Wawili hawa ndio walikuwa na funguo za strong room na kila mtu alikuwa na funguo yake tofauti na ya mwenzake

Si vibaya pia ndugu msomaji ukielewa kuwa jana yake tu kabla ya masaa ya kufungwa kwa benki hii, kulikuwa na kiasi kikubwa saba cha pesa kiliingizwa kwenye tawi hili

Naam!

Dola Milioni 1 za kimarekani

Na sasa wenye funguo ya chumba cha fedha wanatakiwa kusimama

Balaa likaanzia hapa

(SUBSCRIBE HAPO CHINI KUSOMA MAKALA KAMILI NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA) click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

NDIVYO SIVYO

Tarehe 11 Nov 2013, majira ya saa 4 usiku, Rajabu Hassan Khalfani ambaye ni dereva wa bodaboda mjini Chalinze, anarudi kijiweni kwake baada ya kutoka kumpeleka mteja maeneo ya Chalinze Mzee

Njiani anaona gari dogo jeusi likiwa limepakiwa pembeni barabarani huku watu sita wakiwa wamesimama nje ya gari. Infact gari lile halikuwa jeusi, bali lilikuwa lina rangi ya dark green lakini kwa usiku ule lilionekana kama jeusi.

Yes! Ilikuwa ni gari ndogo alina ya Nissan Cefiro

Watu waliokuwa kwenye ile gari, wakampa ishara Rajabu kama watu wanaohitaji usafiri wa pikipiki. Rajabu akasimama na mmojawao akapanda pikipiki ile Lakini ni kama wenzake hawakuridhika na hatua hiyo hivyo wakawa wanabishana na aliyepanda pikipiki akashuka.

Badala yake watu wale wakamwambia Rajabu kuwa gari lao limepata breakdown hivyo akifika chalinze mjini awasaidie kuwaletea fundi Makanika nao watamlipa ujira wake

Rajabu akakubali, na akawaachia namba zake za simu Rajabu “akachapa rapa” kwenda Chalinze Mjini

Waliokuwa na umiliki wa gari lile walikuwa ni wawili Wengine wanne, walikuwa ni abiria waliokuwa wamelipishwa pesa katika gari ile

Rajabu alipofika Chalinze, na huku akiwa ameshaanza kumtafuta fundi kwenye gereji mbalimbali, simu yake ikaita! Alipoipokea akabaini imetoka kwa wale watu walioharibikiwa gari. Kitu alichoambiwa sasa ndio kikaanza kumchanganya

3 Days Before

BUGURUNI POLICE POST

8th Nov 2013

Askari namba E 4564 Detective Corporal Dotto aliingia zamu tangu saa 12 asubuhi na kwa mujibu wa ratiba, angekaa mpaka kesho yake tarehe 19 Nov 2013

Askari huyu alikuwa kitengo cha Anti robbery ndiye aliyekuwa shift incharge siku ile

Majira ya saa 5 usiku ikaingia simu ya upepo

Simu ile ilitoka makao makuu ya polisi chumba cha mawasiliano

D/CPL Dotto aliposikiliza simu ile, alibaini kuwa kuna watu maeneo ya Jeti, Kiwalani wameona mwili wa mtu uliotupwa pembeni ya barabara iliyo karibu na godown maarufu kwa jina la
“Kwa Frenki”

Simu hii ilimtaka kachero Dotto kufatilia tukio lile.

D/CPL Dotto akakusanya haraka askari wakaelekea eneo la tukio.

Pale wakakuta mwili wa mwanaume,usio na fahamu,ukitoka povu mdomoni na damu masikioni na puani.

Walipowahoji mashuhuda jinsi mtu yule alivyofikishwa pale, wakajibiwa kuwa waliona mtu yule akitupwa pale na watu walioshuka kutoka kwenye gari.

Askari wakauchukua mwili ule, wakaandaa PF3 na kuupeleka hospitali ya Amana.

Baadae mwili ule ukahamishiwa Hospitali ya Muhimbili kitengo cha dharula akiwa bado hauna fahamu.

Mtu yule aliendelea kukaa bila fahamu kwa muda wa siku tisa.

Polisi wakiwa na shahuku azinduke ili aeleze yaliyomsibu.

Masaa machache kabla ya mwili kuokotwa siku ile,

8:00 PM

MASHUJAA BAR, VINGUNGUTI

Majira ya saa 2 usiku, wanaonekana vijana wawili wakinywa bia na kula nyama choma za “mafungu”

Nafikiri kila mtu anajua kuwa eneo hili ni maarufu kwa kuuza
“Marginal parts” za wanyama

Hapa namaanisha masikio,makende(grenades), pua, na miguu ya ngo’mbe vinauzwa kwa mafungu

Kwa hiyo vijana hawa walikuwa wakinywa bia huku wakishushia na supu ya pembe za ngombe

Pembeni yao wakiwa na vidosho kutoka KIMBOKA BY NIGHT

Walikuwa wakiiba muda ili waonane na fundi mmoja ambaye alikuwa wa muhimu sana kwao.

Bila kujua kikulacho ki ndani yako

Ni kwamba wale waliokuwa wanakunywa nao, hawakuwa vidosho yaaani,

Walikuwa ni watu proper kama bodaboda wa Makumbusho

Narudia tena,
Kiboko akikwambia Mamba anaumwa, Mwamini

(SUBSCRIBE HAPO CHINI ILI KUPATA MUE3NDELEZO WA MAKALA HII NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA) click here to unlock the post

FBI in Tanzania
By Fortunatus Buyobe

Mwanza, Tanzania
21st May 1996
Ilikuwa ni Jumanne ya vilio jijini Mwanza baada ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba.
Najua unajua lakini niazime sikio

Wakati watu wakiwa kwenye majonzi ya kupoteza wapendwa wao kwenye ajali ile, kuna kijana mmoja mwenye muonekano wa kisomali alikuwa makini sana kwenye kukagua kila maiti iliyoopolewa na kuletwa ufukweni.

Kijana huyu alionekana kama kachanganyikiwa

Kijana huyu aliyekuwa na uraia pacha wa Kenya na Comoro alikuwa ni kijana muungwana na mkimya

Wachache walimfahamu kwa kuwa walisali naye msikiti mmoja huko mtaa wa Utemini Mkolani.

Wengi walimjua kijana huyu kama mfanyabiashara wa samaki na alimiliki mitumbwi kadhaa.

Kijana huyu kwa jina la Fazul alikuwa anazungumza lugha ya kiswahili kwa ufasaha kabisa kama mzalamo

Mara nyingi Fazul alikuwa akitoa michango mbalimbali kusaidia jamii inayomzunguka hivyo akatokea kupendwa

Watu hawakujiuliza kwa mwaka mzima ambao Fazul hakuonekana alienda wapi

Fazul alikuwa Mwanza kwa kazi maalumu.

Hata mwaka 1995 ambao alipotea, alienda Kenya kuonana na bosi wake aliyeitwa Wadih Al-hage

Ni katika mwaka huohuo ndio mke wa Fazul akajifungua mtoto waliyempa jina la Afiya.
Fazul akaomba likizo

Akaenda Comoro na mkewe.

Tarehe 22 May 1996, ikiwa ni siku moja tangu kuzama kwa MV Bukoba, na huku Fazul akiwa bado kwenye likizo, akapokea simu kutoka kwa bosi wake Wadih Al-hage

Simu ikamtaka kukatisha likizo haraka na asafiri mpaka jijini Mwanza.

Kule Fazul alitakiwa ahakikishe kama mwenzao aliyekuwa Bukoba, alikuwemo kati ya abiria waliozama na MV Bukoba

Mwenzao huyu aliitwa Ali Amin Al-Rashid aka Abu Ubaidah Al-Banshir

Unaweza usiniamini endapo nitakuambia kuwa huyu alikuwa ni bowi wa pili wa Al-qaeda akitoka Osama

Huyu somo (Al- Amini Al-Rashid) alikuwa ndiye mkuu wa Operesheni zote za Al-qaeda ukanda wa Afrika.

Unaona sasa wameshafika Afrika Mashariki na wameweza kurandaranda kati ya Mwanza na Bukoba.

Kwa hiyo Fazul alitumwa Mwanza kwenda kuhakikisha kama kweli Al-Banshir alizama melini

Awali, Al-qaeda walipopata taarifa za kuzama kwa Mv Bukoba na Al-Banshir akiwa ni abiria, hawakutaka kuamini kama ile ilikuwa ni ajali ya kawaida

Siku zote ulimwengu wa kimafioso huongozwa na machale.

Ilikuwa ni lazima kuhakiki kama kwanza Al-Banshir alikuwa abiria wa meli ile

Baada ya hapo ilikuwa ni kuhakikisha kama kweli Al-Banshir alikuwa mmoja wa abiria, kama kweli ajali ile ilikuwa ni natural au ya kutengeneza.

Kama ajali ingekuwa ni ya kutengeneza ingemaanisha uwepo wao East Africa

Hawa watu walikuwa na mission gani East Afrika?Naam!

Ni nani aliyejua kuwa kulikuwa na maandalizi ya Operesheni mbili?

1. AL AQSA- Dar Es salaam

2.KABAAL- Nairobi

Ilikuwa hivi

Tarehe 23 Feb 1998 Osama Bin Laden alitangaza “Fatwa” akihimiza “Jihad” dhidi ya wamarekani

Video ya “Fatwa” ya Osama ikasambaa kote duniani.

Kwa upande wa Afrika Mashariki “fatwa” ile haikuwafurahisha wakina Fazul na wenzake
Sio kwamba waliipinga

La hasha!

Hawakuipinga lakini haikuwafurahisha sababu muda ambao “fatwa” ilitolewa, ilihatarisha sana kambi yao ya Afrika mashariki hasa Nairobi kwenye makao yake makuuWakina FAZUL walikuwa wanakaribia kilele cha operations zao mbili hivyo walihisi "Fatwa" ile ni kama ingewaamsha CIA usingizini

Baada ya kina FAZUL kuhakikisha upepo wa “Fatwa” ile haukuwa mbaya kwa upande wao, wakarejea mikakati yao.

Ilikuwa ni mikakati mibaya kabisa dhidi ya wamarekani, bila kujali kuwa uwanja wanaopigania na wamarekani, haukuwa mali ya Wamarekani

They didn’t care for collateral damage

1st May 1998 Fazul kwa kupitia dalali Sikanda Juma anapanga jumba kubwa lenye uzio mali ya Tamarra Ratemo maeneo ya Lunda Estates Nairobi

Dar Es salaam, kijana kutoka Pemba kwa jina bandia la Zaharan Nassoro Maulidi anapanga nyumba namba 213 kwenye flats za Ilala Zinanunuliwa gari tatu jijini Dar Es Salaam (Nissan Atlas yenye friji kwa nyuma na Suzuki Samurai rangi nyeupe)

Kenya inanunuliwa gari moja Toyota Dyner

Yule mpemba wa kujiita Zaharan anaanza kujipatia umaarufu kwa kupika chipsi tamu sana pale Ilala.Hakuna aliweza kubashiri kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia

Hakuna aliyua kuwa nyumba ile ilikuwa ikipokea wageni mbalimbali walioingia na kutoka wakitokea Mombasa Kenya

Mmoja wa watu wale alikuwa ni Mohammed Sadiq Odeh

Huyu hakuwa mgeni kwa watu wa Magomeni.

Naam!

Mohamed Sadiq Odeh alijulikana Magomeni kama "Bwana Somba" yaani bwana samaki

Ni kwa sababu Mohamed alimiliki engine boat aliyofanya nayo uvuvi kwenye fukwe za Mombasa na Tanga

SUBSCRIBE HAPO CHINI KUPATA MUENDELEZO WA MAKALA HII NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA ) click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

THE GATE OF HEAVEN AND RISE OF JIWE

Kuelekea mwishoni mwa mwaka 2005, Inafunguliwa chapuchapu kampuni moja.

Tarehe 29 September 2005 kampuni hii inapewa namba 54040 na msajili wa makampuni BRELA

Kampuni hii inaingiziwa pesa kiasi cha Tshs Bilioni 40 kutoka Benki kuu ya Tanzania.

Sie tukiwa tumelala usingizi!

Kampuni hii haikuwa pekee bali na makampuni mengine ambayo nayo yaliingiziwa kiasi kipatacho Tshs bilioni 73

Ikumbukwe ilikuwa imebaki mwezi mmoja tu nchi kuingia kwenye uchaguzi mkuu tarehe 30 October 2005 kabla ya kusogezwa mpaka tarehe 4 Dec 2005

It is worth noting that, Uchaguzi huu ulisogezwa baada ya kifo cha mgombea mweza wa nafasi ya urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA

Katika uchaguzi huo Freeman Mbowe (Gaidi Mteule) alikuwa anagombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania.

Kumbe wakati watu wako busy wakiendelea na kampeni za Uchaguzi, kuna watu account zao zilikuwa zimenona baada ya kuchotewa pesa kutoka Benki kuu kwa kutoka kwenye akaunti ya madeni ya nje EPA (External Payment Arrears)

Lakini infact kiasi kingi kilichokuwa kwenye accont hii hakikuwa kikidaiwa.

Nchi ilikuwa imesamehewa madeni yale baada ya jitihada kubwa za “Mmachinga” kuonyesha nia ya kulipa kwa vitendo (Alitumia awamu yake ya kwanza kukusanya fedha kulipa madeni makubwa aliyoyakuta)

Katika kitabu chake cha “My Life, My purpose” rais Mkapa amenukuliwa akisema kuchotwa kwa pesa zile kulimuumiza hasa baada ya Kushawishiwa na aliyekuwa Gavana wake wa benki Kuu DAUDI BALLALI kuwa riba ya pesa zile ingetumika kusaidia mgombea wao wakati wa uchaguzi mkuu.

Makapuni mengi yaliyolipwa pesa zile hayakuwa yakiidai serikali hata senti, mengi hayakuwa ya nje bali ya ndani na zaidi yalikuwa hewa.

List ilihusisha pia wafanyabiashara wakubwa maarufu.

Lakini unapaswa ujue kuwa hata aliyepitishwa kuwa mgombea wa CCM hakujua mchezo huu

Katika hotuba yake yake ya kwanza wakati anazindua Bunge Mgombea huyo wa CCM aliyeshida urais alinukuliwa akiongea kuwa Uchaguzi Mkuu ulikuwa na matumizi makubwa ya fedha bila kujulikana zilipotoka.

Let us pause at this juncture,

Kuna kitu unapaswa kujiuliza ndugu msomaji

Iliwezekana vipi watu hawa waweze kukwapua pesa huku Mmachinga akiwa bado madarakani, na tena hata mgombea aliyepitishwa asifahamu?

Read my Lips!

Ni kwamba tangu upite mchakato wa kumpata mgombea wa atakayesimamishwa na CCM kwenye uchaguzi mkuu wa 2005, nchi ilikuwa ni kama ipo kwenye Autopilot Mode

Kwenye mchakato ule wa kuteua mgombea wao,Rais Mmachinga alikuwa amepata mapigo mawili.

Hapa namaanisha watu wake wawili muhimu walikuwa wamepoteza nafasi ya kuteuliwa baada ya yeye kushidwa kuwabeba.

Wa kwanza alikuwa ni msaidizi wake ndani ya Chama yaani Makamu Mwenyekiti Bara Mzee Malecela, na pia msaidizi wake mkuu serikalini ndugu Fredirick Sumaye.

Matokeo haya ni kama yalimchanganya mmachinga hivyo katika miezi sita ya mwisho wa uongozi wake ni kama vile wanamtamdao waliomzidi nguvu na kumpitisha mgombea, ndio walikuwa wanaongoza nchi.

Wanamtandao hawa wakawa wanawatishia viongozi wa mashirika ya umma kwamba wasipofata matakwa yao itawacost wakishika nchi.

Obvious, imeshaaminika mpinzani hawezishinda uchaguzi hivyo ukipitishwa kugombea urais kwa Ticket ya CCM ni sawa umeambiwa upige Penalty huku Goalkeeper akiwa amefungwa pingu mikono na miguu.

Sasa viongozi wa mashirika wa umma wakawaogopa wanamtandao ambao walikuwa wanaongozwa na mamvi.

Ili kujihakikishia vyeo vyao kwenye awamu itakayofatia wakawa watii kwa ahadi wanaweza kupewa uwaziri.

Nakumbuka!

Yes! Kuliundwa hadi balaza la mawaziri kabla hata kampeni hazijaanza na wala mgombea hakuwa akijua kama machawa wake wanatumia jina lake kujinufaisha na kupiga pesa.

This was the logic behind of the sour relationship between Handsome and Mamvi kwani ni kama alionekana yeye ndiye ana ushawishi kuliko Namba moja.

Sasa ndio maana unaona rais mteule anatoa hotuba ile bungeni kuwa hajui pesa zilipotoka na pia akaweka wazi urais wake hauna ubia na mtu zaidi ya makamu wake.

Mamvi was supposed to understand this code prematurely.

Hizi pesa zilitokaje?

Ilikuwa hivi

Sometimes April 2006

Wakati akitimiza wajibu wake, Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali LUDOVICK UTOH alibaini miamala ya mashaka iliyofanyika BOT mwaka 2005

Wakati huu alikuwa akiandaa ripoti ya hesabu za 2005/2006

Ni kwamba alibaini Kampuni iitwayo KAGODA Agricultural Ltd iliwasilisha nyaraka za kugushi zaidi ya 12 kwenda BOT

Nyaraka hizi kwa lugha ya kifedha huitwa Notarized Deed Agreement (NDA)

Nyaraka hii hujazwa na mtu wa nje anayeidai Serikali baada ya kuleta huduma au bidhaa Bongo

Sasa kampuni hii ilijifanya kuwa yenyewe ndio mwakilishi wa makampuni 12 ya nje ambayo yalileta huduma au bidhaa hivyo ikawasilisha BOT Notarized Deed Agreements 12 kwa nyakati tofauti na kuchotewa jumla ya Tshs 40

Kama haitoshi,ofisa mwingine wa BOT ndugu iman Mwakosya naye akaandika dokezo lingine kwenda kwa Gavoo kuwa kampuni ya Mibare Farm ilipwe zaidi ya Tshs Milioni 300 na rupia za india zaidi ya milioni 29

Actually afisa huyu alikuwa anfanyanyika kazi nyaraka feki za NDA zilizoonyesha kuwa kampuni ile ina notary Agreement Deed na kampuni ya India Lacksham Textile Mills Ltd iliyokuwa ikiidai serikali ya Tanzania.

Gavoo naye bila hiyana kazi yake ikawa ni kuangusha his signature of endorsement.

Infact ugunduzi huu wa CAG ukatinga bungeni.

Wakati Wabunge wa Upinzani wakiwasha moto Bungeni kutaka kuwajua wamiliki halali wa kampuni ya Kagoda, aliyekuwa waziri wa fedha Zakhia Meghji alinukuliwa akisema kampuni ile ililipwa kufanya kazi za usalama wa taifa.

Hii inamaana wamiliki wake ilikuwa ni dhambi ya kifo kuwafahamu.

Moto wa kashfa hii ulikuwa ukiendelea kuwashwa na kuzimwa hadi mwaka 2007

Huku kukiwa na taarifa katika vijiwe vya kuaminika pale kwa fundi viatu “Samora” nyuma ya IFM kuwa “Gavoo” ameandika barua ya resignation.

Lakini namba moja alishtukia ule mchezo hakuijibu barua yake

SUBSCRIBE HAPO CHINI KUPATA MUENDELEZO WA MAKALA HII NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA ) click here to unlock the post

I am sharing 'POROUS BORDER' with you

Jan 22, 2024 kwenye kikao cha baina ya CDF na makamanda kwa upande mmoja, na Amiri Jeshi mkuu kwa upande mwingine, Mkuu wa majeshi alitoa kauli iliyoibua udadisi

"Kuna wakimbizi wameteuliwa serikalini kwenye nafasi za maamuzi"

Kauli hii ilikuwa ni nzito kutoka kwa mtu mzito.

Nasema mtu mzito kwa kuwa, mtu aliyetoa kauli hii ni mwenye nafasi ya kupata taarifa zote za intelejensia za nchi hii

Kwanza kama mwenyekiti wa kamati ya majeshi ya ulinzi

Pili akiwa kama kiongozi kwenye taasisi yenye chombo kinachofanya "military intelligence" siku zote.

Kwa hiyo CDF Mkunda alikuwa anajua anachokizungumza ni sahii kutoka vyanzo sahii

Undisputed and not farfetched facts

Kauli hii kwa mtu asiyeutumia ubongo wake vizuri, ataisoma tu kwenye magazeti na kuachana nayo bila kuusumbua ubongo kuona yale yasiyoonekana.

Wapo waliohoji ilikuwaje CDF kutoa kauli ile publicly wakati alikuwa na nafasi ya kuonana privately na Amiri Jeshi wake na kumuuma sikio

Katika swali hili, watu wakatoa majibu mawili yafuatayo:-

"SUBSCRIBE HAPO CHINI KUPATA MUENDELEZO WA MAKALA HII NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA ) click here to unlock the post