A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

CODE AND DECODE- USIKU WA MISHEMISHE

Wasaidizi wake walishawekwa bayana juu ya Afya ya “Chief” iliyokuwa ikizorota siku hadi siku.

In fact ripoti ya afya yake walishakuwa nayo kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.

Ikabidi waitane kikao wanandugu.

Kikao hiki kilikuwa kinajadili mirathi because “they saw it coming”

Wanandugu hawakutaka kabisa yule aliyepo kwenye wosia awe mrithi kwani sio mwanaukoo wao.

Vikao hivi viliendelea kwa siri lakini chief alipopata habari hizi alisononeka sana.

Alisononeka kuona hata wale watu wake wa karibu wakijadili mirathi angali yeye bado yuko hai.

Hawa ndio walimuumiza zaidi,

Lakini taarifa za upande wa pili ambao nao walikuwa wanajadili mirathi hazikumuumiza kwani alijua wao ndio walikuwa nyuma ya maradhi yake.

Hapa nisimame kidogo,

Kasheshe ilishaanza tang usiku jamaa alipowaambia wastaafu wanawashwa na kwamba yeye ndiye Chief kwa wakati ule.

Kauli hii kwa mtu mwenye macho matatu ni lazima ajue ujumbe ule alikuwa anaambiwa nani.

Tayari kulikuwa kunatokota baina ya E1 na “Lulu 1”

Kuna siku Diblo dibala alienda kwa kushtukiza pale kwenye “KOJ”. Tangu jioni aliambiwa “meter” iliyokuwa itumike pale haikuwa imefungwa.

Lakini alipoenda kwa kushtukiza akakuta meter imefungwa. Kama mnakumbuka yule dada alipobanwa alieleza kuwa tangu jana yake alishapigiwa simu afunge meter pale.

Hili swala halikuishia pale,

Ilikuja kubainika kuwa kaka mkuu Muombeni Sefu anavujisha mipango ya E1 kwa Lulu 1.

Jambo hili likamgharimu Kaka mkuu, Pamoja na yule aliyekuwa waziri aliyesomea miamba.

Hiki ndio kilikuwa nyuma ya kauli dhidi ya wastaafu na ramani ya vita ikawa imechorwa baina ya wakuu..
(SUBSCRIBE HAPO CHINI KUSOMA MAKALA KAMILI NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA ) click here to unlock the post

SAKATA LA TEGETA ESCROW

Najua wengi wanalijua swala hili kwa juu juu kwa kuwa linazungumziwa kwa lugha ya kipigaji ya kitaalamu kiasi cha kuwatoa kwenye reli wanaotaka kulielewa sakata hili.

Makala yangu itajitahidi sana kuongelea hili sakata kwa lugha nyepesi ili wote tuelewe.

Picha linaanza kwa Kijana mmoja wa kamamo wa Kihaya kuacha kazi benki kuu ya Tanzania

Kijana huyu japo umri umesogea kidogo anajiunga chuo kikuu cha Dar Es salaam kama “mature student)

Kijana huyu analiza chuo kile kwa kuibuka na “First class” ya biashara.

Kijana huyu baadaye anakuwa mmoja wa shareholders kampuni ya kwanza ya mawasiliano Tritel.

Anamiliki shares kupitia kampuni yake ya VIP Engineering and Marketing

Huyu kijana ni mtu mwenye akili nyingi sana,

Ni bingwa wa lobbying na negotiations.

Enzi zile ukiwa na deal yako yako kubwa ya biashara ambayo inahitaji ushawishi basi isingekuwa ajabu kuelekezwa uonane na kijana huyu ili mambo yako yakunyookee.

Kama umeangalia series ya “The Godfather” basi si vibaya ukimuita kijana huyu “le Conciliale”

Baadaye mzee huyu kupitia kampuni yake ya VIPEM (VIP Engineering and Management) akaingia ubia na kampuni ya Malaysia iitwayo MECHMAR.

(SUBSCRIBE HAPO CHINI KUSOMA MAKALA KAMILI NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA ) click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE 

BIASHARA YA NGOZI ZA BINADAMU

Ilianza kwanza tabia ya watu Kupigwa Nondo kichwani na kuuwawa....

Yote hiyo ni kutokana na Imani za kishirikina......

Iliaminika kuwa nondo iliyotumika kumpigia mtu, Ikiwekwa buchani kuning’ininizia nyama....,

Nyama itauzika hadi ushindwe kuwamudu wateja.

Bwana!watu wakauwawa kwa nondo hadi basi,

Hilo likapita,

Ikaja Biashara haramu kabisa,

Biashara ya Kinyama,

Ndio! Ya Kinyama, Kwani ni Bora ingekuwa basi mtu anauwawa,

La Hasha! Kufa utakufa lakini baada ya kupitia mateso Makali kabla roho haijaacha Mwili.

Ni Kweli! Kabla roho haijaacha Mwili, Kwanza unavamiwa na kuchomwa sindano.

 

Baada ya hapo ngozi yako inaanza kuumuka!

Kumbuka, Hapo bado hujafa ndugu,

Kisha ngozi inakatwa maeneo ya shingoni,miguuni na mikononi

Kisha Inavuliwa kama unavuliwa nguo,

Hapo unakukuruka tu,

Makatili hao wala hawajali,

Wao wanaendelea na “Human skin processing” 

Wanaiwekea dawa ngozi yako ili isiharibike

Hapo sasa ndio unaruhusiwa kufa, 

Wanakupiga kichwani kisha wanatupa au kuuzika mzoga wako polini.

Ilifikia hatua ya watu kutotoka majumbani mara ifikapo tu saa 12 jioni,Muda ambao nuru ya jua hufifia hivyo giza kujitangazia utawala,

Ni kipindi ambacho Mkoa wa Mbeya ulikuwa haujamegwa na kupatikana Mkoa wa Songwe.

Kukutana na mtu gizani tena awe amebeba begi kungeleta balaa.

MWAKA 2000

MBOZI,VWAWA

“Nilipigiwa simu na kupewa taarifa kuwa ndugu yangu kaokotwa Kijijini ISANZA. Walimtambua kwa kwa sura lakini mwili mzima ulikuwa mwekundu uliochunwa ngozi” Ulikuwa na jeraha moja tu kisogoni.

MWAKA 2001

MBOZI

“Tulikuwa tumesafiri kikazi kwenda wilayani MBOZI nikiwa na mfanyakazi mwenzangu ambaye alikuwa mrefu sana tena jitu la miraba minne. Kwenye guest tuliyofikia mhudumu mmoja akatufata akasema kuna jamaa wanamwangalia sana mwenzangu. “... Kumbe kulingana na mwili wa jamaa ulivyo, alionekana ni “bidhaa” ya thamani sana kwao. Mhudumu alituambia anahisi wale jamaa ni “Skin agents”. Amini usiamini, tulirudi Mbeya usiku uleule na kazi tukaiacha bila kumaliza”.

Sina kusudio la kuwachosha kwa kuwapa mkasa huu kwa vipande vipande.

No! Nataka mvae uhusika wa hali ilikuwaje,

Sikia tena hii..

(SUBSCRIBE HAPO CHINI ILI KUPATA MUENDELEZO WA MAKALA HII NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA) click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE
Monday, 24th, June 1996

10:30 AM

Central Police post, Dar es salaam

Majira ya saa nne asubuhi, anaingia kituoni hapa mfanyabiashara mwenye asili ya Asia ndugu Walji D Ladwa

Hapa kafika ili kutoa taarifa juu ya kuibiwa kwa gari lake lenye namba za usajili TZG 50

Bwana Ladwa alidai gari lililoibiwa ni Nissan Patrol lenye namba nyeupe.

Polisi katika upelelezi wao wakatajiwa kuwa gari ile imeonekana akiwa nayo jambazi mmoja sugu sana ambaye alikuwa kwenye radar za polisi kwa muda mrefu.

Jambazi huyu si mwingine bali ni Ernest Joseph Sambua Mushi maarufu kwa jina la White.

Taarifa zikadokeza jambazi lile lipo mkoni Kilimanjaro kwa wakati ule.

Yule mfanyabiashara akajulishwa juu ya hili na akatoa gari lake na dereva ili kwenda Kilimanjaro.

Gari namba TZB 7209

Wakachaguliwa makachero wawili kwenda Kilimanjaro

1. Askari namba C. 4246 Detective Sergeant Thomas Mensah

2. Askari namba C. 7874 Detective Corporal Juma Msiwa

Tarehe 29 June 1996 makachero hawa wakawa kwenye gari la bwana Ladwa likiendeshwa na dereva wa Ladwa ndugu Ismail Mohammed Katembo.

Hivyo jumla walikuwa watu garini kuelekea Kilimanjaro.

Lakini kabla ya safari hii,kulikuwa na mkanganyiko kidogo.

Ni kwamba kabla ya safari hii ya kwenda Moshi, polisi walikuwa wameshakamata gari moja kimakosa wakilifananisha na gari lililodaiwa kuibiwa.

Gari namba lenye namba TZD 8592 Nissan Patrol yenye rangi nyeupe pia.

Gari hii ilikuwa ni mali ya Luteni General Imrani Kombe

Lt General Imran Kombe alikuwa ni afisa wa ngazi ya juu sana kwenye jeshi la wananchi aliyejizolea sifa Kemkem kwenye vita ya Kagera.

Akahudumu kama mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa taifa hadi alipostaafu.

Sasa ilikuwa hivi....
(SUBSCRIBE HAPO CHINI KUPATA MUENDELEZO WA MKASA HUU NA MENGINE MINGI KWA MWEZI MZIMA ) click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

MAUAJI MBELE YA FBI

Watu wa kusini wana msemo wa “Mbwanda kala mbwanda” wakimaanisha mbwa kala mbwa. Ndivyo ambavyo ninaweza kuliita tukio hili.

Baada ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda, wengi wa waliohusika kupanga na kutekeleza mauaji yale walikamatwa na kufikishwa kwenye mahakama ya mauji ya Kimbari mkoani Arusha.

Serikali ya Kagame iliyochukua madaraka ilihakikisha hakuna hata mmoja aliyekuwa na mkono wake katika unyama ule anabaki uraiani bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili haki itendeke.

Lengo hili halikutimia kwa 100%

Ni kwa sababu baadhi ya wahusika walikimbilia nchi jirani kama vile Kongo RDC,Kenya na kwingine kokote.

Mmoja ya waliofanikiwa kukimbia alikuwa ni mfanyabiashara mwenye ukwasi mkubwa Felicien Kabuga. Alikuwa ni mtu wa karibu na rais Habyarimana na mabinti wake wawili waliolewa na watoto wa rais Habyalimana.

Bintiye Bernadette Uwamaliya aliolewa na Jean-Pierre Habyarimana. Pia bintiye Francoise Mukazinza aliolewa na Leon Habyarimana.

Bwana Kabuga alikuwa amehusika na kufadhili radio ya RTLM na gazeti la Kangura. Vyombo hivi vilichagiza mauaji ya kimbari kwa kutangaza na kuchapisha hate speeches.

Pia bwana Kabuga alihusika na kuagiza na kuingiza shehena ya mapanga 500 ambayo yalitumika kwenye mauaji ya Kimbari.

Baada ya serikali ya Kagame kuingia madarakani, Kabuga alikimbilia nchini Uswisi ambako mamlaka zilimzuia kuingia na wakamdeport kwenda Zaire. Baadaye Kabuga akaingia Kenya.

Akabadili kabisa jina lake na kujiita Idris Sudi. Ukaribu wake na aliyekuwa rais wa Kenya Daniel Arap Moi uliweza kumsaidia kuishi Kenya kwa uficho bila usumbufu.

Akiwa Kenya aliweza Kusajili kampuni ya NSHIKABEM na kuendelea kufanya biashara kwa mafanikio kwa kutumia majina ya wanasiasa wakubwa na viongozi wa umma.

Alikuwa hatoi pua yake sehemu yoyote hata kwenye matukio makubwa yaliyohusu familia yake. Binti yake alipoolewa mwaka 1995 mwaka mmoja tu baada ya mauaji ya Kimbari, aliyesimamia shughuri yote alikuwa ni Kenneth Matiba aliyekuwa mwanasiasa wa upinzani Kenya na mfanyabiashara mkubwa.

Mwaka 1997 polisi walinusa uwepo wa Kabuga nchini Kenya lakini walipoenda kuvamia kwa ajili ya kumkamata hawakumkuta bali walikutaujumbe kutoka kwa askari mwenzao ukimtaadhalisha juu ya mpango wa kumkamata.

Kuna wakati Wapelelezi wa kesi za kimbari waliweza kumfatilia na kumuona kabuga kwenye nyumba inayomilikiwa na Hosea Kiplagat aliyekuwa ni binamu wa rais Moi.

Hosea Kiplagat

Pembeni tu ya nyumba ile, kulikuwa na nyumba nyingine mali ya mtoto wa Moi aitwaye Gideon.

Gideon Moi

Hapa unaweza mwenyewe kujiongeza kujua ni nani aliyekuwa akimlinda Mr. Kabuga ambaye alikuwa akitafutwa kwa dau la dola million tano za kimarekani.

Wakati Kabuga akiendelea kufurahia safe heaven in Kenya, kuna kijana mdogo alikuwa akichipukia ili aje kuwa mtu wa karibu na Kabuga.

Kijana huyu ambaye aliwashangaza watu kwa uwezo wake wa kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha, mwaka 1997 alijikuta anaajiliwa kwenye Nairobi Star alipomaliza tu elimu yake ya kidato cha nne bila kusomea kozi ya uandishi.

Gazeti lile lilikufa mwaka 1998 baada ya kifo cha mbunge wa Kieni aliyeitwa Munene Kairu.

Kijana yule akawa anaandika makala zake kwenye magazeti ya Nation na People daily

Makala yake moja ilihusu uharibifu wa mazingira kwa kukata miti katika eneo la Maliashoni kwenye msitu wa Mau. Makala hii iliwavutia sana wanasiasa wa jimbo la Rift Valley.

Kati ya waliovutiwa alikuwemo Zakayo Cheruiyot ambaye alishakuwa katibu mkuu wa wizara ya usalama wa ndani Kenya na mbunge wa Kuresoi kusini kwa awamu mbili. Huyu alikuwa ni mshauri wa karibu wa rais Moi.

Zakayo Cheruiyot

Ukazaliwa urafiki wa yamini baina ya Kijana huyu na Mr. Zakayo Cheruiyot.

Katika urafiki wao, Mr. Zakayo kwa kumuamini sana Kijana huyo, alianza kumshirikisha kwenye biashara.

Ndani ya biashara kijana yule akafanikiwa kuonana na Felicien Kabuga. Aliyewakutanisha ni Zakayo.

Walikuwa wanakutana mara kwa mara sehemu mbalimbali na Kabuga lakini kijana yule hakushirikishwa yalipo makazi ya Kabuga.

Biashara baina yao ikaendelea ingawa kijana huyu hakuacha kazi yake ya kuandika makala kwenye magazeti. Pia alikuwa na mahusiano ya karibu na maafisa wa ubalozi wa Marekan Kenya.

Baada ya Serikali ya Moi kutoka madarakani, Mambo yalianza kwenda mrama kwa upande wa Kabuga.

Mwezi mmoja tu baada ya rais Mwai Kibaki kuchukua madaraka, aliyekuwa balozi wa marekani nchini Kenya akamshutumu Zakayo aliyekuwa ni mkuu wa usalama wa ndani wakati huo kwa kumficha Kabuga.

Mr. Zakayo akatolewa kwenye nafasi yake na kuhojiwa na polisi ambapo alikama kumficha Kabuga.

Baadae Zakayo na yule kijana walihitilafiana na haikujulikana sababu ya hali ile.

Muda wote Zakayo alihisi huyu dogo anaweza akauza mechi na akawa anachunguza nyendo zake kwa siri.

Dogo naye akavutiwa na dau la dola millioni tano. Akajua ule ndio wakati wa kuaga umasikini.

Laiti angejua, angeachana na wazo lile….

Dogo akaenda ubalozi wa Marekani chini kenya na kuelezea ajuayo. Maafisa ubalozi wakapeleka taarifa zile Federal Bureau of Investigation FBI.

Maafisa wa FBI wakawasiliana na dogo ili kujiridhisha. Dogo akawathibitishia kabisa kuwa ameshaonana na Kabuga mara kadhaa na ni mshirika wake wa biashara.

Ikaandaliwa operation ya kumkamata Kabuga…

Haraka ikatumwa timu ya makachero wa FBI nchini Kenya.

Dogo akaambiwa “amvute” Kabuga nyumbani kwake ili wajadili jambo linalohusiana na biashara zao “business meeting”

FBI wakawashirikisha idara ya upelelezi Kenya ili wawaongeze nguvu katika zoezi lao.

Lakini hawakuwatajia ni nani anatakiwa kukamatwa na wala hawakumtaja informer wao.

Zoezi llifanyika mapema asubuhi tarehe 15 January 2003 ambapo makachero wa Kenya na Marekani waliizingira nyumba aliyokuwa akiishi kijana yule mtaa wa Karen jijini Nairobi. Ilikuwa si rahisi mtu asiyehusika kujua kama nyumba ile imezingirwa.

Kwenye nyumba ile ndipo walipotarajia kuwa Felicien Kabuga angefika baada ya kupewa wito na kijana yule.

Kijana yule aliyefahamika kwa jina la William Munuhe Gichuki alikuwa ndani ya nyumba ile simu yake akimsubiri Kabuga.

Yalipita masaa sita bila Kabuga kutokea na hata makachero wale walipojaribu kumpigia simu William hakupokea.

Ili kutoharibu zoezi, maafisa wale wakaondoka kimya kimya majira ya saa 7 mchana bila kuingia ndani ya nyumba ile.

Kesho yake Willium alipopigiwa tena simu haikupokelewa.

Siku ya tatu polisi wakaamua kwenda kugonga kwenye ile nyumba lakini hawakujibiwa.

Wakaamua kuvunja mlango na kuingia.

Wakakutana na maiti ya Willium juu ya kitanda chake aliyeonekana amefariki siku mbili nyuma kwa makadilio.

Maiti ya William

Pembeni ya kitanda kulikuwa na jiko la mkaa ambalo waliotekeleza mauaji yale walitaka kuwaadaa watu kuwa alikufa kwa gesi ya Carbon monoxide kutoka kwenye mkaa ule.

Kiuhalisia mwili wa william ulikuwa umepigwa risasi iliyoingilia kwenye sikio la kushoto.

Na risasi ile alipigwa siku ile ike ambayo makachero walikuwa wameizingira nyumba yake na kusubiri kwa masaa sita bila ya waliyemtega kutokea.

Makachero waliamua kuondoka siku ile bila kujua tayari William alishageuzwa maiti na wabaya wake.
(SUBSCRIBE HAPO CHINI KWA MUENDELEZO WA MAKALA HII NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA) click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

DEREVA KIRIKUU

 Mshamu ni dereva wa kirikuu chenye namba ya usajili T 902 CHR Kirikuu hiki ni mali ya mzee mmoja wa kichaga maarufu kwa jina la Mzee Urassa Mshamu alikuwa akipaki kirikuu hiki kwenye kijiwe cha Manzese mahakama ya ndizi kuvizia wateja. Mambo yalikuwa sawa mpaka siku moja…

 Tarehe 15 December mwaka 2013 majira ya saa 12 jioni, watu wawili walifika pale kijiweni kwa Mshamu Watu hawa wakamwambia Mshamu wanahitaji wakodi gari lake ili awabebee mzigo wa mbao kuupeleka Mbagara Kongowe Mshamu akawatajia bei na wakapatana kiroho safi Baridi barafu! 

Wakaenda kwenye mzigo, wakapakia na safari ya Kongowe ikaanza. Mshamu alika mbele na mmoja wa waliokodi gari, huku mwenzake akiwafata nyuma kwa pikipiki Mshamu alikuwa amemchukua rafiki yake aitwaye Selemani awasindikize (Alikaa nyuma kwenye mzigo)

 Giza lilishaanza kuingia Walipofika Mbagara Kizuiani abiria aliyekaa na Mshamu mbele ya gari, akamtaka ampakie mtu mmoja ambaye alisema ni fundi ujenzi Mtu yule akapanda nyuma na mfuko wa kiroba, safari ikaendelea Walipofika Kongowe, Mshamu akatakiwa tena asimame ili wawapakie watu wengine.

 Mshamu akauliza hao watu ni kina nani? Akajibiwa ni watakaoshusha mzigo kwani waendako ni mbali na barabara hivyo watakosa usaidizi. Mshamu akakataa! Akasema watu waliopo garini wanatosha kabisa kushusha mzigo ule. 

Safari ikaendelea wakiwa wameshaanza kushika rough road Baada ya kutembea kwa mwendo fulani, Mshamu akashangaa wanaingia kwenye mapori ya kutisha. Mshamu akasimamisha gari! Akasema hawezi kuendelea hata hatua moja zaidi ya pale walipofika. Ilishahitimu saa 3 na nusu usiku. Mshamu akawa anashuka kutoka kwenye gari… 

Ghafla yule aliyekuwa anawafata kwa pikipiki akaenda mbele na kublock kirikuu. Muda huohuo Mshamu akashangaa anapigwa na ubapa wa panga. Akaamriwa akae chini, Yeye na rafiki yake (Selemani) wakafungwa kamba mikononi na miguuni Jamaa wa pikipiki katoa wazo wawaue Wazo hili likapingwa na yule aliyekuwa amekaa mbele na Mshamu Wakawapeleka mbali na kuwatelekeza maporini. 

Mungu mkubwa! Mshamu alifanikiwa kujifungua kamba kwa meno. Akamfungua pia Selemani Wakatembea kurudi barabarani Kule waliwakuta madereva bodaboda ambao waliwaeleza yaliyowasibu Madereva wakaanza kufatilia alama za matairi gari ile ilipopita (ilipita rough road) Safari yao ikawafikisha mpaka mtaa wa Rufu ulioko Mbande Wakaona kirikuu kilichopakiwa kwenye goli moja la uwanja wa mpira Waliposogelea gari ile, wakatoka watu nyuma ya gari na kukimbia Madereva boda wakawakimbiza wakiwaacha nyuma Mshamu na Sele Ni wakati huu ndipo wakaona mtu mwingine akishuka kutoka kwenye kirikuu chao upande wa ndereva. 

Wakapiga yowe la Mwizi Yule jamaa akawa anakimbia Hakwenda mbali akakutana na mpiga kura aliyetoka kuitikia yowe Yaani “uswazi” kuna watu wanakaa “sailensa” tu kusubiri kiumane Basi mpiga kura huyu akampiga fimbo mbili kichwani yule jamaa aliyeshuka kwenye gari na kukimbia Fimbo kama za Ndugai alizowahi kumpiga mtu Kongwa Jamaa akalala chini. Mshamu akamtambua mtu yule ndiye aliyemkodi na kukaa naye siti ya mbele.

 Wapiga kura wakaongezeka Wao hawakutaka kusikia lolote With their cult belief in violence Wakaanza kumpopoa mawe Pale akafika balozi wa mtaa na kuwataka rai the “furios mob” waache kujichukulia sheria mkononi. 

Lakini wananchi wakaendelea kumpiga mtu yule ambaye kumbe walikuwa wakimfahamu kwa jina la Juma White Juma White akaendelea kupigwa huku akiambiwa amtaje mshirika wake.

 Akawatajia jina la Shandrack Meshack Balozi akashtuka sana kusikia jina lile kwani alikuwa akimfahamu Shadrack. Alifahamu pia kuwa Shadrack alikuwa jirani na nyumba ambapo gari ile ilikutwa imepakiwa. 

Swali likawa Shabani yuko wapi? Hadi muda huu balozi alishakuwa amepiga simu polisi kuwataka wafike eneo la tukio. Lakini hadi polisi anafika, wananchi wenye gadhabu ambazo zilishindwa kuthibitiwa, walikuwa wameshamchoma moto Juma White.

 Mshamu, Selemani, balozi na polisi wakaongozana kwenda kituo cha polisi Mbagala wakitumia kirikuu kile kile. Lakini wakati watu hawa wapo kituoni kule nyuma kuna mpiga kula mmoja aitwaye John Anthony naye alikuwa ameamshwa usingizini baada ya kusikia yowe la mwizi. John akaamka, akamfungulia mbwa wake na akawa ameshikilia kwa kamba mkononi.

 John akajibanza kwenye moja ya vichochoro karibu na nyumbani kwake karibu na barabara ya Songas. Haikupita muda mrefu, akamuona kijana aliyekuwa akitweta huku akiwa na wasiwasi akija usawa na alipo pale kichochoroni. Akamsimamisha na kumuuliza anatoka wapi na anaenda wapi? Kijana akajibu anaelekea Chamanzi na kuwa ameporwa pikipiki yake maeneo ya Mzinga Mbagara.

SUBSCRIBE HAPO CHINI KUPATA MUENDELEZO WA MAKALA HII NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

KARATA TATU

Ukitembelea Kariakoo katika makutano ya mtaa wa Mchikichi na Mtaa wa Kongo, Utaona Jengo la ghorofa 8 

Kabla Ghorofa halijajengwa Kwenye kiwanja kile kulikuwa na nyumba moja ya udongo Iliyokuwa Ikimilikiwa na mzee BUSHIRI PAZI na mkewe NEEMA BUSHIRI PAZI

Mzee huyu ambaye ni marehemu alimiliki nyumba ile kupitia barua ya “offer” kutoka Ardhi ya tarehe 4 January 1990

Alipofariki nyumba ile ikarithiwa na mkewe NEEMA

Neema naye alipofariki, Kwa mujibu sheria ya Kiislamu nyumba ile wakarithishwa watoto sita wa marehemu.

HAMISI BUSHIRI PAZI akiwa ni mtoto pekee wa kiume akatambulika kama ndiye msimamizi mkuu wa nyumba ile kwa niaba ya dada zake.

Hamisi akawagawia kila mmoja wa dada zake chumba ndani ya nyumba ile.

Hapa naongelea mambo ya mwaka 1998 Sheikh

Hapa maeneo ya Kariakoo yakiwa tayari ni maeneo yaliyochangamka kibiashara.

Mwaka huo wa 1998 anatokea kijana mmoja wa mwenye asili ya mkoa wa Kigoma ambaye nyumba ile inamvutia kuanzisha biashara yake.

Anaenda kuongea na mmoja wa wanafamilia ile mdada aitwaye TATU BUSHIRI

Anamwambia TATU kuwa ana “Interest” ya kupata eneo kwenye nyumba ile ili afungue biashara yake.

Kwa kuwa TATU alikuwa akimiliki chumba kimoja kwenye nyumba ile ya udongo, anashawishika kumpangisha kijana yule kwenye chumba chake kwani anetajiwa dau nono.

Kipindi kile hasa kwa kuzingatia nyumba yenyewe ni ya udongo, mtu akikutajia dau la kukulipa laki sita kwa mwaka halikuwa dau dogo.

Tatu akakubali kumpangisha kijana yule Chumba chake kwa malipo ya Tshs Milioni 1.8 kwa miaka mitatu.

Kijana yuke aendaye kwa jina la MUSA KAZUBA akalipa pesa ile kwa cash na ukaandikwa mkataba wa kupangisha pango.

Mungu si Athumani,

Kwa kuwa Kariakoo ilizidi kukua kwa kasi, akatokea mtu mwingine aliyekuwa na “interest” na eneo lile.

Mtu huyu aitwaye ABDALAH JUMA ALLY aliongea na wanafamilia na kuwapa deal iliyowavutia.

Aliwaambia anataka kuiendeleza nyumba ile na ajenge nyumba ya tofali za “Block” tofauti na ile ya udongo iliyopo

Lakini kwa msharti

Kwa masharti kuwa akimaliza kujenga atakuwa anakusanya kodi kwa muda wa miaka saba akilipa milioni 14 kwa mwaka.

Na muda ukiisha atawaachia jengo zuri la kisasa ambalo atakuwa ameliendeza familia ile.

Hili lilikuwa ni deal zuri la kuvutia hivyo halikukataliwa.

MUSA KAZUBA akaambiwa apishe ujenzi, na jengo likikamilika arudi kwenye eneo lake alilokuwa amepangisha.

MUSA naye akakubali kwani alijua jengo likiendelezwa atanufaika pia kwa kuwa na sehemu nzuri ya biashara yake.

Zilongwa mbali, Zitendwa mbali

Kwa nini?

Ni kwamba baada ya jengo kuisha, sehemu ambapo kilikuwepo chumba alichokuwa amepanga Musa, Kilikuwa kimegeuka njia badala ya Chumba.

Musa akakabidhiwa chumba kingine ambacho hakikumvutia kibiashara.

It was likely  mkataba wa upangaji ulikiukwa.

Haya yote yalitokea kwa sababu kulikuwa na a very calculated Move kabla Musa hajaenda kupanga na hadi anakuja mwekezaji wa jengo.

Usicheze na Kariakoo Chief

Ni kwamba Musa akaenda kufungua kesi mahakama ya wilaya ambayo ilihamishiwa Baraza la nyumba la Mkoa

Katika baraza la Nyumba musa akafungua shauri namba 112 B la mwaka 1999

Maamuzi yakatoka kuwa aliyempangisha Musa (TATU BUSHIRI) amlipe jumla ya Tshs Milioni 15

Yaani kwanza amlipe Musa pesa ya kodi aliyopokea (mil 1.8) pamoja na riba yake (kwa rate ya mahakama)

Kisha alipe Tshs laki 9 kila mwezi tangu siku shauri lilipoamuriwa (May 1999) mpaka itakapotimia pesa yote milioni 15

Pia ampe musa Chumba kingine kwa miaka mitatu.

TATU akashindwa kumlipa Musa kwa mujibu wa hukumu

Badala yake akakatia rufaa uamuzi ule.

Kwenye baraza la rufaa la Ardhi na makazi akaangua pua

Mahakama kuu akaangikia pua

Mahakama ya rufaa akaangukia pua

Wakati huo Musa kwa upande mwingine akiendelea kutafuta kukazia hukumu

Yes!

Mwaka 2000 Musa akatinga mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kuomba kukazia hukumu kwenye kesi namba 71 ya mwaka 2000

Tarehe 24 July 2001 mahakama akamruhusu Musa kuuza jengo kufidia deni.

wanafamilia ambao hawakuwa sehemu ya mgogogo kati ya Tatu na Kazuba, ambao nao walikuwa wamiliki, waliibuka na kudai hawakuwa wakijua kilichokuwa kinaendelea mahakamani.

Walikwenda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutambua uwepo wa mgogoro huo na kuweka mapingamizi kadhaa wakipigania haki yao.

Mnada kabla ya hukumu

Wakati mapingamizi hayo yako mahakamani, madalali wa mahakama walianza kutangaza kupiga mnada nyumba hiyo siku kadhaa kabla hata
(SUBSCRIBE HAPO CHINI ILI KUPATA MUENDELEZO WA MKASA HUU NAMENGINE MINGI KWA MWEZI MZIMA) click here to unlock the post

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE 

UNSOLVED MURDERS

My dear readers, 

It has been a while since my last post. 

Ukimya wangu ulisababishwa na safari yangu nchi ya jirani ya Kenya kuitikia wito wa mteja wangu aliyetaka kufanyiwa Environmental Impact Assessment kwenye mradi wake anaouanzisha.

Nikiwa huko nilikuwa nawamiss sana. Nilikuwa nawaza jinsi ambavyo mngenishambulia kwa ukimya wangu. Kwa hofu kuu nikadisable chat group
Ninaomba sana mniwie radhi kwa hili.

Yote kwa yote sikuacha kudodosa habari mbili tatu. Mmoja wa wenyeji wangu aliniambia kuwa amefatilia makala zangu mbili tatu ambazo niliongelea maswala ya nchini kwao na akavutiwa sana nami. Tukapiga stories nyingi sana ambazo bila kujua ndio zimezaa tena andiko hili.

Kama ilivyo Tanzania, nchi ya kenya pia imejaa vitimbi vya kuwa na kesi za mauaji ambazo upelelezi wake haujawahi kuhitimishwa. Kwa mfano mpaka leo haijulikani nini hasa kilikuwa nyuma ya kifo cha Kolimba masaa machache tu baada ya kusema CCM imekosa dira na mwekeleo. Mpaka leo hatujui kwa undani juu ya kifo cha ghafla cha makamu wa rais Dr. Omary Ally Juma masaa machache baada ya kutoka kwenye maonyesho ya saba saba. Pia hatujui ilikuwaje aliyekuwa mkuu wetu wa usalama wa taifa Luteni Jenerali Imran Kombe aliuwawa vipi na polisi waliodai walimfananisha na mwizi wa gari wakati maaskari wakina Matiku walikuwa wanamfatilia tangu alipotoka Dar es salaam mpaka kijijini kwake Moshi. Askari hawa waliatolewa jela baadae kwa msamaha wa rais. 

Unsolved murder cases ni nyingi kwa kwetu tanzania ikiwepo kupotea kwa watu kama Azory Gwanda na Ben Saanane. Makala ya leo itajikita zaidi kwenye mikasa ya vifo nchini Kenya ambayo mpaka leo hii haijapatiwa ufumbuzi.

Mwaka 2017 ikiwa zimebaki siku chache tu kabla ya Uchaguzi mkuu wa Kenya (August 8 2017) mwili wa Chriss Msando uliokotwa katika msitu wa Muguga kaunti ya Kiambu baada ya kutoweka tangu tarehe 2 August 2017.

Chriss Msando alikuwa ni mkuu wa kitengo cha teknohama katika tume ya uchaguzi wa Kenya IEBC ambaye alikuwa akihusika moja kwa moja kuhakikisha hakuna wizi wa kura katika uchaguzi ule.

Msando alionekana kwa mara mwisho jioni ya jumatano katika kituo cha runinga cha KTN na aliongea yafuatayo kuhusu mfumo wa upigaji kura;

“We are well prepared and it is all systems go. No rigging, no hacking and no manipulations of votes this time,”. “Everything is set in a way that only one person have the password that controls the entire  streaming of results.”

Akimaanisha

“Tumejiandaa vizuri kimfumo. Hakutakuwa na wizi wa kura wala uwezekano wa mfumo kudukuliwa. Ni mtu mmoja tu mwenye password ndio atakuwa anaratibu mfumo mzima wa utoaji matoke.”

Je, Inamaanisha kauli hii ndiyo iliyomponza kwa kuwa ni yeye pekee ndiye aliyekuwa na password ya mfumo? Mimi na wewe hatujui.

Kinachojulikana ni kwamba Mwili wa Msando uliokotwa ukiwa hauna nguo huku pembeni yake kukiwa pia na maiti ya binti wa miaka 21 Maryanne Carol Ngumbu ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa udaktari. Msando na Maryanne walionekana wakinywa pamoja kabla ya kutoweka kwao.

CCTV footage zilionyesha bwana Msando akiwa na Mwanamke mwingine tofauti na ambaye alikutwa akiwa ameuwawa pembeni yake. Mwanamke huyu hakuongelewa sehemu yoyote katika uchunguzi wa polisi na hata haijulikani kama aliwahi kuhojiwa.

Kwa mujibu wa postmortem report, ilithibitishwa kwamba Msando alipitia mateso makali kabla ya kifo chake kwani mwili wake ulikutwa na majeraha mengi.

Siku mbili tu baada ya mkasa huu, tarehe 4 august 2017, ikavuja taarifa kuwa Polisi nchini Uganda wamekamata watu watatu wanaoaminika kuwa walihusika na kifo cha Msando.

Watu hao waliingia Uganda wakitumia gari nyeusi aina ya Toyota Fortuner ikiwa na namba za Uganda lakini waliposachiwa walikutwa na plate number nyingine ya nchini Kenya ambapo mmiliki wa namba ile alikuwa ni mwanasiasa mkubwa. Ili kulinda mahusiano ya nchi mbili mwanasiasa huyo hakuwahi kutajwa jina lake popote.

Watu wale waliingia kenya kupitia mpaka wa Malaba na nia yao ilikuwa ni kwenda Juba sudani. 

Mathew Butia raia wa Kenya, Joseph Okongo na Moses Goloba raia wa Unganda ndio waliokamatwa ndani ya gari ile.

Pamoja na kuwa na taarifa zote hizi mpaka leo hakuna yeyote aliyefikishwa mahakamani mpaka leo. Naamini upelezi wa kesi hii unanawaongoza wapelelezi kwa watu wasiogusika na hivyo kuishia njiani.

Kama kifo cha Msando hakijakusikitisha, basi kifo cha Jacob Juma  kitakusisimua.

Huyu Jacob Juma alikuwa ni Mfanyabiashara mkubwa aliyekuwa akifanya tenda mbalimbali za serikali. Akiwa na miaka 44 tu, tayari alishakuwa mtu mwenye ukwasi mkubwa. Kuna wakati Jacob Juma aliifungulia serikali kesi za madai na alikuwa akishinda na kulipwa fidia kubwa kubwa.

Pia Jacob Juma alikuwa anapenda sana kupeleka vita zake kwenye mitandao ya kijamii either akigombana na serikali au mahasimu wake wa kibiashara.

Siku chache kabla ya mauti yake, Jacob Juma alikuwa amekata rufaa dhidi ya Serikali kwa kumfutia leseni yake ya uchimbaji wa madini na alikuwa akidai fidia ya Kshs trillion 2.

Usiku huo alionekana na CCTV camera za mabarabarani akiendesha gari lake Mercedes benz katika barabara za Westland na Lavington jijini nairobi na alionekana akimpakia mwanamke kutoka kwenye moja ya apartments zake.

Baadae usiku wa saa 3 alionekana kwenye CCTV akitokea kwenye moja ya bar na kuendesha kuelekea nyumbani kwake. 

Sasa akawa amefika kwenye barabara ya Ngong ambayo haikuwa na CCTV. 

Lilikuwa kosa kubwa!

Wakatokea watu watano na kuanza kumiminia jumla ya risasi 10 gari yake na kutokomea kwa pikipiki kusikojulikana bila kuchukua chochote.

Risasi mbili zilizomwingia kifuani zilitosha kabisa kukatiza maisha yake palepale.

Mke wa Msando akiwa hajui lolote alijaribu kumpigia simu mumewe usiku ule bila mafanikio mpaka alipopewa taarifa kesho yake.

Polisi walifika haraka sehemu ya tukio na kulivuta gari lake huku maiti yake ikiwa bado kwenye gari. Hii inasemwa ilichangia kwa kiasi kikubwa kuharibu crime scene.

Mpaka leo wauaji wa Juma Jacob hawajafahamika.

MESHACK YEBEI

Huyu alikuwa ni shaidi aliyekuwa anatakiwa kwenda kutoa ushaidi kwenye mahakama ya kimataifa ICC dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto baada ya vurugu za uchaguzi.

Jumapili asubuhi ya December 28 2014 mke wa Yebei ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi nane alimuandaa kijana wao aitwaye Shammah ili aongozane naye kwenda clinic na pia kijana huyo akatibiwe tonsils.

Mmewe Meshack Yebei akaona naye si vibaya akiambatana nao hospitali.

Walifika Turbo Health centre wakawa kwenye foleni ya kusubiri matibabu ambapo kijana wao Shammah aliyekuwa na umri wa miaka mitatu aliomba apatiwe maji ya kunywa.

Meshack akamwacha mke wake kwenye benchi na kijana wao na yeye akatoka haraka kwenda kwenye duka la madawa jirani na pale ili kumfatia maji kijana wao. 

Ule ndio ulikuwa mwisho wa Meshack kuonekana tena.

Huku nyuma mkewe na mwanae wakatibiwa na hadi wanarudi nyumbani mmewe hakurudi kabisa siku ile.

Namnukuu kaka wa Meshack aitwaye Kennedy Yebei

“Tuliingiwa na wasiwasi Meshack aliposhindwa kurudi jioni lakini kuna wakati tulivumilia tukijua labda kapatwa na dharula na atarudi”.

Siku iliyofuata asubuhi majira ya saa nne na nusu,mama yake akapokea ujumbe mfupi kutoka namba +256733125351 ambapo mtumaji alitaka ionekane ni mwanae ndiye katuma ujumbe ule.

Ujumbe ule ulioandikwa kwa lugha ya Kalenjin ulisomeka hivi

“Abwati ale ichamegei, kwawe Uganda urgently. Kimia k ng’amotik chebo Bensouda chekile Partrick ak Lugusa. Ami komye, mosich wasiwasi. Meshack, ako namba nenyu ni”.

Ukimaanisha;

(SUBSCRIBE HAPO CHINI ILI KUPATA MUENDELEZO WA MAKALA HII NA NYINGINE NYINGI KWA MWEZI MZIMA) click here to unlock the post