Buyobe
Buyobe @Buyobe

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

MONEY HEIST/Ujambazi Ubungo

Mwishoni Mwa mwaka 2004 kabla hajaingia madarakani, mwanzoni Mwaka 2005 akiwa Madarakani na hata miaka iliyofatia katika utawala wake, Rais Kikwete alipata Changamoto kubwa sana ya ujambazi kwenye mabenki.

Mwaka 2004 May 21 majambazi yalivamia NBC Moshi na kupora 5.3 billions.

September 20,Mwaka 2005, duka la kubadilisha pesa la Mc Sons lilivamiwa jijini Dar na majambazi walikwapua Tshs Milioni 150 na kuondoka bila wahusika kubainika.

March 30,2006 benki ya Standard charted Dar ilivamiwa zikakombwa Tshs Milioni 300.

Huu mchezo sasa ukazoeleka!

Mwaka ule ule wa 2006(mwezi mmoja tu uliofuata) tarehe 20 April likapigwa tukio Kabambe pale lilipokuwa eneo maarufu kama Ubungo mataa (Sasa Kijazi interchange)

Naam,

Ilikuwa ni saa 6 na dk 30 mchana watu wa dar walishuhudia movie la kivita katika uhalisia.

Ilikuwa hivi,

Watu hawakutilia maanani mijibaba iliyoshiba ilipoingiza gari lao aina ya Toyota collola yenye namba T533 AAB kwenye kituo cha mafuta cha TUICO(sasa hivi Oil Com)

Pia hawakujali gari aina ya Pickup Hard body ilipokuja na kupaki nyuma ya ile gari ya kwanza.

Pengine walihisi ni maaskari kanzu ambao huvaa kiraia na kutumia magari yenye namba za kiraia.

Hawakujua,

Watu wale walikuwa na “mchoro” wao pale.

They were all there for a specific damn show.

Walikuwa na taarifa sahii kwa wakati sahii.

Katika upande mwingine Gari mbili aina ya Land Cruiser “mkonga” zilikuwa zikifuatana kwa ukaribu toka Bank ya NMB(Bank house) na sasa zilikuwa zimefika barabarani ya Sam Nujoma.

Gari ya mbele ambayo yenye namba za usajili SU 34390 ilikuwa ikiendeshwa na bwana ALY OMARY LUMBI LUMBI huku pembeni yake katika kiti cha abiria akiwa kakaa karani wa NMB tawi la Wami bwana ERNEST MANYONI.

Katika siti za nyuma za gari ile ile walikaa askari wawili
1. D. 6866 Police Constable ABDALAH MARWA

2. Corporal ADIMU KILOWOKO

Askari hawa walikaa pamoja na masanduku ya pesa ambazo kwa ujumla wake ilikuwa ni Tshs Bilioni Moja.

Pesa hizi zilikuwa zinapelekwa NMB Wami Morogoro

Gari la nyuma yake lenye usajili SU 36177 liliendeshwa na Juma Nyundo.

Pia walikuwemo askari wawili

1. C 2199 Sgt. TAJI WALES MMUMI

2.E. 9784 CPL VENANCE MALINGO

Gari hii ilikuwa imemeba vifaa vya ofisi(Stationaries)

Kila askari katika gari zote alikuwa na SMG na risasi 30.

Sasa gari hizi zikawa zimefika ubungo mataa zikisubiri taa za kuongoza magari ziwaruhusu kushika barabara ya Morogoro ili waendelee na safari yao kwenda tawi la NMB Wami.

Mwezi ukaandama,

Hapa namaanisha taa sasa zikawaruhusu

Gari ya mbele ikawa inakunja uelekeo wa Mbezi.

Hawakujua Masikini!

Ile collola na Hard Body zikachomoka ghafla kutoka kwenye magesho yao pale Kituo cha mafuta.

Watu wakabaki wamepigwa na bumbuwazi jinsi gari zile zilivyochomoka.

Wakiwa bado kwenye mshangao wakaona gari ya mbele ya NMB inamiminiwa mvua ya risasi.

Ile gari ya nyuma ya NMB baada ya kuona dhahama ile ikataka kunyosha kama inaenda Buguruni na sio Wami tena.

It was a fatal mistake!
Endelea kusoma hapo chini >>>>>> click here to unlock the post

Buyobe
Buyobe @Buyobe

_>>>>>>>>>>. *NDANI YA CHUMBA CHA KUNYONGEA.*_<<<<<<<<<<<<

Adhabu ya kunyongwa hadi kufa, ni mojawapo ya adhabu kongwe na ya kuogofya zaidi duniani... Na ndio adhabu ya juu zaidi.... Kunyongwa hadi ufe kabisa baada ya kuthibitishwa na mahakama tuhuma zako
Kuna taratibu ngumu na za muda mrefu hadi mtuhumiwa afikie kunyongwa kwakuwa kuhukumiwa kunyongwa ni jambo la kwanza lakini kutimizwa kwa adhabu ni jambo lingine... Unaweza ukahukumiwa kunyongwa na usinyongwe, ni mpaka mkuu wa nchi asaini hati yako ya kifo ndio unaweza kunyongwa!.

Kabrasha la chumba cha kunyongea ni kubwa hivyo tuangalie dondoo zake wiki ya mwisho ya kutekeleza adhabu hasa masaa 72 ya mwisho...!!!! Maandalizi huwa mengi lakini haya ndio muhimu zaidi....
Endelea hapo chini >>>> click here to unlock the post

Buyobe
Buyobe @Buyobe

>>>>>>>>>>>>. MAUAJI KISIMANI <<<<<<<<<<<<<<<<

PETER TYENYI(53) alikuwa ni mtumishi wa idara ya Usalama wa Taifa. Maisha yake katika siku zake za mwisho wenye utata ziliwashangaza wengi hasa majirani ambao ni watumishi wenzake aliokuwa akifanya nao kazi Pale KIJITONYAMA.

Alitumbukia kwenye ulevi uliopitiliza katika bar mbalimbali maeneo ya KIJITONYAMA na bar aliyoipendelea zaidi ilikuwa ni SIMBA KAPAKATWA.

Alikuwa anaweza akaagiza chakula akala na kujifutia mabaki ya chakula kwenye nguo zake bila hata kunawa mikono. Pia alikuwa anaweza akanywa na kula na kuondoka bila kulipa.

Wengi walinong'ona kuwa mzee PETER TYENYI atakuwa na frustration zilizotokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea katika ndoa yake.

Inasemekana mke wake Bi JOYCE MWAKILAMA, alikuwa akitoka kimapenzi nje ya ndoa na mmoja wa mawaziri wa serikali ya JK.
Mwanamke huyo alikuwa mjamzito na PETER hakuutambua kabisa ujauzito huo.

Kutokana na haya mzee PETER alitengana na familia yake ambapo yeye alikuwa akiishi kwenye nyumba za wanausalama mlemle KIJITONYAMA huku mkewe na watoto wakiishi kwenye nyumba yao maeneo ya SINZA.
Hata hivyo mzee PETER alikuwa akiwatembelea wanae mara kwa mara. Endelea hapo chini >>>>> click here to unlock the post

Buyobe
Buyobe @Buyobe

*_UTAJIRI WA PESA ZA "NDAGU"._*

Mwaka huu mwanzoni nilikuwa mkoani Arusha kwa jamaa yangu mmoja tuliyetoka nae Kijiji kimoja huko mkoani kwa baba wa taifa.

Siku moja katika matembezi mjini na huyu jamaa yangu, Ghafla nikasikia naitwa jina langu kwa kilugha changu na mchoma mahindi aliyekuwa pembeni yetu "Requal, Omwanono Ge zisiku ndola ukulili igo" nikashangaa kidogo maana alikuwa mmama wa makamo na sikuweza kumkumbuka kabisa. Ikabidi nimjibu "Mazomu", baadae akahamia kwa jamaa akawa anamuuliza umempata wapi huyu kiumbe maana sijamuona zaidi ya miaka 10, katika maongezi ndio nikaja kugundua ni Sarah, sio jina sahihi (Jirani yangu kabisa kule kijijini) ni kweli hatujaonana miaka 10 na zaidi.

Ule urembo wake umeisha kabisa na sasa anaonekana kama bibi yangu japo amenizidi miaka 4 tu ya kuzaliwa.Kiukweli alikuwa amechoka sana na alionekana mtu aliyekata tamaa na maisha kabisa na hapa ndipo nilipoona Kuna haja ya kuweka hapa huu mkasa ili wengine wajifunze.

*_STORY YA FAMILIA YA AKINA SARAH._*

Sarah ametoka familia ya watoto watano pale kijijini kwetu, wa kike wawili na wakiume watatu, mkubwa tumpe jina Joseph, anaefuata wa kiume "nyanza", na wa mwisho wa kiume aitwe "Gedo". Hiki kisa kinamhusu zaidi Sarah, Gedo, mama yao pamoja na mume aliyekuja kumuoa Sarah. Kabla hatujafika huko tutamzungumzia kidogo Joseph ili kupunguza maswali huko mbeleni.

Baba yao Sarah alikuwa na wake wawili na mama yao Sarah hakuwa kipaumbele Cha baba yao, mke mdogo ndiye aliyependwa zaidi na familia ya mke mkubwa ni kama ilitelekezwa vile.

Baba yao Sarah alikuwa na ndugu mmoja tu wa tumbo moja wa kiume na wa kike mmoja pia walipenda sana. Hawa wazee ilikuwa ni mfano kijijini pale kwa jinsi walivyokuwa wanapendana. Huyu wa kiume ambaye ni baba yake mkubwa Sarah alikuwa na wake wawili na mke mkubwa alikuwa anasadikika ni mchawi mkubwa sana pale kijijini; anasadikika kufuga misukule Kule kijijini watu wanamuogopa mno tukikutana nae porini mwenyewe huwa tunajificha ili apite, huwa havai viatu akitembea na haachi unyao anapokanyaga. Naye atahusika kidogo kwenye huu mkasa.

*_MKASA WA JOSEPH._*

Joseph ni mtu mzima kidogo amezaliwa miaka ya 70's, huyu jamaa ana asili ya roho nzuri sana, mcheshi na mkarimu mno alikuwa family friend wa ukoo wetu, alioa mwanamke mrembo sana kutoka Kijiji cha jirani yule mke hata ukikutana nae leo ni vigumu kujua Kama ile ni product ya kijijini. Endelea hapo chini. >>>>> click here to unlock the post

Buyobe
Buyobe @Buyobe

*_ASKARI MSTAAFU ALIYEKUWA ANANYONGA WATU GEREZA LA ISANGA -DODOMA._*

Kifo kinatisha; kifo hakina huruma; kifo hutenganisha wapendanao, lakini kwa bahati mbaya, siku ikifika hakuna anayeweza kukikwepa.

Akionyesha hofu ya kifo alipokuwa na bendi ya Orchestra Makassy, Remmy Ongala aliimba kibao kinachoitwa “Siku ya Kufa”. Maudhui ya kibao hicho yalirejewa na Remmy mwenyewe japo kwa mahadhi tofauti alipojiunga na bendi ya Super Matimila. Huko alitunga kibao kiitwacho “Kifo Hakina Huruma”.

Kana kwamba ana uwezo wa kufanya majadiliano na kifo aliimba: “Kifo, kifo, siku yangu ikifika eeh, kifo niarifu mapema, niage wanangu, niage familia yangu yote, pesa zangu nizigawanye, zimebaki nizile mwenyewe, kifo nakusubiri kwa hamu.”

Mwanamuziki huyo, aliyefahamika zaidi kwa jina la Dk Remmy, alifariki dunia akiacha kifo kikiendelea kuchukua uhai wa mamilioni ya watu duniani katika mazingira tofauti. Baadhi hufa ghafla ajalini, wapo wanaofariki dunia baada ya kuugua, wengine huuawa na wenzao kwa hasira au kisasi au kwa bahati mbaya au bila kujua, lakini kuna wanaouawa kwa hukumu inayotolewa na vyombo vya haki; huhukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Wanaopatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia huhukumiwa kifo. Japokuwa kila nafsi itaonja mauti, wanaohukumiwa kifo ndio huweza kujua siku na aina ya kifo.

Hivi mtu akihukumiwa kifo na mahakama, je, wanaofanya kazi hiyo ni nani? Kitanzi kikoje? Hali inakuwaje kabla? Je, hupata fursa ya kuaga ndugu na jamaa? Wanaotekeleza hukumu ya kunyonga wenzao hadi kufa pia wanakuwa wametenda kosa la kuua, je, huchukuliwa hatua gani kisheria? Je, wanaoajiriwa kufanya kazi hiyo wanapatikanaje? Wanajisikiaje kukatisha uhai wa wenzao?

Lakini pia katika utumishi wao, ufanisi wao unapimwaje? Je, hupata utulivu wa moyo na amani kiroho?

Kwa kawaida kazi nyingi hutangazwa wazi magazetini na wale wanaojiona wana sifa zinazohitajika, huandika barua za kuomba na kusubiri kuitwa kwa mahojiano. Lakini, ni vigumu kukutana na tangazo la kazi hii ngumu kuliko zote.

Pia, najua kwamba baadhi ya kazi huhitaji wasomi wa kiwango cha juu, nyingine watu wenye ujuzi fulani lakini zipo zinazohitaji wenye nguvu.

Binafsi nadhani kazi hii inahitaji watu wenye moyo wa ujasiri ambao hawawezi kukosa utulivu wa moyo wala amani kiroho wakitekeleza jukumu lao kwa watu waliohukumiwa kifo.

Maswali hayo na mengine mengi nimekuwa nikijiuliza kwa siku nyingi na katika kufuatilia nililazimika kufunga safari hadi mkoani Dodoma ambako nilifanikiwa kumshawishi mtekelezaji wa hukumu hizo afanye mahojiano nami.

Saa 12.00 jioni, nikiwa na mwenyeji wangu wa Dodoma tulifika nyumbani kwa mtu tuliyekuwa tukimtafuta, Anangisye (siyo jina lake halisi). Endelea hapo chini. >>>>>>. click here to unlock the post

Buyobe
Buyobe @Buyobe

*_UJASUSI NDANI YA BOEING._*

Kampuni kubwa ya kutengeneza ndege Duniani ya Boeing yenye makao makuu yake Illinois Chicago Marekani imekumbwa na msukosuko wa ndege zake toleo jipya kabisa aina ya 737 MAX 8 kupata ajali mara tatu.

Kampuni ya Boeing imeajiri wafanyakazi zaidi ya 153,000 na gross profit yake kwa mwaka ni zaidi ya $Bil 25.

Washindani wa kampuni ya Boeing kibiashara ni Airbus yenye makao makuu yake Leiden Netherlands na imeajiri zaidi ya wafanyakazi 120,000 na gross profit ya kampuni hii ya Airbus kwa mwaka ni zaidi ya $ Bil 10.

Kampuni zingine zinazofuatia kwa ushindani na Boeing ni ya Antonov ya Ukraine na ya Beriev ya Urusi.

Kampuni zote hizo zinatengeneza ndege tofauti zikiwemo za kijeshi, za mizigo na Kwa wingi za abiria.

Ktk Dunia hii ilivyojaa ushindani wa kibiashara ni wazi kwamba kampuni zingine lazima zione wivu Kwa kazidiwa kibiashara na Boeing.

Boeing ndo kampuni pekee inayoaminika Ktk kuunda ndege imara zaidi na za kuaminika kuliko kampuni zote.

Hapa ndo ujasusi unapotumika ili kuizamisha kampuni husika iogopwe na wateja wake.

Ili taifa lolote lisonge mbele kiuchumi ni lazima ujasusi wa kiuchumi ufanye kazi yake ipasavyo.
Kenya imetumia sana ujasusi wa kiuchumi ili kupaa juu na kweli imefanikiwa ktk hilo ,China pia, India, Malaysia na US ndo inaongoza Duniani ku apply ujasusi wa kiuchumi.

Pamoja na uwezo mkubwa wa CIA lakini imeshindwa kubaini mapandikizi ya majasusi walioajiriwa Kipindi kirefu ndani ya Boeing ili kuihujumu kiuchumi, haikuwa rahisi kwa kampuni kubwa Kama Boeing kutengeneza ndege zenye hitilafu kubwa kwenye injini na kisha kuzipeleka sokoni.
Endelea hapo chini >>>> click here to unlock the post

Buyobe
Buyobe @Buyobe

_*HISTORIA YA KWELI JUU YA MAISHA LE MUTUZ.*_

*_Sehemu ya (1--4)*

_Anasimulia Le Mutuz,_

Safari yangu ya USA ulikua ni uamuzi wangu mgumu wa kuacha Ubaharia nikiwa Melini "MV. Luxemburg"ICMB Belgian Shipping Line tukiwa South China Sea tunatokea Shanghai/China tunarudi Singapore kazi yangu Melini nilikuwa Assistant Engineer au 0fisa wa Meli ndani ya Meli.

Maisha ni kwa grade and class Maofisa mnaishi sehemu maalum na mnakula sehemu maalum na mna hang out sehemu maalum sheria za Meli hamtakiwi kuchanganyikana na Crew yaani Mabaharia wa kawaida infact hata Chakula ni tofauti Maofisa mnakula vizuri sana kuliko Mabaharia ...

l was a lucky man cause nilikuwa ninasoma Chuo Kikuu Cha Ubaharia Zeeman Marine Engineering College/Antwerpen, Belgium ambako nilijiunga nacho Miaka 4 na huu ulikua Mwaka wa Tano ninamalizia Leseni ya Uinjinia wa Meli ambayo ni Equivalent to Degree cause Melini zamani hakukuwa na Degree ila Leseni Only na Masomo ya Meli ni kila Miezi 6 Darasani na Miezi 6 unasafiri kufanya kazi Melini so by Mwaka wa Tano nilikuwa Baharia wa Ukweli nimetumia like 3 Years Baharini ambayo Practically katika Ubaharia inaitwa "SEA TIME" ambayo inaheshimika sana unapoamua kuomba kazi mpya ya Ubaharia Kampuni nyingine ndani ya Meli.

Nilikuwa na Bosi wangu Engineer Feyerick Mzee aliyekuwa anavuta Cuban Cigar all the times binafsi nilikua sinywi Pombe wala kuvuta sigara hii ilinifanya kuwa Baharia maarufu sana ndani ya ile Melicause kila ljumaa tulikuwa tunapewa mgao wa Meli Katoni 5 za Beer, Katoni 2 za Sigara na Chupa 2 za Pombe Kali bure mimi nilikuwa always nabadilishana na Maofisa wengine wao wananipa Juice na Soda ...

Mzee Feyerick alikuwa na tabia ya kukaa chini na kunipa darasa kuhusu Maisha nilikua kijana mdogo sana infact nilikuwa nimeichezea Miaka yangu kwenye makaratasi nikisaidiwa sana na Mwili Mkubwa lakini hata hivyo sura yangu ilikua inani betray always kuwa ni mdogo so nilikuwa natembea na Kitambulisho all the times ...

Kama kawaida Mzee Feyerick my Bosi wa Engine Room alinikumbusha sana kwamba Kijana mdogo achana na hii kazi ya Ubaharia haikufai Nchi Kavu kasome utafute maisha bora ya kisasa", maneno mazito yalinigusa sana

My Boss Mbelgiji Feyerick alikua ananiambia the bitter truth kua niachane na mambo ya Meli akaniambia "Hii ni kazi ya Wazee na watu wasiokuwa na Maisha sio kwa kijana kama wewe" in all my childhood.

Nilikuwa naulilia Ubaharia nilianza nikiwa Jamhuri Primary School nilipokutana na "MABAHARIA WA NCHI KAVU" yaani Wanafunzi wenzangu Darasani kina Juma Jagan Burr (now in Canada) na Marehemu Raja Kaka hawa ndio Wanafunzi 2 walionipa the idea ya Ubaharia cause walikuwa na ndugu Mabaharia ambao walikuwa wakiwasaliana nao sana kutoka Nje l was in yaani "BAHARIA NCHI KAVU" Baba yangu mzazi then alikuwa Waziri wa Kilimo he was stunned kusikia kua nina mawazo ya kua Baharia alianza kusikia kutoka kwa marafiki zake ambao nilikuwa nawasumbua sana

Endelea hapo chini >>>> click here to unlock the post

Buyobe
Buyobe @Buyobe

_*HISTORIA YA KWELI JUU YA MAISHA LE MUTUZ.*_

*_Sehemu ya (5-8) *

_Anasimulia Le Mutuz, click here to unlock the post

Buyobe
Buyobe @Buyobe

*_HAYATI DR. SHIKA USIYEMJUA._*

*_Sehemu ya kwanza._*

Lancefort Ltd ni kampuni iliyosajiliwa nchini Russia miaka kadhaa iliyopita, na kwasasa haifanyikazi kwa kipindi kirefu baada ya watendaji wake kupotea gafla kwa mazingira ya kutatanisha.

Kutoka mjini Rostov on don napokaa mpaka Moscow ni mwendo mrefu kidogo ambao ni km 1200 na zaidi, kwa mwendo wa trein ni 5hrs,
nimefika mjini moscow na kuanza kuuliza hasa legality ya kampuni hiyo ndani ya moscow na Urusi kwa ujumla, nimefanikiwa kupata maelekezo ya kukutana na Mtanzania mmoja anaisha mtaa wa Tverskaya Street, ambaye kanikaribisha na kuanza kufanya uchunguzi wangu, nikaamua kwanza nipate hifadhi ndani ya hotelya Sputnik.

Baada ya kwenda kwa watanzania wanaoishi huku nimegundua huyu mzee alipata matatizo kwa kuhisiwa ni spy wa Marekani, ambaye kapandikizwa kutokea Afrika, na amekuwa akitafutwa na kufuatiliwa nyendo zake zote kuanzia kwenye kampuni yake na nyumbani alipokuwa anaishi.
Mke wake bi Luisa Kvonkov ndo alibanwa na kueleza kwao ni Tanzania Magu, Lakini inasemekana kwamba kuna kampuni kubwa la kimarekani aidha shirika la upelelezi ambalo liko nyuma ya kampuni ya Lancefort, ndio chanzo cha kutiwa msuko suko huko alikokuwa anamiliki kampuni hiyo.... Endelea hapo chini. >>>>> click here to unlock the post

Buyobe
Buyobe @Buyobe

>>>>>>>>>>>>MAUAJI SONGEA<<<<<<<<<<<<

WHO WAS THE MURDERER? A lifeless body in the bush With a notebook on it's chest With a fatal wound on it's forehead The Accused denied the traces left This MURDER is mysterious. UZI >>>>>>.>>>>

#SimuliziZaBuyobe

MAUAJI SONGEA

Tukio lilianza kama kesi ya mtu kupotea... SHOLASTIKA NUNGU alikuwa akiishi na mumewe REGNATO MAPUNDA maeneo ya MUUNGANO kijiji cha ZOMBA mkoani SONGEA.

Jumapili tarehe 19 MARCH 2017 majira ya saa nane mchana REGNATO alimuaga mkewe kuwa anatoka kidogo. REGNATO alimwambia mkewe kuwa anakwenda kuangalia mechi ya mpira iliyokuwa inachezwa kijiji jirani cha LUGAGALE.

Huku nyuma, SHOLASTIKA aliendelea na shughuri zake za nyumbani ikiwemo kupika. Ilipofika majira ya saa 12 jioni aliwaaga watoto kuwa anatoka kidogo atarudi punde. Majira ya kama saa 2 au 3usiku REGNATO alirudi nyumbani lakini mkewe hakuwepo...Endelea hapo chini. >>>>>> click here to unlock the post