by Marley Digital

SABABU 5 ZA KUTUMIA CLUBZILA KUCHAPISHA MAUDHUI YAKO

05 Feb, 2023

SABABU 5 ZA KUTUMIA CLUBZILA KUCHAPISHA MAUDHUI YAKO.
Clubzila ni nini? 
Clubzila ni jukwa maalum linalomuwezesha muandaa maudhui au creator kuuza maudhui yake mtandaoni kwa maelezo zaidi    BOFYA HAPA. Zifuatazo ni faida za kutumia mtandao wa clubzila kuchapishia maudhui yako.
Udhibiti wa maudhui.
  • Moja ya faida kubwa ya kutumia clubzila Kama jukwaa lako pendwa la kuuzia maudhui , Clubzila inakuwezesha kuuza maudhui yako kwa mtu mmoja mmoja, sio kwamba ukiuzia mtu mmoja anaweza kuipakua na kuisambaza kwa watu wengine  na kwa kiasi flani inapunguza kipato cha muandaa maudhui,hivyo clubzila imeandaa namna ambayo muandaa maudhui anaweza kuweka maudhui yake mtandaoni nayule anaelipia ndiye anaweza kupata maudhui hayo kwa Kuingia kwenye ukurasa wako wa  clubzila na sio tu kwa kupakua  maudhui baada ya kufanya manunuzi. 

Kuingiza kipato kupitia maudhui yako.
  • Muundo wa jukwaa (platform) LA  Clubzila ni kwamba muandaaji wa maudhui amepewa nafasi ya kipekee ya kuipa thamani Kazi yake, kutokana na uzuri wa Kazi zako yule ambae atavutiwa na akapenda kufuatilia maudhui yako Hanabudi kulipia gharama uzlizoziweka ili aweze kupata maudhui pendwa kila utakapoweka Kazi mpya. 
Kuza soko lako(uza nje ya nchi).
  •  Miongoni mwa malengo ya clubzila ni kukua ndani na nje ya Tanzania, kama ilivyo kwa clubzila kwamba haya ni malengo yetu, basi inakupasa pia wewe creator ndani ya clubzila kuwa na maono hayo, na kuongeza juhudi katika kuandaa Kazi nzuri, ambazo zitapelekea soko lako lisiwe Tanzania tu Bali hata nchi nyingine barani Africa 
Pata ushauri wa kitaalamu.
  • Kwa kutumia clubzila utapata ushauri ni namna gani uiandae Kazi yako iwe yenye kuvutia na yenye muonekano wa ufanisi ili watu waweze kuvutiwa na kuipenda Kazi yako.na kwa namna hii itakuongezea uwezekano wa kupata wafuasi wengi zaidi na vilevile kipato kitaongezeka. 
Urahisi wa kuuza kazi zako
  • Kutokana kwamba clubzila inatembelewa na watu wengi wenye kuvutiwa na Mada tofauti tofauti, ukiwa kama creator mwenye Kazi zilizoandaliwa kwa ufanisi Kuna uwezekano mkubwa watu kuvutiwa na kile unachokifanya na hivyo kua na nafasi ya kufanya mauzo kemkem. 
Ongeza thamani ya brand yako.
  • Kama tulivyo ona hapo juu, Clubzila itakusaidia kukuza soko lako ndani na nje ya nchi hivyo Clubzila inauwezo wa kukuza brand yako ikiwa kama wewe unatoa huduma mtandaoni au kwa kupitia clubzila unafanya biashara za bidhaa tofauti tofauti,kuna uwezekano mkubwa wa huduma na bidhaa zako kuonekana na watu wengi na kuvutiwa watu wengi zaidi na kwa namna hiyo ni rahisi kukua na kupata maendeleo katika kile unachokifanya Kazi 

Sioni SABABU ya wewe kuchelewa kujiunga na mtandao huu  mkubwa wa clubzila, kama bado hujajiunga tembelea tovuti hii Clubzila na uanze kuvuna matunda ya ufanisi wako. 
 
Others posts
  • CLUBZILA NI NINI? JINSI YA KUTUMIA KUCHAPISHA MAUDHUI YAKO @Marley Digital - 29 Oct, 2022

    Clubzila ni jukwaa digitali (digital platform) inayokuweze...

  • FAHAMU MTANDAO WA CLUBZILA @Marley Digital - 04 Mar, 2022

    CLUBZILA. Clubzila ni mtandao unaowezesha mtumiaji kuwe...