by Marley Digital

FAHAMU MTANDAO WA CLUBZILA

04 Mar, 2022


CLUBZILA.
Clubzila ni mtandao unaowezesha mtumiaji kuweza kuuza maudhui yake ya kidigitali (maandishi,picha,video,faili,matukio mubashara(live streams,) kwa urahisi zaidi.
WALENGWA.
Watengeneza maudhui ambao maudhui yao yana thamani pamoja na mashabiki wa watengeneza maudhui
AINA ZA MAUDHUI.
MAANDISHI
AUDIO
VIDEO
PICHA
LIVE STREAMS
ZIP FILES-PDF,E BOOKS,ETC

MITINDO YA MAUZO.
Ifuatayo ni baadhi ya mitindo ya malipo muuza maudhui anaweza kutumia kuuza maudhui yake ndani ya platform ya Clubzila.
Kupitia Clubzila, muuza maudhui anaweza kuamua kuuza maudhui yake kwa mtindo wa malipo ya Ada ya  kila mwezi.
Mchapisha maudhui anaweza kuweka gharama (bei/ada)ambayo mtu atahitajika kulipia kwa mwezi ili aweze kua mfuasi wake na kuweza kuona maudhui yake anayoyachapisha ndani ya mwezi huo, pindi mwezi utakapoisha,mfuasi atahitajia kulipia tena ili aweze kuendelea kupata maudhui yale. Clubzila inampa mchapishaji uwezo wa  kuuza maudhui moja moja (individual content).kwa gharama utakayoweka mwenyewe. Yaani,unaweza kuamua ,ili mtu aweze kuona nakala fulani anahitajika alipie gharama ya mara moja ya kiasi cha pesa alichoweka muandaa  maudhui, na kwa mtindo huu,maudhui hayo yataonekana kwa wale watu watakaolipia ile gharama pekee, na sio kwa wengine. Wewe kama muandaaji maudhui,kuna watu wengi sana wanaopenda kazi yako na kunufaika nayo na kupelekea wao kua tayari kuunga mkono  juhudi zako. Clubzila ina chaguo linaloruhusu mtu kuunga mkojo  maudhui yako moja kwa moja kwa ku “TIP” katika ukurasa wako ,kama sehemu ya kuthamini juhudi na  maudhui yako.
Kama wewe ni muandaaji wa maudhui ya video za moja kwa moja(live streaming),platform ya clubzila inakuwezesha kuweza kurusha maudhui yako moja kwa moja kwa walengwa wako,lakini pia, Clubzila imekuongezea uwezo wa kuuza maudhui hayo kwa urahisi zaidi kwa kuweka gharama unayotaka walengwa wako walipie ili waweze kuungana na wewe kwenye live stream yako.

JINSI YA KUJIUNGA NA KUTUMIA CLUBZILA.
Katika platform unaweza kujiunga kama mtumiaji wa kawaida au mchapisha maudhui.Mtumiaji wa kawaida anakua na uwezo wa kuona maudhui ya wengine(creators)   
Kwa kufuata hatua hizo , utakua umekamilisha utaratibu wa kujiunga na jukwaa la Clubzila kama mtumiaji. Baada ya hapo ni vyema ukaenda kwenye sehemu ya kuhariri ukurasa wako, nakujaza taarifa zingine zinazikuhusu pamoja na kuweka  picha yako kwenye profile yako ili iwe rahisi kwa watu kukutambua

JINSI YA KUCHAPISHA MAUDHUI.

Ili kuchapisha maudhui kwenye jukwaa, inabidi kwanza uwe umejisajili (kama ilivyoelezwa hapo juu), hakiki akaunti yako kwa kupakia(upload) kitambulisho chako. Baada ya kufanya hivyo utasubiri kwa  muda usiozidi saa 24 akaunti yako itakua imehakikiwa, na utakua tayar kwaajili ya kuanza kuchapisha maudhui.
KUCHAPISHA MAANDISHI
Kuchapisha maandishi ni rahisi, unachopaswa kufanya ni kuhakikisha upo katika ukurasa wa nyumbani (home page),na utaona sehemu inayokuruhusu wewe kuweza kuanza kuandika. Tumia sehemu hiyo kuchapisha maudhui yako.
KUCHAPISHA PICHA&VIDEO NA SAUTI (AUDIO).

KUCHAPISHA ZIP FILES
Unaweza kuchapisha zip files kwa kubofya kitufe cha zip files kama inavyoonekana katika mfano hapo. Kisha,chagua zip file unayotaka kuchapisha kisha ,bonyeza kitufe cha kuchapisha.

KUCHAPISHA LIVE STREAM
Ili kufanya live stream ya kulipia, Nenda kwenye sehemu ya kuchapisha maudhui, kisha bonyez kitufe cha alama ya mawimbi,seti bei ya live stream yako(kiasi unachotaka watu walipie)na uanzishe live stream yako.
JINSI YA KUTOA PESA
Bofya alama ya profile yako
Bofya "dashboard" 
Bofya "withdrawal" 
Weka  kiasi unachotaka kutoa
Bofya "withdrawal"


JINSI YA KUSHARE LINK YA REFERRAL

Bofya alama ya profile yako
Bofya" referral "
Copy referral link yako, Tuma kwa uwapendao wajiunge kupitia link yako, ili upate commsion ya hadi 10% ya faida inayopatiakana kutokana na watu waliojiunga kupitia link hiyo.

JINSI YA KUNUNUA MAUDHUI 1)ukichagua wallet kama njia ya malipo na kama una salio la kutosha kwenye wallet,basi itakamilisha malipo moja kwa moja.
2)ukichagua mobile money kama njia ya malipo, itakuletea ukurasa wa kujaza namba za simu,kisha itakuletea  maelekezo ya mtandao.
NAMNA YA KUWEKA PESA KWENYE WALLET
WALLET Ni akaunti yako ya kidigitali ya mtandao wa clubzila inayokiwezesha kuhifadhi pesa zako na kuweza kuzitumia kwa haraka zaidi na kwa muda wowote pale unapohitaji. Namna ya kuweka pesa :
  • Bofya wallet
  • Weka kiasi unachotaka 
  • Bofya "add Funds"
  • Weka namba ya simu
  • Weka namba ya siri



JINSI YA KUTIP
TIP (pesa ya shukrani) ni kiasi cha pesa unachomtumia mchapisha maudhui kama sehemu ya kumpa motisha kutokana na kazi nzuri aliyoifanya.. 
  • Bonyeza" Tip"
  • Weka kiasi
  • Chagua Namna ya malipo

1)ukichagua wallet kama njia ya malipo na kama uko na salio la kutosha kwenye wallet,basi itakamilisha malipo moja kwa moja.
2)ukichagua mobile money kama njia ya malipo, itakuletea ukurasa wa kujaza namba za simu,kisha itakuletea  maelekezo ya mtandao.

JINSI YA KUJIUNGA NA VIDEO MUBASHARA( LIVE STREAM
JINSI YA KUMTUMIA MTU UJUMBE. “Hakikisha mmoja wenu amesubscribe kwenye page ya mwenzake ili muweze kutumiana ujumbe.
JINSI YA KUONA MAPATO Taarifa zote muhimu za mapato utaziona hapo
JINSI YA KUONA SUBSCRIBERS WAKO Taarifa zote muhimu kuhusu idadi ya wafuasi wako utaziona hapo
JINSI YA KUONA WAANDAA MAUDHUI ULIONUNUA MAUDHUI YAO Taarifa zote muhimu kuhusu kurasa za maudhui ulizojiunga nazo utaziona hapo

JINSI YA KUONA MIAMALA ULIYOIFANYA Taarifa zote muhimu kuhusu malipo/miamala uliyoifanya utaziona hapo

JINSI YA KUZUIA NCHI NA MTU MMOJA MMOJA Jaza nchi unayotaka kuifungia, kisha hifadhi/save
.
JINSI YA KUWEKA PROFILE PICTURE
JINSI YA KUWEKA COVER IMAGE Bofya sehemu ya" change cover", kisha pakia picha yako
NAMNA YA KUWEKEA ULINZI AKAUNTI YAKO
  •  Bofya alama ya profile yako
  • Bofya my page 
  • Bofya edit my page
  • Bofya menu
  • Bofya privacy and security 

Utapata chaguzi tofauti,chagua unachohitajia juu ya akaunti yako




 
Others posts
  • SABABU 5 ZA KUTUMIA CLUBZILA KUCHAPISHA MAUDHUI YAKO @Marley Digital - 05 Feb, 2023

    SABABU 5 ZA KUTUMIA CLUBZILA KUCHAPISHA MAUDHUI YAKO. Clu...

  • CLUBZILA NI NINI? JINSI YA KUTUMIA KUCHAPISHA MAUDHUI YAKO @Marley Digital - 29 Oct, 2022

    Clubzila ni jukwaa digitali (digital platform) inayokuweze...